Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kamwe do not entertain kumwaga chakula ndani kwako, hakikisha chakula kinapikwa cha kutosha watu kushiba vizuri lakini kisiwe kinamwagwa. Kosa/dhambi kubwa sana hii kumwagamwaga vyakula.
nilishagombana na wife kwa sababu hiyo mwisho nikaamua kufuga bata kuku na sungura ili mabaki wale wanyama sio kumwaga jalalani
 
Ugumu wa Maisha ndo ulionijenga na kusimama hapa Leo hii kama Mimi.
Niliwahi kumuona Mama yangu Mzazi mchana kweupe akiwa anatengeneza samaki huku akitoa machozi mateso na manyanyaso ya Mzee wangu baada ya kuoa mke wa pili .

Tuliteseka sana , Ndugu? Ndugu kitu gani wanafiki wakubwa wachawi kwanza wafie mbali
Iliniuma sana mpk Leo Huwa nakumbka na kujisikia vibaya hata kunifanya kuwa jasiri na hata mbabe sana....

Mpaka nilipo maliza Chuo kikuu niliondoka home miaka zaidi ya 5 ....
Sikua Tyr kurudi nyumbani bila kitu mkononi ....
Maisha ni magumu Sana, ila Mungu wetu ni Mwema sana.
 
kuna kipindi nishawahi zurura sana maduka ya dawa kuomba kazi toka Kimara mwisho hadi kariakoo nikarudi tena kuanzia Magomeni nikazunguka hadi Morroco ni kuacha namba wakati huo sina chochote ghetoo natafuna mchele tu maana nilikua naogopa hata kupika utaisha gesi hamna, kodi inaelekea kuisha mzee kashaninawa (we si ushamaliza chuo jitegemee) Dady's voice nilikaa siku hadi tatu sili hadi Mungu alipofanya njia
 
matatizo ndo hufanya akili zetu kuwa aggressive kwenye kutafuta fursa.

siku zote mwanaume usikubali kuwa na maamuzi yatakayoplekea familia yako ilazimike kwenda kulia kwa familia ingine ili ipate chakula, nguo ama malazi. (allocate your income wisely)
Vingine vya magari hivyo na mijengo sita sita ni majaaliwa.
Samahani Ndugu yangu... Nimepiga screanshot
Comment yako hii Kwa matumizi yangu binafsi hapo baadae.
 
Kipindi Nikiwa na miaka 16, niliwahi kutoroka mateso ya mama mkubwa na kutembea kuanzia Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Hadi Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, umbali wa kilometa zaidi ya 400 kwa muda wa siku 19 kukatisha kipande cha mbuga ya Tarangire. Kulikuwa na wanyama wengi isipokuwa simba, tembo na chui. Nilikutana na kundi kubwa la mbwa mwitu lakini Kama siku yako haijafika, haijafika tu.
Kyai kya rangi
 
Ili kuimarika kuna mapitio mengine ni muhimu kuyapitia ili yawe ukumbusho wa kukosa pale ukipata.

Ila kiukweli kabisa hakuna faraja kwenye ufukara.

Nakumbuka kuna kipindi nilipigika ikawa natembelea washkaji mida ya misosi kiasi cha kujua ratiba ya mlo wa masela wote.

Kuna msela wangu (Mungu amlaze mahala pema) ilikuwa ikifika jioni ananipigia simu kuniita tukapige story, kumbe alishajua hali yangu na ule wito ulikuwa ni msaada indirectly maana alihakikisha nakula ndio naondoka.

Na kila nikiondoka mkewe ananipa kikontena cha msosi ananiambia shem naona chakula cha leo umekipenda beba na hiki utakula baadae.

Hawakujua jinsi gani walikuwa wakinisevu.
Hao ndio Wana wakukufaa mpaka kifo.
 
….wakati mgumu upo kwa kila mtu na wakati mwepesi upo kwa kila mtu…..hv ni vipindi ambavyo kila mtu atapitia kwa wakati tofauti kikubwa imani…

Kamwe usipoteze imani iliyojaa matumaini…

Mungu yupo…pambana,hakuna kinachotokea bila ya sababu weka uthubutu kwenye kila hitajio lako

Asantee….
 
Ila umaskini ukiongeza madeni balaa tupu[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
20230620_164522.jpg
 
Nimeandika, nikafuta, nimeandika tena nikafuta…..aisee nikianza kueleza vile umasikini umenifanya server za JF zitajaa leo [emoji28], ila umasikini usikie kwa watu tu nyie [emoji23][emoji23].

Cvez Jobless mwenzangu una lolote la kuchangia hapa? [emoji23][emoji23][emoji23]

Acha tuendelee kula bata tu.
Leo umekuwa Mlabata. Ila aisee umaskini ni kitu kibaya kuliko vyote, usione watu wanauza bandari ukadhani wanapenda, ni kwasababu wanaujua umaskini vilivyo. Tuache tu maisha haya aliyeyapanga anajua kwanini.
 
Nilikuwa naishi na bibi yangu, kwakuwa hatukuwa na chakula ndani ikabidi aniache pekeyangu aende kwa baba zangu wadogo kuomba pesa ya matumizi.

Safari yake ilikuwa ya siku mbili kama sijakosea. Aisee nilishikwa na njaa nikachemsha yale mamchicha mekundu nikala baadae nikaenda kwa jirani nikakuta wanatoa vichwa kwenye samaki wadogo kanda ya ziwa tunawaita Furu.

Ikabidi niwaombe vile vichwa, nakumbuka nilidanganya naenda kumpa bata wangu. Nilichemsha vile vichwa nikala nikanywa na supu angalau nikawa vizuri.
Pole sana mkuu,kila nikitaka kuandika yangu nakutana na yale konki mpaka nimeona wacha tu nisimkufuru Mungu,muhimu ni kumshukuru yeye kwa kile kidogo unachokipata,maana kuna watu wanapitia maisha magumu sana hapa duniani hivyo si vibaya unapopata ziada kujitahidi hata kusaidia na wengine ambao hali zao ni mbaya...
 
Unaweza ukadhani ni masihara ila hivi vitu vipo mkuu, kuna muda nilikuwa naona kabisa vidonda vya tumbo vinanyimelea, ile njaa ya kukosa kula siku nzima unaona kabisa tumbo linawaka moto kama limemwagiwa tindi kali.

Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
Katika vitu ambavyo naweza ua mtu, ni kuchezea chakula. Huwa sikubali familia ichezee chakula. Haya maisha ni chakula hakuna kingine.
 
Back
Top Bottom