BUMIJA
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 5,950
- 11,295
Sio wote wenye magari[emoji23] Hata JF inawashangaa,Wamesahau kuwa wana JF wote tunasukuma ndinga kali na life fulani hivi la ki sure.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio wote wenye magari[emoji23] Hata JF inawashangaa,Wamesahau kuwa wana JF wote tunasukuma ndinga kali na life fulani hivi la ki sure.
Ipo nje ya mji kidogo, vianziHii iko maeneo gani kiongozi?
Unajua japo shuhuda ninzito ila kushindia miwa nibalaa,tupu,nimecheka sio kwa ubaya mzee.Unapata wapi nguvu za kucheka?? Duh
Touching story,Mama yangu alikuwa mpika na muuza gongo kule Gongo la mboto mapolisi waliweka informer kila tukiwa tunaenda kupiga gongo wanakuja wanamkamata mama analia tukiwa mapolini kule kinyerezi(enzi hizo kinyerezi kulikuwa pori la kukamata hadi sungura na digi digi kabisa) sasa mama alikamatwa mfuluzo mbaya zaidi wakati mahita anatawazwa kuwa IGP si akapitisha opereshen maalum ambayo mama akabebwa na ma pipa na mtambo wa gongo mpaka kituoni akatuacha mimi na wadogo zangu watatu.Mimi niliachwa kwa sababu ni mdogo ikabidi mimi nikabidhiwe jezi na mchezo sijauelewa hivyo nikajikuta nina majukumu ya kulisha wadogo zangu na kumtafutia mama chakula ili ale kule lock up kwa sababu ndugu tulikuwa nao wachache pale Dar ambao kama vile walitutenga kwa sababu ya umasikini.Dingi ameshasepaga muda kakimbia familia sababu ni hiyo hiyo umasikini.
Ikanibidi niwe naenda matembezini na kiroba kwapani huko kutafuta mashamba ya watu mfano wa mashamba nilikuwa nayaonea ni ya miogo na viazi na minazi na mapera kule ulongoni enzi hizo hata TANESCO hawajaweka umeme hata nyumba moja.
Huwezi amini nilijua hadi kupandia minazi ili niibe madafu usiku anyway tu cut the story nilikuwa naondoka na kiroba kitupu nawaacha madogolas wamejikunyata nikirudi wanabidi wapokeee chochote ntachokuja nacho kwenye kiroba kuna siku nilikimbizwa na mwenye shamba ambae lilikuwa na miogo mitamu kumbe aliweka lindo baada ya kuona katikati ya shamba lake nimelaza mashina yote aisee.
KUMBE kitendo cha kuwa namletea miogo kila siku maza mapolisi wakawa wananichora na kunidiscuss siku moja nilikosa miogo nikapeleka madafu mawili mama aliachiwa tuongee nae nje ya kituo si akaanza kulia na kuniambukiza kilio na mimi kumbe ile ilikuwa pona yake si mkuu wa kituo akazipata zile habari maana kumbe watu wanapewa dhamana mimi sijui taratibu wakaniuliza eti kesho nije na mkubwa tumdhamini kwa vile ndugu walishatutenga ikabidi nikamchukue MAMA SALAWALA(sijui yupo wapi) ambae huwa tunamuuziaga gongo anaishi mzambarauni Gongo la mboto.
Mama akatoka mtaji ukawa umefilisiwa maana walibeba mtambo wa gongo na mapipa yote ikabidi mama awe raia mwema akaanza kuazima shamba tukawa tunalima huku tunashindia maembe
Anyway njaa ni noma inakosesha hadi ladha ya maisha
Sitaki kueleza mengi at the end nikafaulu mtaa mzima kwenda shule ya AZABOY nikaona shida zinazidi nyumbani hata nauli nikakosa ikabidi niende kujipendekeza kwa madogo wa dogo dogo center Mabibo karibia na shule ya loyola walipangishiwa nyumba na wadhamini wao wazungu.
Story ni ndefu ila acheni nijiite Billie humu JF kwa sababu hata mama yangu kwa sasa nimuanzishia biashara anaishi kwenye nyumba nzuri na kuna flame za kupangisha 8 na ana nyumba za wapangaji 5.
Upande wa mimi now nilivyo sitaki kusema ila nipo na familia ambayo watoto kula mpaka uwashikie fimbo au uwawekee katuni na almost kila kitu ndani hadi vyakula vinaharibika.SIJITAPI NAONGEA UKWELI TUPU NIMEJIFUNZA SHIDA NI ELIMU NZURI SANA KAMA UKIWEZA KUZITOROKA.
Nyumba za ibada unaweza ukafia humo labda msikitini ila hizi mbwa nyingine zimejiandaa kupokea tu wala sio kutoaHii inaweza kuwasaidia
Kwa hustler yeyote ukiingia kwenye mji au nchi yoyote ambao ww ni mgeni huna pa kufikia wala hujui utapata wapi kibarua, cha kufanya uliza mwenyeji yeyote akuelekeze mahali Soko kubwa la mji lilipo.
Amini nakwambia hutolala njaa pindi ukifika sokoni na hutakosa kazi ya kufanya hata kubeba mzigo utabeba na pesa utapata.
Why Sokoni na si mahala pengine? Sokoni ndio sehemu ambapo kuna mzunguko mkubwa wa pesa katika mji au kitongoji husika. Baada ya hapo sasa utaweza kuangalia ufanyaje ili utoke kimaisha.
Sehemu nyingine ambayo inaweza kukuokoa ni Migahawani au Hotelini. Hii sehemu inaweza kukuokoa usilale na njaa na pia unaweza kupata ujira mdogo. Ukifika maeneo hayo omba kazi ya kufanya usafi na hata kuosha vyombo. Hii itakusaidia sana kupata ujira mdogo na chakula pia.
Mwisho kabisa ni nyumba za ibada iwe msikitini au kanisani. Huku kunaweza kukupa fursa ya kukutana na watu wenye hofu na kumjua Mungu hivyo ni mara chache sana kwa wewe mgeni kukosa hifadhi au chakula, na ukiwa nao vizuri unaweza ukapatiwa connection ya kazi.
Kikubwa ukifika sehemu yoyote jiepushe sana kuomba Fedha bali omba kibarua /kazi ,hii itakuwezesha upate pesa ya kujikimu na vilevile kukuepusha dhidi ya fedheha na udhalili wa kuombaomba. Kumbuka mwanadamu hapendi kuombwa pesa.
Katika kutafuta pesa epuka kitu kinachoitwa kuona aibu, watu watakuchukuliaje nk. Mwanaume hachagui kazi as long as kazi hiyo ni ya halali na haimuondolei utu wake.
Kuna kipindi nilipitia SONONA kuu katika maisha YANGU........Daaaah acheni mikasa ni mingi lakn nakumbuka tu wakat nimeenda kuripoti chuo,,hela ya kuungaunga ile usajili ikakataa sikua hata mia,,,nilikaa siku mbili bila kula hadi vidonda vilitoka kooni aiseeee haya maisha. Lkn hali ile ilinitia uchungi nilijiapiza Mungu akiendelea kunijaalia uhai iwe mvua iwe jua kamwe wanangu wasije kupitia yale maisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mke unaye mpaka leo?!
Amina bro mimi nauogopa umasikini kuliko jini aiseeTouching story,
MUNGU amekua mwema sana kwako stay blessed [emoji120][emoji3590]
Akikujibu niambie.
Yale mabango ya seminar ,life after campus 😀😀nilikuwa nayachukulia poa,ila nyuma yake ni😀😀Naomba nijue maana ya kutembelea chaki.
Nitakuja na kisa changu cha maisha baada ya kumaliza chuo ila ngoja kwanza nisome comments za waungwana.
Mm naogopa sana umaskini na siku zote za uhai wangu NAMWOMBA mwenyez MUNGU aniepushe nao...............Amina bro mimi nauogopa umasikini kuliko jini aisee
Huu Uzi utachukua nyota 5 thanks mkuu Tupo hapa kujifunza......Nilichojifunza ukiwa na hela njaa ikija inakupiga chabo inaamsha zake inaona kabisa jamaa hatishiki, yaan unaweza shinda siku nzima bila kula na njaa huhisi.
Kivumbi miaka hiyo unaamka hujui utakula nini, inafika jion unamtembelea msela geto angalau upige story uambulie nae haweki msosi mezani, unaamua kuangalia movie moaka unasinzia msela anaamka anakula akizan uko fofofo unajikaza ale amalize bila kuamka ili usimkate stimu, akimaliza kula unaamka unasepa, unafika geto unakunywa maji unalala, usingizi hauji. Panakucha unaamua ukapambane kitaa unaambulia patupu. Kila dili ikija inakurika aisee unaona hapa hapanifai.
Unajitafuta unajipata wale wale wanaanza kutangaza unaringa, unajivuna sana, jamani mbona wakati wa msoto hamkusema nateseka nasota sana.
Ni bora ninunue sigara japo sivuti nizituoe lakini kuna watu siwezi kuwasaidia hata wapigane na nyoka ntakaa upande wa nyoka.
mbona vitu vya kawaida sana hivo bossIla tatizo ni kwamba humu jamiiforums karibu kila mtu ana degree, niashara inayomlipa / kazi ya maana, nyumba na gari....
Hata mimi naamini hivyo. Hii dunia haikuwa mahala pake.
Yule jamaa alikuwa na roho ya kipekee. Hakusubiri kuombwa.
Hii story yangu ni cha mtoto, baada ya mauti yake waliibuka wengi mno. Kuna aliowapa hifadhi ya makazi, aliowapa mitaji na hata aliolipia ada za watoto wao.
Kuna binadamu Mungu aliwaumba waje kuwa mfano wa wema tu kwa binadamu halafu waondoke.