Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini Hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu... Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy [emoji4]View attachment 1722606
Unauza urojo na ukwaju?
 
Biashara yangu ina copyright issues hivyo samahani jamani sitaitaja maana naifanya mwenyewe tu huku Zanzibar watu wengine bado hawajapata mechanism ya kucopy.

Na soon baada ya wao kucopy nahamia kwenye phase 2.

Mtanisamehe! [emoji120]
[emoji16][emoji16][emoji16]

Nimeshaijua
 
Labda uuze mk*ndu lakini nao huwezi kupata faida kila siku sababu hauuzi daily na at the end utaishia kuoza tu nyuma tu, Mtoto wa kiume ukianza kufikiria masuala ya kuuza mwili mapema mapema inasikitisha saana.

Think deep, usifikirie katika mambo yasiyo na tija.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sasa mkuu wewe unaleta utani na maisha watu tupo mtaani tumepigika, siunaona mtu kaanzisha uzi kama hivi! Maana yake anahitaji msaada, pia wengine wanafaidika kupitia michango ya mawazo inayotolewa,

Unaposema unabiashara ya mtaji mdogo na inakupa faida kubwa, na huisemi, mtu anaona kama unambania au kumnyanyasa kisaikolojia, unatuongezea maumivu mkuu ujue watu tumewahi kwenda kuomba kazi kwenye makampuni ya wageni tukazuiliwa kuingia ndani na wabongo wenzetu,ma secretary wanachana na kutupa barua za maombi ya kazi kwenye dustbin. Kiufupi tunapitia mengi sana mpaka tumejawa na stress inafikia point tunajikuta tukikutana na mtu anayekunyima mchongo kama hivi unakumbuka maumivu yote uliyopitia ya kunyanyaswa na wabongo wenzetu.

Nisamehe sana mkuu niliandika kwa makosa na hasira tu zinazotokana na stress I'm sorry [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Nikuombe kitu kimoja siku nyingine ukitaka kutusaidia ficha location yako alafu eleza wazo lako ili kulinda maslahi yako kama anavyofanya CONTROLA, wengi tutanufaika na Mungu atakubariki [emoji120][emoji120]
Haaahaaaaahaaaaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Biashara ya chakula...sembe kilo 1 linatoa plate 9_10...
Dona linatoa plate 7
Sasa ukatafuta kijiwe ukaspeciliaze kwenye uchomaji nyama mzuri plus mapande...ukatengeneza formula nzuri ya pilipili..yaan ni ugali na nyama na mboga majani na maharage...kwasiku unalaza 20faida...ila wateja wa dona bei sio ya buku...maana dona halivimbi ni hasara kibiashara...
Idea nzuri mkuu ukizingatia vyakula vingi ni same. Ukija na nyama choma asee inaweza kuhit sana.
 
Ndugu zanguni mawazo ndio benki kuu kabisa ya kila wazo unalotaka kufanya, basi kwa uzoefu wa waliopitia changamoto fulani za kiuchumi na kijasiriamali ni vyema mngetushirikisha biashara ndogo ambazo mlizibuni na maeneo mlikofanyia hizo shughuli zenu hadi mkafikia hatua ya na mafanikio mliyo nayo sasa.

Tunatarajia ushuhuda, miongozo na shauri zenu zitusaidie nasi kujikwamua hapa tulipo ili nasi tusogee mahali fulani.
Utanisamehe kama nakwaza, kwasasa mi naona anzisha dini mpya ambayo bado kuanzishwa, hapo umeulaa na kutokelezea mboni
 
HAKUNA BIASHARA ISIYOLIPA KAMA UKIAMUA KUIFANYA KWA MOYO MMOJA NA UKAJIFUNZA, NARUDIA TENA KUJIFUNZA, KWA MARA NYINGINE KUJIFUNZA JINSI BIASHARA HIYO ITAKAVYOKUFAIDISHA NA MBINU ZA KUPATA WAHITAJI WA HUDUMA YAKO.

Nyie manosema biashara ni siri ya mtu basi siri yenyewe ndiyo hiyo hapo.

Usifanye biashara kama huna uelewa nayo. Usifanye biashara kama wateja wako huwajui na hujui wanapatikana wapi.

Usifanye biashara kisa wengi wanasema inalipa.

Usifanye biashara kisa umekutana na idea jamiiforum.

Usifanye biashara kama huna malengo nayo.

Usifanye bishara kama lengo lako ni kupata basic needs pasipo focus ya kufika mbali.

Tambua utofauti uliopo kati ya biashara ya kuanzia kutengeneza mtaji na biashara ya kukufanikisha maishani.

Biashara ni sanaa, inahitaji ubunifu ili kuendelea kuwepo sokoni. Wapo wanamuziki maarufu enzi hizo ila leo hawapo na hatuwasikii, hivi ndivyo biashara ilivyo.

Jifunze principles za biashara na usifanye biashara kisa unao mtaji, kama huna hobby ya business ACHA usiguse biashara na utafute mwenye hobby aendeshe biashara yako.

Mwisho, ukishika biashara moja, komaa nayo mpaka ikutoe ndipo uongeze biashara nyingine.

Narudia tena, kama unafanya biashara kwasasa, hakikisha hiyo biashara imekutoa na ndipo uanze biashara nyingine.

Akili za kuambiwa changanya na zako la sivyo utabaki kuishi NA idea za watu ambazo hujui wao wanazitumia vipi kupata faida kubwa kwenye biashara ambayo wewe unaiona ya kawaida.
 
Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu. Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy [emoji4]

View attachment 1722606
Hujatuambia ni biashara gani, unaturingishia tu mapesa
 
Back
Top Bottom