Hii comment yako imenikumbusha mbali sana.
Kipindi cha mapito magumu nilikutana na ndugu kabisa wa mzee wangu. Nikamwambia hali halisi ya maisha.
Yule mzee alinijibu unakosaje hata mlo mmoja, huoni unajaza dunia tu si bora ungekufa na baba yako tu.
Hii kauli iliniliza kama mtoto mdogo.
Ila Mungu si wa mmoja, hivi karibuni tu kulipitishwa mchango wa kifamilia, mzee kashikwa na tezi dume analia kama mtoto. Watoto wake hakuna hata mmoja mwenye muelekeo.
Nilistopisha ule mchango na nikasimamia operation yake mpaka kutoka kwake hospitali.
Yule mzee anajifanya kasahau kila kitu ila najua nafsi yake inamsuta kila akiniona.