Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Nilikuwa naishi na bibi yangu, kwakuwa hatukuwa na chakula ndani ikabidi aniache pekeyangu aende kwa baba zangu wadogo kuomba pesa ya matumizi.

Safari yake ilikuwa ya siku mbili kama sijakosea. Aisee nilishikwa na njaa nikachemsha yale mamchicha mekundu nikala baadae nikaenda kwa jirani nikakuta wanatoa vichwa kwenye samaki wadogo kanda ya ziwa tunawaita Furu.

Ikabidi niwaombe vile vichwa, nakumbuka nilidanganya naenda kumpa bata wangu. Nilichemsha vile vichwa nikala nikanywa na supu angalau nikawa vizuri.

Tulipokuwa tunapitia hali ngumu Bibi alijua ninaumia japo nilikuwa sisemi chochote alinitia moyo huku akilengwa na machozi "IPO SIKU UTAKULA VIZURI NA UTAKULA UNACHOKITAKA"
 
Kuna Mdau juu amesema mkewe mjamzito alikua anashindia Muwa. Nikaimajini wamama wajawazito wanavyopaswa kula mlo kamili na wasikae na njaa kisha nikaufikiria Muwa. Aiseh MAPITO NI MENGI.
Unaweza ukadhani ni masihara ila hivi vitu vipo mkuu, kuna muda nilikuwa naona kabisa vidonda vya tumbo vinanyimelea, ile njaa ya kukosa kula siku nzima unaona kabisa tumbo linawaka moto kama limemwagiwa tindi kali.

Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
 
Ili kuimarika kuna mapitio mengine ni muhimu kuyapitia ili yawe ukumbusho wa kukosa pale ukipata.

Ila kiukweli kabisa hakuna faraja kwenye ufukara.

Nakumbuka kuna kipindi nilipigika ikawa natembelea washkaji mida ya misosi kiasi cha kujua ratiba ya mlo wa masela wote.

Kuna msela wangu (Mungu amlaze mahala pema) ilikuwa ikifika jioni ananipigia simu kuniita tukapige story, kumbe alishajua hali yangu na ule wito ulikuwa ni msaada indirectly maana alihakikisha nakula ndio naondoka.

Na kila nikiondoka mkewe ananipa kikontena cha msosi ananiambia shem naona chakula cha leo umekipenda beba na hiki utakula baadae.
Hawakujua jinsi gani walikuwa wakinisevu.
Huyu mwanao ndo maana mungu alimpenda zaidi, alikuwa na moyo wa pekee
 
Unaweza ukadhani ni masihara ila hivi vitu vipo mkuu, kuna muda nilikuwa naona kabisa vidonda vya tumbo vinanyimelea, ile njaa ya kukosa kula siku nzima unaona kabisa tumbo linawaka moto kama limemwagiwa tindi kali.

Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
Njaa haizoeleki kaka.

Umesema kweli ukikipata kula ila pia kila unapojaaliwa kumpa mwingine chakula basi fanya hivyo.

Unaweza dharau kipande cha muhogo lakini kikamaanisha karamu kwa mwingine.
 
Nilipauka nkapauka kweli. Kulikuwa na maduka 2 ambayo nilikuwa mteja pendwa (very important uwe na maduka ambayo wewe ni customer wa kila siku), sasa nikaanza kukopa bwana. Nmekopa nkakopa tena ikafika kipindi mangi akaniambia, mjuba, sasa hivi unakopa mtaji, em nenda katafte kwanza uje upunguze madeni.
Nkakosa pa kwenda.

Sitasahau siku nmelala njaa. Imefika saa nane usingizi ukapaa na njaa takatifu, nikaenda bombani nkafungua maji nkanywa. Maji ya Dom yana chumvi wazee, ile chumvi ndo ikazidisha njaa kabisa.

Sikulala kabisa. Asubuh nmeamka hata nguvu ya kutembea sina. Msela wangu mmoja sijui alijuaje, akanipigia simu akanipa hi af akanitumia li twente ndo nkasogeza maisha.

This life be humble aisee.
 
Back
Top Bottom