Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu. Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy [emoji4]

View attachment 1722606

Embu kanunue godoro kwanza kabla hujapeleka bank si kwa uchafu huwo sehemu unayolala puuh
 
Hii idea nilikuwa nayo jana tu hapa. Nilitaka kuweka laki 6 kwenye kakibanda ka chips baada ya kufatilia nikaona miyeyusho kwanza vibanda vingi na chips zina usumbufu. Nikafikiri nikiweka pungufu ya hiyo kwenye kibanda cha mamantilie si napata hela ingawa siwezi kamwe kufanya hiyo kazi mpaka niweke wadada.

Bado niko dilemma.
Kibanda cha chips shida wapishi walevi kinoma
 
Safi saana! Think deep it ain't illegal yet.

Mimi ilikuja Kama zali tu. Sikuplan Mara ghafla Kama nilionyeshwa kitu ba malaika. Nikapata wazo nikalitekeleza kimya kimya next day faida laki. Wahoooo!
Nije chemba unishirikishe bas, sipo zenji nipo pande nyingine kabisa
 
Well..biashara hiz lazima ujitambue ni mfumo gan utatumia...mfano kwa sisi ambao hatuwez kaa hapo kwenye biashara sabab ya majukum mengne..lazima ufikiri kwa kina sana ni biashara gan ambayo ni self managing.yaan unamweka kijana yeye anakupa hesab tu..precisely isiwe na makando kando kama biashara za boda au bajaj etc...hapo akili lazima itulie

Ila kwa mtu ambae anakaa mwenyew golin aisee zipo biashara nying sana znaweza kukupa hyo hela kwa siku...

Ni kuchangamsha ubongo tu..uliza sana watu.angalia sana wenzio wanafanya nin..pita ma youtube utapata kitu tuu

Ila angalau icheze faida from 20-50 % ikiwa zaid bas kheri

Yaan angalau ukiweka mtaj wa 1m...ikupe faida ya 200k minimum..iwe siku.week or mwez...ukiwa na branchez nying ...unakunja hela ya maana tu per week...ila ndo hvyo kama hukai golin bas buni somethn self managing...hapo ndo huwaa anajulikana Mwenye akili na anaekariri...hapo gpa zinaachwa huko mbali.
 
Nimeuza viazi vya mafungu na kwenye sado pale Temeke sterio sokoni apo nipo chuo udsm mwaka wa pili dah afu najishangaa hata nilikua sioni haibu..lkn leo marafiki zangu ndio wanulizia ile biashara mana ninayofanya saivi ni tofauti na matarajio yao .thanks god kwa kidogo ninachopata
Msomi wa Udsm kweli Aibu aiandike HAIBU?,Nina wasiwasi sana na hii coment
 
Mimi sifanyi biashara mkuu,Mimi naunganisha mteja na mfanyabiashara.
Hiyo nayo ni biashara mkuu. Kutoa huduma na kuuza bidhaa zote ni biashara. Biashara kama yako kutunza siri ni sehemu muhimu lakini haiwezi kuzuia kushare na wengine idea yako (sina maana lazima uiweke hapa).

Nimefanya biashara ya kuuza digital products kama vile vitabu na makala mbalimbali. Wateja wangu wote nawapata online na nilikuwa nauza mpaka 180,000 kwa siku, sometimes hali ikiwa mbaya ndani ya wiki na nusu kupata 250,000 ilikuwa jambo la kawaida.

Hapo nimetoa idea ila namna ya uendeshaji wa shughuli hiyo unahitaji mbinu fulani ambazo kwa kawaida zinahitaji kujituma sana na kuwa mbunifu.

Hapa kwa asilimia kubwa tunapata ideas tu ila mbinu za utekelezaji mpaka kupata matokeo husika ni wewe mwenyewe na jitihada zako pamoja na ubunifu. Unaweza pewa idea nzuri yenye faida ila communication skills yako upande wa biashara ikawa mbovu, hapo lazima utafeli.

Mtu atakupa idea ya biashara ila kuna mengine watu tunazidiana. Mwingine anaishi wateja walipo, ila mwingine wateja wake wako mbali na gharama za kuwafikia zinakuwa kubwa, mwingine yeye biashara imemvutia ila hajui wapi wateja walipo. Swing kila kitu kipo karibu yake ila anakosa kujiamini tu ili achukue bidhaa ampelekee mteja.
 
Premier bet buku saba unapata ukiuza laki moja.....sasa ivi raia hawana ela mie nilikua nauza laki nne per day mpaka tano wikiend sasa ndio balaa nagonga laki nane mpaka 1M.......nilikua na mashine mbili moja ya vibosile kuanzia mkeka wa buku kumi na kuendelea hawa walikua balaa mtu anakuja na laki tatu anatoa mkeka mmoja tu mashine nyingine ya hawa wenzangu na mie mikeka ya jero buku mpaka buku tisa.....

Nilikua nafunga kijiji balaa pale mtaani nikikosekana masaa tu natafutwa kwenye simu na wafanya biashara wa lile eneo huwa wananiambia nasie tunauza vinywaji na vyakula sana kupitia wewe mimi mwenyewe sikuwahi kuwaza kabisa kama kuwa kwangu pale ni faida kwa wengine......

Nilisoma chuo miaka mitatu kupitia ile biashara nilimaliza 2015 kizaazaa alipoingia huyu bwana wateja wakaanza kupungua mdogo mdogo mwishowe hakuna kabisa umeuza sana laki tena wikiendi kufika 2017 mwishoni nikafunga rasmi biashara........
Dah "huyu jamaa" aendeelee kupumzika kwa amani tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom