Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Nimesoma hii Comment yako machozi yamenilenga[emoji26]

Iko hivi Mkuu...Kuna watu ni Daraja,Baraka katika maisha ya watu wengine....Hata wewe pia...

Hujawahi kuona unaweza kuwa kwenye changamoto fulani halafu Mungu anamleta mtu wewe mwenyewe huelewi..Then huyo mtu atakusaidia kwenye hiyo changamoto.. ukivuka hapo anaondoka na siyo mmegombana... ni ukaribu tu unapungua..Maana yake ni nini? Kazi yake ameimaliza...Anatakiwa akafanye kingine kwa wengine na wengine tena...Hawa watu wanaitwa "Destiny Helper"
Amin tena hii imewahi kunikuta nikiwa nchi za watu ni mtu maarufu hapa bongo kwenye sinema amewahi kunisaidia wakati huo hata hatujuani...!
 
Without test there is no testmony.......niliwahi kimbia na sufuria la viazi vitamu kwenye mji wa mwalimu mmoja nika survive siku mbili kwa viaz vile.......unatafuta kazi hupati na hata vitu ulivonavyo haviuziki maana ni low standard au outdated😃😅😅
 
Sitasahau nilivyoanza kukopa hela kwenye applications za mikopo nilizokuwa nazidharau nikiona matangazo yangu Facebook. Sasa picha linaanza kuna siku nataka kukopa TENI kwenye Moja ya application za MIKOPO wakaomba picha yangu ya kuscan nilikuwa bar then nakimbia toilet kupiga picha kwa Siri ghafla umeme ukakata daah ilikuwa noma sana wakuu. Chanzo Cha yote hayo ni kupitia ugumu wa kuichumi usiombe yakukute[emoji23]
Mm inani gomea kukopa hizo apps asee sijui shida nn wakat nashida na hela balaaaa
 
Nimesoma comments zoote
Kwa hakika maisha ni tough
Neno moja lisikauke kinywani ni AHSANTE MUNGU
binafsi sikuwahi kupitia maisha magumu hata kidogo
Kwetu tupo 6
Ila mshua alipambana kadri ya alivyoweza kuweka mambo level nyumbani
Leo wa tatu kati ya sisi sita tunaweza kusema tunajitegemea

Wazazi wanapambana sana sana Sanaa kujenga tabasamu kwetu
Thus mama au mzee wanapotaka chochote hua sisiti kutoa pesa
Mlijengwa kwenye msingi mzuri, wababa wengi wa Sasa hawajui mamlaka Yao na jukumu lao kwa kizazi Chao kiasi Cha kulaaniwa bila wao kujua, unakuta baba kijana kabisa hajengi msingi wa watoto wake ila na muda mwingine watoto wamekuwa kidogo na hawana msingi mzuri anashinda kuomba hela kama mtu asiye na nguvu na watu wanashangilia, ila baba wa hivyo huwa ananya'gwa mamlaka yake na Mungu na uzee wake huwa mbaya sana tena wa kuomba omba kama ombaomba, ila baba aliyesimama kwenye msingi wake huku anamkumbusha Mungu ambariki ili asimamie majukumu yake vizuri hata watoto wakiondoka wote Bado Mungu huwa anampa watu wa kumuhudumia nyakati za uzee.
 
Without test there is no testmony.......niliwahi kimbia na sufuria la viazi vitamu kwenye mji wa mwalimu mmoja nika survive siku mbili kwa viaz vile.......unatafuta kazi hupati na hata vitu ulivonavyo haviuziki maana ni low standard au outdated😃😅😅
Ungeitiwa mwizi bruh 😄
 
Ili kuimarika kuna mapitio mengine ni muhimu kuyapitia ili yawe ukumbusho wa kukosa pale ukipata.

Ila kiukweli kabisa hakuna faraja kwenye ufukara.

Nakumbuka kuna kipindi nilipigika ikawa natembelea washkaji mida ya misosi kiasi cha kujua ratiba ya mlo wa masela wote.

Kuna msela wangu (Mungu amlaze mahala pema) ilikuwa ikifika jioni ananipigia simu kuniita tukapige story, kumbe alishajua hali yangu na ule wito ulikuwa ni msaada indirectly maana alihakikisha nakula ndio naondoka.

Na kila nikiondoka mkewe ananipa kikontena cha msosi ananiambia shem naona chakula cha leo umekipenda beba na hiki utakula baadae.

Hawakujua jinsi gani walikuwa wakinisevu.
Jamani,usiwasahau watoto wa huyo jombaa km bado mna uhusiano na baada ya jamaa kufa
 
Wakuu kufulia ni kubaya sana,alafu mbaya zaidi kila mmoja ana kiwango chake cha kufulia ambacho mtu mwingine anaweza kuona kawaida tu,bakhresa kufulia kwake ambako kutamtia stress sio sawa na kufulia kwangu mimi ama wewe.

Kuna wakati nilikuwa napiga pasi ndefu yani nakula jioni mpaka jioni,ugali nyanya moja na matembele ambayo nilipanda kwangu,wakati huo wife hayupo nilikuwa najibana ili nimtumie wife na mtoto.

Kwa kuwa mimi ni muislamu nilikuwa naona nisikae na njaa bure tu,one day nilirudi home sina kitu ndani niko na unga tu na nje kuna matembele tu,nikaona isiwe kesi nikachuma matembele ambayo nilikuwa na ratiba ya kuyalima ila nikasitisha kwanza,nikakaanga matembele na mafuta nikala zangu na ugali ilikuwa saa kumi jioni nimekula ugali,usiku ukapita asubuhi yake nikaamkia funga nikaja kula tena ugali na tembele usikubwa saa moja.

NIlifulia mpaka nikaenda jikoni nikatafuta matenga ya vyakula nikakuta dagaa wa siku nyingi wameshapiga vumbi jingi sana kama wameoza hivi,nikasema nyie hamjaoza dawa yenu moto,nikawa nawaunga vizuri wale dagaa hata siwaoshi maana nilihisi nikiwakosha nitapunguza nyama,nikawa nawapika siku kadhaa wamenivusha mpaka wameisha lile vumba la chini la dagaa nikaishi nalo fresh.

Siku moja nimepigika vibaya nikapanga nikakope kwenye duka fulani hivi nyanya alafu niwapige ssaundi kwamba ntapitisha hela yao baadae,lengo nikapike ugali tembele nyanya,daah nafika lile duka limefungwa daah,nikasema sio kesi nikarudi home nikapika ugali nikaenda kuchuma tembele ambalo lipo nyuma ya nyumba la kutosha alafu nikalipika hvyo hivyo na chumvi(ikanoga tu) bahati nilikuwa na mafuta nikala ilikuwa mida ya jioni kama saa 9 hivi,baada ya hapo sikutia kitu kwa siku ile.

yani unaipigia nauli mahesabu alafu unaanza kuwaza hivi nimipanda wapi mpaka wapi napata unafuu wa nauli ? Nikipata hizo plan nilikuwa naishi nazo hata ikipungua 100 inanisaidia kununua kitunguu,thamani ya pesa kwangu ilipanda sana aisee.

Kuna wakati narudi home sina shilingi naanza kusearch kwenye mabegi ya wife na vipochi vyake nakuta mia tano,buku naishi nazo yeye simuambii.

kuna wakati nakaa nakumbuka kwamba siku kadhaa nyuma niliona mia mbili chini ya uvungu wakati natafuta peni,basi naanza kuisaka naikuta naifanyia bajeti,ila kitu kilikuwa kinanipa moyo ni kwamba YATAPITA,KWANI YAMEPITA MANGAPI ?

Kuna ile unapekua kwenye makochi upate nauli huwenda watoto walichezea pesa wakatupa humo,unaangalia kwenye vungu za makochi huwenda utakuta chochote lakini wapi hukuti kitu.

Nilikuwa na kawaida ya kusahau pesa mfuko wa suruali,ila hali ambayo niliipitia nilikuwa nikipekua nguo zangu chafu nakuta zilishapekuliwa zamani na mimi mimi,so ilikuwa ni kawaida kupekua nguo moja mara tatu nikitegemea miujiza ya kwenye muvie lakini waapi.

Nilikuwa na unga wa sembe ndani ulikaa muda kama umeharibika hivi ila nikasema hapana huu unga haujaharibika na kama umeharibika basi daea yake moto maana moto huua vidudu vibaya,niliutumia vizuri ule unga mpaka ukaisha na wala sijaumwa hata nini.

Kuna siku nimekaa plan zote zimegoma moja haikai mbili haikai nikashika simu nikachagua majina yangu potential kama ma5 hivi,nikampigia kila mmoja nikamuomba alfu 5 aniazime,bahat nzuri wote walinipa so nikawa na kama 25 alfu hivi,nikasema hii 25alfu ningemuomba mtu mmoja ningekosa,so nikapata akili ga kuigawa vipande ile 25alfu alafu kila mdau wangu atacheza na buku tano anifanyie muamala,akili ilikaa saws na nikapata.

My take : ukiwa na shida IGAWANYE KWA WATU WENGI USIMTEGEMEE MTU MMOJA PEKEE.
IGawe shida yako kwenye vifungu vidogo kishs kila mtu mtawanyie kifungu chake apambane kukusaidia,usitake kutatuliea shida yako yote na mtu mmoja utakuwa dissapointed

ilifikia hatua kuna mdogo wangu kamaliza form four ndio nikawa nampiga virungu vya alfu kumi kumi kila baada ya siku kadhaa,mdogo wangu hana kazi lakini ndio nampiga virungu vya vocha mara anitumie buku 10 alikuwa akipiga deiwaka home so viakiba vyake nilikuwa nampiga virungu mimi kiroho safi alikuwa ananikopesha.

Ila nikiwa na watu kwenye pirika zangu nafurahi najifanya nimesahau shida kwamba nimefulia ila ukweli ninao moyoni peke yangu.

Nilichojifunza kwenye shida.

1.shida na kufulia kusikuondolee kutimiza majukumu ya kila siku labda majukumu hayo yategemee fedha,ila kama umefulia kama ulikuwa na ratiba ya kusoma soma,kusali sali,kutembelea wagonjwa katembelee,usizipe airtime shida zikaingilia ratiba kea sababu maisha yana ups and down nyingi sana.

2.ukifanikiwa kidogo inua watu wako wa karibu ambao huwa muna share mambo mbalimbali,ukiwainua hawa hata siku ukidondoka watatokea wachache watakushika mkono kukuinua(ila tenda wema nenda zako)lakini ukiwa na shida haikufanyi usiombe msaada wa watu ambao uliwainua.

3.umasikini unatufundisha thamani ya hata ile pesa ndogo,kuna wakati nilikuea naona alfu 20 ni pesa ya kutumia siku moja au mbili,ila nilipopigwa na ukame nikajua kwamba alfu 20 ni pesa ambayo ilikuwa inanitosha kula zaidi ya wiki kama unga na mkaa upo ndani.

4.umasikini unanifundisha kueahurumia wengine,kuna ile unapita sehemu mtu anakuomba pesa ya kula,kama umepitia msoto ukikumbuka unanza kuwaza hivi wakati napitia msoto laiti ningekuea naomba kama huyu kuna ambaye angeniamini ? JAWABU HAPANA,lakini kweli msoyo unaupitia ila ukiwa omba omba hauaminiki,so hata huyu anayekuomba kuna uwezekano mkubwa anapitia msoto ila humuamini sooo utampaa na kumsaidia.

5.Umasikini umenifundisha kwamba kula chakula sio lazima,unaweza kushindia maji siku nzima na ukaiona kesho,nilishindia maji sana japokuwa ilikuwa nikipata senti hata alfu 10 ya pamoja napaniki naona ni pesa nyingi naanza kula ovyo wakati kabla ya hapo kumiliki laki 5 kila mwezi ilikuwa kawaida,ila unapigwa umame mpaka ukiea na alfu 10 unachanganyikiwa kwa namna ilivyokuwa nyingi.

Kikubwa ni stress katika kufulia stress ni mbaya sana,stress zinaua na kudumaza akili.
 
Hatimae nimemaliza comments.

Nyie haya maisha kuna watu wanapitia mambo magumu acha kabisa. Nakumbuka kuna rafiki yangu tulisoma wote chuo, angalau mie nilipata kaajira ila yeye akawa anajishughulisha tu na vibiashara na kwao life gumu.

Kuna kipindi aliomba nimkopeshe kiasi fulani cha pesa aboost kwenye biashara zake na akawa amechelewa kurejesha kwa wakati tuliokuwa tumekubaliana na mimi nina shida nayo. Alinipiga kalenda weee mwisho akaamua akawa hapokei simu. Nikawa nina hasira nae kumbe bwana biashara zilimuendea vibaya akapigika balaa.

Ikawa hata kula yake taabu na anaogopa kurudi nyumbani kuongeza mzigo. Nilivyojua nilijisikia hatia balaa, huruma iliniingia ikabidi nimkopee tu pesa mahali aanze upya. Bahati nzuri angalau sasa akapambana mambo yakawa nafuu na baadae Mungu akamsaidia akapata kazi nzuri tu na alinilipa pesa zote na cha juu.

Ama kweli hatuna budi kumshukuru Mungu hata kwa kidogo alichotujaalia.
 
Mlijengwa kwenye msingi mzuri, wababa wengi wa Sasa hawajui mamlaka Yao na jukumu lao kwa kizazi Chao kiasi Cha kulaaniwa bila wao kujua, unakuta baba kijana kabisa hajengi msingi wa watoto wake ila na muda mwingine watoto wamekuwa kidogo na hawana msingi mzuri anashinda kuomba hela kama mtu asiye na nguvu na watu wanashangilia, ila baba wa hivyo huwa ananya'gwa mamlaka yake na Mungu na uzee wake huwa mbaya sana tena wa kuomba omba kama ombaomba, ila baba aliyesimama kwenye msingi wake huku anamkumbusha Mungu ambariki ili asimamie majukumu yake vizuri hata watoto wakiondoka wote Bado Mungu huwa anampa watu wa kumuhudumia nyakati za uzee.
Ahsante mkuu kwa neno Zuri

Hakika mzee wangu amepambana
Kuna mambo mengi sana yamenikaa vyema
Kwa hakika anastahili heshima kuu
 
Siku ukipata pesa kidogo sio lazima ziwe nyingi, unaweza ukawa hata na buku mbili ukaichenji mia mbili mbili then ukiona madogo sehemu hasa watoto unawapa..au ukanunua hata mfuko wa pipi unawapa..trust me inafungua sana mambo!
Ni jambo jema lkn angalia isije ikakucost siku moja,endapo ikija kutokea mtoto yoyote akapata shida suspect wa kwanza unaweza kuwa ni wewe, unaweza ukawa unafanya kwa nia njema lkn yakija kutokea ya kutokea wazazi wanaweza wasikuelewe,ni heri kutoa kwa kutumia njia salama kama kwenye vituo vya vya malezi vya watoto, misikitini au makanisani,hayo ni maoni yangu tu lkn.
 
Nikawa na familia kazi ikaota mabawa nkawa nashnda ndan mpka akil ikawa kama imefika mwsho wa kuwaza mahitaj ya nyumban yakawa n ngum kuyatiza hata sukar ya uji wa watoto asubuh ikawa ngum kupatika ges ikaisha ndio ikawa mwsho wa kutumia ges n mwendo wa kuni uko nyuma ya nyumba.. Mungu s zumarid kuna jiran akahama alikua amepanda mihogo mahind mboga za majan kibao na nyumba iko kwwnye fence akankabdh funguo il madalali wakileta watu niwe nawafungulia yale mahind na mihogo mboga za majan ndio zlnpa ahuen muda mrefu sana asubh naamka na mfuko wangu naenda navunja mahind kama 8 naleta wanachemsha tunakula tunavuka mchana n ugali mboga za majani dah kwel hakuna kukata tamaa Apo nlmwona Mungu kwenye maisha halis mana hata dukan tulkua tumefkia hali ya kutokukopesheka hata kiberit ilfka kpnd dada wa kaz anawasaidia had mawazo ndan ya nyumba mana akil zmefika mwsho dada wa watu akaomba aende kwao il kupunguza bajet aliomba nauli tu mana hali aliiona toka tuko sawa mpaka kuanguka kiuchumi.. umaskin unaumiza sana na unadhalilisha sana hata msiba wa ukoo wanaweza waskwambie ukaja kuskia tu flan ashazikwa tuliona tuskusumbue baba kumbe wameona huna impact hata wakikutaarfu
 
mimi ntachangia kidogo hapa japo sijasota kivile ila nami nilipitia kikaongoni kidogo ila sababu kubwa ilikuwa ni mzee wangu ila nilimuonyesha jambo ambalo alikuwa haliamini ya mimi kama mimi kusimama pekee yangu bila KUZITEGEMEA FEDHA ZAKE WALA MARAFIKI ZAKE WENYE PESA mzee wangu ni don kimtindo na ana kampani ya watu wazito ila tatizo lake kubwa huwa anachotoka au sema kwa watoto wake kiwe sheria tena na UTEKELEZAJI juu ila siku nilivyomwambia NO hakuamini nakuanzia hapo akanidump mazima nikaondoka home mimi na kibegi changu tu mungu ndo anajua walikuwa nisaidia watu ambao sikudhania kabisa kabisa nikajivuta mdogo mdogo hadi nikawa na familia na kazi yangu safii tu ila huo msoto mungu ndo anajua ila sasa ananiheshimu balaa na wala sijawahi mwambie maisha yangu baada ya kuondoka nilifanya nini na nilienda wapi miaka saba tupo mji mmoja ila hatuonani ? hii niseme tu ukweli ilipunguza mapenzi kwa baba kwa kiasi kikubwa japo si mchukii ila huwa namuona kama mshakaji tu uzuri anajiweza huwa hanisumbui.
 
Back
Top Bottom