Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kipindi Nikiwa na miaka 16, niliwahi kutiroka mateso ya mama mkubwa na kutembea kuanzia Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Hadi Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, umbali wa kilometa zaidi ya 400 kwa muda wa siku 19 kukatisha kioande cha mbuga ya tarangire. Kulikuwa na wanyama wengi isipokuwa simba, tembo na chui. Nikikutana na kundi kubwa la mbwa mwitu lakini Kama siku yako haijafika, haijafika tu.
Usirudie tena huo ujinga wa kukatiza mbuga za wanyama zenye mbwa mwitu.....

Umeskia we Dogo.
 
Huyu mwanao ndo maana mungu alimpenda zaidi, alikuwa na moyo wa pekee
Hata mimi naamini hivyo. Hii dunia haikuwa mahala pake.

Yule jamaa alikuwa na roho ya kipekee. Hakusubiri kuombwa.

Hii story yangu ni cha mtoto, baada ya mauti yake waliibuka wengi mno. Kuna aliowapa hifadhi ya makazi, aliowapa mitaji na hata aliolipia ada za watoto wao.

Kuna binadamu Mungu aliwaumba waje kuwa mfano wa wema tu kwa binadamu halafu waondoke.
 
Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
Nikusahishe kidogo mkuu, ukipata nafasi ya kula na unaijua njaa, ukijaliwa kupata nafasi ya kuwasaidia wengine chakula usifikirie mara mbili.... njaa sio kabisa.

Mimi mwizi nimkute kitu pekee alichoiba ni chakula nakausha tu
 
Nimeandika, nikafuta, nimeandika tena nikafuta…..aisee nikianza kueleza vile umasikini umenifanya server za JF zitajaa leo 😅, ila umasikini usikie kwa watu tu nyie 😂😂.

Cvez Jobless mwenzangu una lolote la kuchangia hapa? 😂😂😂

Acha tuendelee kula bata tu.
Kaka acha tu kufulia kusikie kwa jirani tu. Na nikifulia najikuta mikono inaishiwa nguvu kabisa na mwili unauma kama nimepigwa.

Maisha ya kuunga unga sio poa kabisa.
 
Unaweza ukadhani ni masihara ila hivi vitu vipo mkuu, kuna muda nilikuwa naona kabisa vidonda vya tumbo vinanyimelea, ile njaa ya kukosa kula siku nzima unaona kabisa tumbo linawaka moto kama limemwagiwa tindi kali.

Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
Najua Kile unasema. Life sucks aiseh
 
Nilipauka nkapauka kweli.
Kulikua na maduka 2 ambayo nilikua mteja pendwa (very important uwe na maduka ambayo wewe ni customer wa kila siku), sasa nkaanza kukopa bwana. Nmekopa nkakopa tena ikafika kipindi mangi akaniambia, mjuba, sasa hv unakopa mtajo, em nenda katafte kwanza uje upunguze madeni.
Nkakosa pa kwenda.
Sitasahau siku nmelala njaa. Imefika saa nane usingiz ukapaa na njaa takatifu, nkaenda bombani nkafungua maji nkanywa. Maji ya Dom yana chumvi wazee, ile chumvi ndo ikazidisha njaa kbsa.
Sikulala kabisa. Asubuh nmeamka hata nguvu ya kutembea sina.
Msela wangu mmoja sijui alijuaje, akanipigia sim akanipa hi af akanitumia li twente ndo nkasogeza maisha.
This life be humble aisee.
Muhimu sana kuwa na Duka unaloaminika. Yaani Unakuwa unafanya Madeni Recycling. Unalipa na kukopa hapo hapo.

Hakikisha unakuwa na hati safi hapo dukani ili uendelee kukopesheka siku za usoni.
 
Umenikumbusha mbali, nilikopa godoro nikailaza chini sikuwa na kitanda akaniongezea na stuli ya kukalia halafu nikaoa siku 15 mbele wakati wa jion wife anasonga ugali jamaa anapiga hodi karibu mara paap nataka pesa ya godoro na ya stuli mbele ya wife daah nikamuomba aniongezee siku 15 inafika asubuhi napiga mswaki kurudi ndani nikakuta wife kabeba vitu vyake kampelekea daah
 
Hata mimi naamini hivyo. Hii dunia haikuwa mahala pake.

Yule jamaa alikuwa na roho ya kipekee. Hakusubiri kuombwa.

Hii story yangu ni cha mtoto, baada ya mauti yake waliibuka wengi mno. Kuna aliowapa hifadhi ya makazi, aliowapa mitaji na hata aliolipia ada za watoto wao.

Kuna binadamu Mungu aliwaumba waje kuwa mfano wa wema tu kwa binadamu halafu waondoke.
Hawa binadamu unaweza kuta waliumbwa kuwa Malaika wakajikuta wapo duniani aiseh.
 
Na Daima shida zinakujaga kwenye hali hii ya mke na mtoto mdogo. Ile kauli ya SINA HATA MIA ukisikia mtu anasema unaweza sema ana utani.
Hii comment yako imenikumbusha mbali sana.

Kipindi cha mapito magumu nilikutana na ndugu kabisa wa mzee wangu. Nikamwambia hali halisi ya maisha.
Yule mzee alinijibu unakosaje hata mlo mmoja, huoni unajaza dunia tu si bora ungekufa na baba yako tu.

Hii kauli iliniliza kama mtoto mdogo.

Ila Mungu si wa mmoja, hivi karibuni tu kulipitishwa mchango wa kifamilia, mzee kashikwa na tezi dume analia kama mtoto. Watoto wake hakuna hata mmoja mwenye muelekeo.

Nilistopisha ule mchango na nikasimamia operation yake mpaka kutoka kwake hospitali.
Yule mzee anajifanya kasahau kila kitu ila najua nafsi yake inamsuta kila akiniona.
 
Kufulia wanakuita kwa kimombo "Broke", kwa kinaijeria "sapaa", kusikiage tuuuu!

Nakumbuka wiki nzima niliwahi kuwa na bajeti ya 200 kwa siku naenda kula mhogo wa kuchemsha, nje ya hapo natembea kama saa zima sehemu flani ilikuwa na miti ya mapera na peaches.

Nilikuwa napenda sana mambo ya simu na niliweza kuwarekebishia watu wengi vitu vya kwenye simu ila mimi nilikuwa na kitochi kimechoka.

Nilianza kuhesabu majina kwa cm huku nikisema Nani anaweza kuniazma bila kuanza kunipa darasa la maisha ama kunitangaza

Sendo yangu ilikatika upande moja nikawa naipiga msumali ijishike, baada ya siku 3 inaachia napigilia tena, ilijaa matundu kibao

Nilikuwa natoa nguo zote kwenye tenga na kuanza kusachi moja moja kama ina hela naambulia patupu, kesho narudia nazikunguta kabisa lakini wapi
Kufulia sio poa kabisa
 
Back
Top Bottom