Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Hii inaweza kuwasaidia

Kwa hustler yeyote ukiingia kwenye mji au nchi yoyote ambao ww ni mgeni huna pa kufikia wala hujui utapata wapi kibarua, cha kufanya uliza mwenyeji yeyote akuelekeze mahali Soko kubwa la mji lilipo.

Amini nakwambia hutolala njaa pindi ukifika sokoni na hutakosa kazi ya kufanya hata kubeba mzigo utabeba na pesa utapata.

Why Sokoni na si mahala pengine? Sokoni ndio sehemu ambapo kuna mzunguko mkubwa wa pesa katika mji au kitongoji husika. Baada ya hapo sasa utaweza kuangalia ufanyaje ili utoke kimaisha.

Sehemu nyingine ambayo inaweza kukuokoa ni Migahawani au Hotelini. Hii sehemu inaweza kukuokoa usilale na njaa na pia unaweza kupata ujira mdogo. Ukifika maeneo hayo omba kazi ya kufanya usafi na hata kuosha vyombo. Hii itakusaidia sana kupata ujira mdogo na chakula pia.

Mwisho kabisa ni nyumba za ibada iwe msikitini au kanisani. Huku kunaweza kukupa fursa ya kukutana na watu wenye hofu na kumjua Mungu hivyo ni mara chache sana kwa wewe mgeni kukosa hifadhi au chakula, na ukiwa nao vizuri unaweza ukapatiwa connection ya kazi.

Kikubwa ukifika sehemu yoyote jiepushe sana kuomba Fedha bali omba kibarua /kazi ,hii itakuwezesha upate pesa ya kujikimu na vilevile kukuepusha dhidi ya fedheha na udhalili wa kuombaomba. Kumbuka mwanadamu hapendi kuombwa pesa.

Katika kutafuta pesa epuka kitu kinachoitwa kuona aibu, watu watakuchukuliaje nk. Mwanaume hachagui kazi as long as kazi hiyo ni ya halali na haimuondolei utu wake
 
Umasikini acheni nyie wazee unauma sana ,nikifikiria enzi nasoma form two mama kapanga chumba kimoja nakaka tumerudi likizo tunalala na mama yetu mzazi humohumo,nabibi humohumo namdogo wetu humohumo...achane nyie wazeee...vijana wakiume kulala chumba kimoja namzazi wakike kisa kukosa getho sio poa akili itakukaa sawa tu nalazima kama unajitambua ukakaze msuli ,nikupitia hali hyo iliyotufanya sote )mm nakaka kujituma kwakiwango cha rami hadi sasa tu namiliki nyumba ya vyumba kumi,nahata hatuishi hapo nyumbani tunajitegema kila mmoja.ufukara unakufnaya akili ikae sawa.
 
Touching story,
MUNGU amekua mwema sana kwako stay blessed 🙏❤️
 
Nyumba za ibada unaweza ukafia humo labda msikitini ila hizi mbwa nyingine zimejiandaa kupokea tu wala sio kutoa
 
Kuna kipindi nilipitia SONONA kuu katika maisha YANGU........

In that situation nilipoteza Kila kitu muhimu nilicho kipambania katika maisha yangu...............

Nili lose appetite kwenye Kila kitu kiasi Cha kukaa siku tatu bila kula chochote na huisi NJAA.............

Siku ya nne jion nikasema Nile japo kidogo maana nili Anza hisi NJAA nyumbani issues za misosi haikuwa shida....

Nikapakua sahani kubwa wali sato na mboga mboga na mchuzi wa kutosha lile tonge la kwanza lilitosha kunichana chana kama wembe kuanzia mdomoni, kwenye koo mpka kwenye utumbo......

Nilishindwa kukila kile chakula zaidi ya kukitazama na kutamani lakini nilikua nimechanika vibaya.....

Kwa muda wa siku tatu zingine nili ishi Kwa juice,uji na mtori tena ulipita Kwa maumivu mengi baada ya kipona madonda ya mdomoni kwenye koo mpka kwenye utumbo nikawa very strong linapo kuja swala la uvumilivu wa NJAA
 
Nilichojifunza ukiwa na hela njaa ikija inakupiga chabo inaamsha zake inaona kabisa jamaa hatishiki, yaan unaweza shinda siku nzima bila kula na njaa huhisi.

Kivumbi miaka hiyo unaamka hujui utakula nini, inafika jion unamtembelea msela geto angalau upige story uambulie nae haweki msosi mezani, unaamua kuangalia movie moaka unasinzia msela anaamka anakula akizan uko fofofo unajikaza ale amalize bila kuamka ili usimkate stimu, akimaliza kula unaamka unasepa, unafika geto unakunywa maji unalala, usingizi hauji. Panakucha unaamua ukapambane kitaa unaambulia patupu. Kila dili ikija inakurika aisee unaona hapa hapanifai.
Unajitafuta unajipata wale wale wanaanza kutangaza unaringa, unajivuna sana, jamani mbona wakati wa msoto hamkusema nateseka nasota sana.
Ni bora ninunue sigara japo sivuti nizituoe lakini kuna watu siwezi kuwasaidia hata wapigane na nyoka ntakaa upande wa nyoka.
 
Akikujibu niambie.

Huyo mke ninaye mpka leo.
I love her and she loves me.

Na sasa nimemfungulia shule ya wanafunzi wa awali ana wanafunzi zaidi ya 200 sasa. kila mwanafunzi analipa ada 480,000 kwa mwaka.
na mimi nina kazi nzuri tu Mgodini hapa Kahama

Uvumilivu wake ndo umeleta matunda mpka leo kwa kunitia nguvu na kujiona kuwa its possible

“As long as your breathing, Never give up”

Fight to the last drop of blood in your veins!!!!
 
Huu Uzi utachukua nyota 5 thanks mkuu Tupo hapa kujifunza......
 

Sure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…