Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Kuna vijana wamejiajiri hapa mitaa ya sokoni karibu na kituo cha bajaji na bodaboda wao wanatengenza vitafunwa Waha hawa jamaa ,andazi 200,chapati 500,bagia 100,donati 300..kila muda wako busy .Acha kijana aseme hakuna mishe Ila vikazi vya kupata 20 Kwa siku vingi Sana ni vile tu
 
Mhh Muha anatengeneza bites😜..sili hata kama dawa...kazi za kuingiza 20 nyingi mnoo shida yetu tunaishi kwa kufake..na hatupend kujichosha
 
Mkuu, ushauri wangu kwako ni kuwa jitahidi uwezavyo upate biashara hata ndogo ikiweza kukupa net profit ya atleast 10k+ per day.

Ni mkondo huo ndio utakusaidia kuepukana na unemployment circle baada ya kuhitimu masomo, unless uwe na msingi wa kuanzia baada ya kuhitimu lakini bado pia utakuwa umegain experience.

Usikate tamaa, binafsi huwa nina principle yangu kuwa "Loss happens when capital/business meets poor plans". Ninacho amini me ni kuwa, biashara haifeli unafeli wewe na mipango yako. Ndio maana ulichofeli ww kuna mtu kimempa mafanikio.

Chunguza ni wapi ulikosea before, fanya maboresho kisha wekeza tena either biashara ile ile (km bado ina potentials) au buni kitu kingine, kukata tamaa ni zaidi ya kufa ukiwa unatembea.
 
Yani hapa niko nasolve hiki kitendawili,nikipata majibu tu.Mimi tajiri.
 
Sasa mkuu wewe unaleta utani na maisha watu tupo mtaani tumepigika, siunaona mtu kaanzisha uzi kama hivi! Maana yake anahitaji msaada, pia wengine wanafaidika kupitia michango ya mawazo inayotolewa,

Unaposema unabiashara ya mtaji mdogo na inakupa faida kubwa, na huisemi, mtu anaona kama unambania au kumnyanyasa kisaikolojia, unatuongezea maumivu mkuu ujue watu tumewahi kwenda kuomba kazi kwenye makampuni ya wageni tukazuiliwa kuingia ndani na wabongo wenzetu,ma secretary wanachana na kutupa barua za maombi ya kazi kwenye dustbin.

Kiufupi tunapitia mengi sana mpaka tumejawa na stress inafikia point tunajikuta tukikutana na mtu anayekunyima mchongo kama hivi unakumbuka maumivu yote uliyopitia ya kunyanyaswa na wabongo wenzetu.

Nisamehe sana mkuu niliandika kwa makosa na hasira tu zinazotokana na stress I'm sorry [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Nikuombe kitu kimoja siku nyingine ukitaka kutusaidia ficha location yako alafu eleza wazo lako ili kulinda maslahi yako kama anavyofanya CONTROLA, wengi tutanufaika na Mungu atakubariki [emoji120][emoji120]
 
Ukiachaga pombe za kienyeji unakuwaga na akili saana, mwanzoni umetoa ushuzi mtupu ila Sasa ndo umeongea Kama mwanaume.

Anyways, your apology has been accepted.

Siku nyingine nitatoa na dira na mchanganuo mzima wa mchongo then namute location. Wanaume wanaongea kiume hawatukanani na kupeana mipasho.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Naku PM mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…