Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kamwe do not entertain kumwaga chakula ndani kwako, hakikisha chakula kinapikwa cha kutosha watu kushiba vizuri lakini kisiwe kinamwagwa. Kosa/dhambi kubwa sana hii kumwagamwaga vyakula.
nilishagombana na wife kwa sababu hiyo mwisho nikaamua kufuga bata kuku na sungura ili mabaki wale wanyama sio kumwaga jalalani
 
Ugumu wa Maisha ndo ulionijenga na kusimama hapa Leo hii kama Mimi.
Niliwahi kumuona Mama yangu Mzazi mchana kweupe akiwa anatengeneza samaki huku akitoa machozi mateso na manyanyaso ya Mzee wangu baada ya kuoa mke wa pili .

Tuliteseka sana , Ndugu? Ndugu kitu gani wanafiki wakubwa wachawi kwanza wafie mbali
Iliniuma sana mpk Leo Huwa nakumbka na kujisikia vibaya hata kunifanya kuwa jasiri na hata mbabe sana....

Mpaka nilipo maliza Chuo kikuu niliondoka home miaka zaidi ya 5 ....
Sikua Tyr kurudi nyumbani bila kitu mkononi ....
Maisha ni magumu Sana, ila Mungu wetu ni Mwema sana.
 
kuna kipindi nishawahi zurura sana maduka ya dawa kuomba kazi toka Kimara mwisho hadi kariakoo nikarudi tena kuanzia Magomeni nikazunguka hadi Morroco ni kuacha namba wakati huo sina chochote ghetoo natafuna mchele tu maana nilikua naogopa hata kupika utaisha gesi hamna, kodi inaelekea kuisha mzee kashaninawa (we si ushamaliza chuo jitegemee) Dady's voice nilikaa siku hadi tatu sili hadi Mungu alipofanya njia
 
Samahani Ndugu yangu... Nimepiga screanshot
Comment yako hii Kwa matumizi yangu binafsi hapo baadae.
 
Kyai kya rangi
 
Hao ndio Wana wakukufaa mpaka kifo.
 
….wakati mgumu upo kwa kila mtu na wakati mwepesi upo kwa kila mtu…..hv ni vipindi ambavyo kila mtu atapitia kwa wakati tofauti kikubwa imani…

Kamwe usipoteze imani iliyojaa matumaini…

Mungu yupo…pambana,hakuna kinachotokea bila ya sababu weka uthubutu kwenye kila hitajio lako

Asantee….
 
Leo umekuwa Mlabata. Ila aisee umaskini ni kitu kibaya kuliko vyote, usione watu wanauza bandari ukadhani wanapenda, ni kwasababu wanaujua umaskini vilivyo. Tuache tu maisha haya aliyeyapanga anajua kwanini.
 
Pole sana mkuu,kila nikitaka kuandika yangu nakutana na yale konki mpaka nimeona wacha tu nisimkufuru Mungu,muhimu ni kumshukuru yeye kwa kile kidogo unachokipata,maana kuna watu wanapitia maisha magumu sana hapa duniani hivyo si vibaya unapopata ziada kujitahidi hata kusaidia na wengine ambao hali zao ni mbaya...
 
Katika vitu ambavyo naweza ua mtu, ni kuchezea chakula. Huwa sikubali familia ichezee chakula. Haya maisha ni chakula hakuna kingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…