Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Kupitia Uzi huu Kama Kuna mtu yupo dar na anataka tushirikiane kwenye biashara ya ujasiriamali ikiwemo :


Kuuza maziwa fresh /mtindi

Kuuza chakula

Chips..

Nipo tayari zama dm nikupe contact zangu
Kabla ya kuzama pm, iyo biashara ndo tunaenda kuijadili namna ya kuifanya na kuitafuta soko? Nataka kufahamu upo stage gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini Hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu... Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy [emoji4]View attachment 1722606
Biashra gani hyo kwa mtaji juu utengeneze one laki
 
Yani hapa niko nasolve hiki kitendawili,nikipata majibu tu.Mimi tajiri.
Tupo pamoja sema ni ngumu kukitegua maana hatupo zenji

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchawi ni ku Brainstorm tu anza General kuangalia Sector(Industries) zote chambua moja baada ya nyengine mpaka utapata kitu kimoja then kakifanyie Field Study.

Hakuna kitendawili hapo mtaji wa 250K mkubwa sana kukupa 1M kwa mwezi na ikawa 3M ndani ya miezi mitatu.

Kuna jamaa kariakoo ukiangalia mtaji wao hauzidi 100K wanfikisha hiyo 1M+ kwamwezi...katika field observation nilizofanya ndani ya dakika 20 nilizokuwa napata huduma hapo wameingiza mauzo ya 5000 na bidhaa 50+ zipo prepared kuuzwa, bidhaa wanayouza ina Profit margin ya ½ kwa ½ na mtaji.

Mimi kwasasa nimeamua kukaa kimya nitapaza sauti nitapojenga misuri yangu zaidi.
 
Kupitia Uzi huu Kama Kuna mtu yupo dar na anataka tushirikiane kwenye biashara ya ujasiriamali ikiwemo :


Kuuza maziwa fresh /mtindi

Kuuza chakula

Chips..

Nipo tayari zama dm nikupe contact zangu
Hapo kwenye chips nifafanulie kidogo
 
Unauza maziwa gani ya kupima au ya pakiti ya viwandani kama ya viwandani nenda pale kariakoo msimbazi stand ya mbagala utachokiona kikopi kama kilivyo au utajua utajiongeza vipi.
Maziwa ya ngombe mkuu haya ya kukamuliwa daily
Mi naishi kibaha ila nikipata sehemu ya kuyauzia kkoo sishidwi kuja huko daily
 
Premier bet buku saba unapata ukiuza laki moja.....sasa ivi raia hawana ela mie nilikua nauza laki nne per day mpaka tano wikiend sasa ndio balaa nagonga laki nane mpaka 1M.......nilikua na mashine mbili moja ya vibosile kuanzia mkeka wa buku kumi na kuendelea hawa walikua balaa mtu anakuja na laki tatu anatoa mkeka mmoja tu mashine nyingine ya hawa wenzangu na mie mikeka ya jero buku mpaka buku tisa.....

Nilikua nafunga kijiji balaa pale mtaani nikikosekana masaa tu natafutwa kwenye simu na wafanya biashara wa lile eneo huwa wananiambia nasie tunauza vinywaji na vyakula sana kupitia wewe mimi mwenyewe sikuwahi kuwaza kabisa kama kuwa kwangu pale ni faida kwa wengine......

Nilisoma chuo miaka mitatu kupitia ile biashara nilimaliza 2015 kizaazaa alipoingia huyu bwana wateja wakaanza kupungua mdogo mdogo mwishowe hakuna kabisa umeuza sana laki tena wikiendi kufika 2017 mwishoni nikafunga rasmi biashara........
Hii sio kwanza mambo magumu wateja wa kubet kwenye vikaratasi wengi wamehamia online. Haya mambo ya technology yanabadilisha mifumo mingi
 
Nikuombe kitu kimoja siku nyingine ukitaka kutusaidia ficha location yako alafu eleza wazo lako ili kulinda maslahi yako kama anavyofanya @CONTROLA, wengi tutanufaika na Mungu atakubariki
emoji120.png
emoji120.png
Hivi huyu mwamba yupo? Mungu ampe afya mpaka ajiulize
 
Back
Top Bottom