Wakuu kufulia ni kubaya sana,alafu mbaya zaidi kila mmoja ana kiwango chake cha kufulia ambacho mtu mwingine anaweza kuona kawaida tu,bakhresa kufulia kwake ambako kutamtia stress sio sawa na kufulia kwangu mimi ama wewe.
Kuna wakati nilikuwa napiga pasi ndefu yani nakula jioni mpaka jioni,ugali nyanya moja na matembele ambayo nilipanda kwangu,wakati huo wife hayupo nilikuwa najibana ili nimtumie wife na mtoto.
Kwa kuwa mimi ni muislamu nilikuwa naona nisikae na njaa bure tu,one day nilirudi home sina kitu ndani niko na unga tu na nje kuna matembele tu,nikaona isiwe kesi nikachuma matembele ambayo nilikuwa na ratiba ya kuyalima ila nikasitisha kwanza,nikakaanga matembele na mafuta nikala zangu na ugali ilikuwa saa kumi jioni nimekula ugali,usiku ukapita asubuhi yake nikaamkia funga nikaja kula tena ugali na tembele usikubwa saa moja.
NIlifulia mpaka nikaenda jikoni nikatafuta matenga ya vyakula nikakuta dagaa wa siku nyingi wameshapiga vumbi jingi sana kama wameoza hivi,nikasema nyie hamjaoza dawa yenu moto,nikawa nawaunga vizuri wale dagaa hata siwaoshi maana nilihisi nikiwakosha nitapunguza nyama,nikawa nawapika siku kadhaa wamenivusha mpaka wameisha lile vumba la chini la dagaa nikaishi nalo fresh.
Siku moja nimepigika vibaya nikapanga nikakope kwenye duka fulani hivi nyanya alafu niwapige ssaundi kwamba ntapitisha hela yao baadae,lengo nikapike ugali tembele nyanya,daah nafika lile duka limefungwa daah,nikasema sio kesi nikarudi home nikapika ugali nikaenda kuchuma tembele ambalo lipo nyuma ya nyumba la kutosha alafu nikalipika hvyo hivyo na chumvi(ikanoga tu) bahati nilikuwa na mafuta nikala ilikuwa mida ya jioni kama saa 9 hivi,baada ya hapo sikutia kitu kwa siku ile.
yani unaipigia nauli mahesabu alafu unaanza kuwaza hivi nimipanda wapi mpaka wapi napata unafuu wa nauli ? Nikipata hizo plan nilikuwa naishi nazo hata ikipungua 100 inanisaidia kununua kitunguu,thamani ya pesa kwangu ilipanda sana aisee.
Kuna wakati narudi home sina shilingi naanza kusearch kwenye mabegi ya wife na vipochi vyake nakuta mia tano,buku naishi nazo yeye simuambii.
kuna wakati nakaa nakumbuka kwamba siku kadhaa nyuma niliona mia mbili chini ya uvungu wakati natafuta peni,basi naanza kuisaka naikuta naifanyia bajeti,ila kitu kilikuwa kinanipa moyo ni kwamba YATAPITA,KWANI YAMEPITA MANGAPI ?
Kuna ile unapekua kwenye makochi upate nauli huwenda watoto walichezea pesa wakatupa humo,unaangalia kwenye vungu za makochi huwenda utakuta chochote lakini wapi hukuti kitu.
Nilikuwa na kawaida ya kusahau pesa mfuko wa suruali,ila hali ambayo niliipitia nilikuwa nikipekua nguo zangu chafu nakuta zilishapekuliwa zamani na mimi mimi,so ilikuwa ni kawaida kupekua nguo moja mara tatu nikitegemea miujiza ya kwenye muvie lakini waapi.
Nilikuwa na unga wa sembe ndani ulikaa muda kama umeharibika hivi ila nikasema hapana huu unga haujaharibika na kama umeharibika basi daea yake moto maana moto huua vidudu vibaya,niliutumia vizuri ule unga mpaka ukaisha na wala sijaumwa hata nini.
Kuna siku nimekaa plan zote zimegoma moja haikai mbili haikai nikashika simu nikachagua majina yangu potential kama ma5 hivi,nikampigia kila mmoja nikamuomba alfu 5 aniazime,bahat nzuri wote walinipa so nikawa na kama 25 alfu hivi,nikasema hii 25alfu ningemuomba mtu mmoja ningekosa,so nikapata akili ga kuigawa vipande ile 25alfu alafu kila mdau wangu atacheza na buku tano anifanyie muamala,akili ilikaa saws na nikapata.
My take : ukiwa na shida IGAWANYE KWA WATU WENGI USIMTEGEMEE MTU MMOJA PEKEE.
IGawe shida yako kwenye vifungu vidogo kishs kila mtu mtawanyie kifungu chake apambane kukusaidia,usitake kutatuliea shida yako yote na mtu mmoja utakuwa dissapointed
ilifikia hatua kuna mdogo wangu kamaliza form four ndio nikawa nampiga virungu vya alfu kumi kumi kila baada ya siku kadhaa,mdogo wangu hana kazi lakini ndio nampiga virungu vya vocha mara anitumie buku 10 alikuwa akipiga deiwaka home so viakiba vyake nilikuwa nampiga virungu mimi kiroho safi alikuwa ananikopesha.
Ila nikiwa na watu kwenye pirika zangu nafurahi najifanya nimesahau shida kwamba nimefulia ila ukweli ninao moyoni peke yangu.
Nilichojifunza kwenye shida.
1.shida na kufulia kusikuondolee kutimiza majukumu ya kila siku labda majukumu hayo yategemee fedha,ila kama umefulia kama ulikuwa na ratiba ya kusoma soma,kusali sali,kutembelea wagonjwa katembelee,usizipe airtime shida zikaingilia ratiba kea sababu maisha yana ups and down nyingi sana.
2.ukifanikiwa kidogo inua watu wako wa karibu ambao huwa muna share mambo mbalimbali,ukiwainua hawa hata siku ukidondoka watatokea wachache watakushika mkono kukuinua(ila tenda wema nenda zako)lakini ukiwa na shida haikufanyi usiombe msaada wa watu ambao uliwainua.
3.umasikini unatufundisha thamani ya hata ile pesa ndogo,kuna wakati nilikuea naona alfu 20 ni pesa ya kutumia siku moja au mbili,ila nilipopigwa na ukame nikajua kwamba alfu 20 ni pesa ambayo ilikuwa inanitosha kula zaidi ya wiki kama unga na mkaa upo ndani.
4.umasikini unanifundisha kueahurumia wengine,kuna ile unapita sehemu mtu anakuomba pesa ya kula,kama umepitia msoto ukikumbuka unanza kuwaza hivi wakati napitia msoto laiti ningekuea naomba kama huyu kuna ambaye angeniamini ? JAWABU HAPANA,lakini kweli msoyo unaupitia ila ukiwa omba omba hauaminiki,so hata huyu anayekuomba kuna uwezekano mkubwa anapitia msoto ila humuamini sooo utampaa na kumsaidia.
5.Umasikini umenifundisha kwamba kula chakula sio lazima,unaweza kushindia maji siku nzima na ukaiona kesho,nilishindia maji sana japokuwa ilikuwa nikipata senti hata alfu 10 ya pamoja napaniki naona ni pesa nyingi naanza kula ovyo wakati kabla ya hapo kumiliki laki 5 kila mwezi ilikuwa kawaida,ila unapigwa umame mpaka ukiea na alfu 10 unachanganyikiwa kwa namna ilivyokuwa nyingi.
Kikubwa ni stress katika kufulia stress ni mbaya sana,stress zinaua na kudumaza akili.