Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Usirudie tena huo ujinga wa kukatiza mbuga za wanyama zenye mbwa mwitu.....

Umeskia we Dogo.
 
Huyu mwanao ndo maana mungu alimpenda zaidi, alikuwa na moyo wa pekee
Hata mimi naamini hivyo. Hii dunia haikuwa mahala pake.

Yule jamaa alikuwa na roho ya kipekee. Hakusubiri kuombwa.

Hii story yangu ni cha mtoto, baada ya mauti yake waliibuka wengi mno. Kuna aliowapa hifadhi ya makazi, aliowapa mitaji na hata aliolipia ada za watoto wao.

Kuna binadamu Mungu aliwaumba waje kuwa mfano wa wema tu kwa binadamu halafu waondoke.
 
Ukipata nafasi ya kula aisee kula, kuna watu hiki chakula wanakitafuta hawakipati.
Nikusahishe kidogo mkuu, ukipata nafasi ya kula na unaijua njaa, ukijaliwa kupata nafasi ya kuwasaidia wengine chakula usifikirie mara mbili.... njaa sio kabisa.

Mimi mwizi nimkute kitu pekee alichoiba ni chakula nakausha tu
 
Kaka acha tu kufulia kusikie kwa jirani tu. Na nikifulia najikuta mikono inaishiwa nguvu kabisa na mwili unauma kama nimepigwa.

Maisha ya kuunga unga sio poa kabisa.
 
Najua Kile unasema. Life sucks aiseh
 
Muhimu sana kuwa na Duka unaloaminika. Yaani Unakuwa unafanya Madeni Recycling. Unalipa na kukopa hapo hapo.

Hakikisha unakuwa na hati safi hapo dukani ili uendelee kukopesheka siku za usoni.
 
Umenikumbusha mbali, nilikopa godoro nikailaza chini sikuwa na kitanda akaniongezea na stuli ya kukalia halafu nikaoa siku 15 mbele wakati wa jion wife anasonga ugali jamaa anapiga hodi karibu mara paap nataka pesa ya godoro na ya stuli mbele ya wife daah nikamuomba aniongezee siku 15 inafika asubuhi napiga mswaki kurudi ndani nikakuta wife kabeba vitu vyake kampelekea daah
 
Hawa binadamu unaweza kuta waliumbwa kuwa Malaika wakajikuta wapo duniani aiseh.
 
Na Daima shida zinakujaga kwenye hali hii ya mke na mtoto mdogo. Ile kauli ya SINA HATA MIA ukisikia mtu anasema unaweza sema ana utani.
Hii comment yako imenikumbusha mbali sana.

Kipindi cha mapito magumu nilikutana na ndugu kabisa wa mzee wangu. Nikamwambia hali halisi ya maisha.
Yule mzee alinijibu unakosaje hata mlo mmoja, huoni unajaza dunia tu si bora ungekufa na baba yako tu.

Hii kauli iliniliza kama mtoto mdogo.

Ila Mungu si wa mmoja, hivi karibuni tu kulipitishwa mchango wa kifamilia, mzee kashikwa na tezi dume analia kama mtoto. Watoto wake hakuna hata mmoja mwenye muelekeo.

Nilistopisha ule mchango na nikasimamia operation yake mpaka kutoka kwake hospitali.
Yule mzee anajifanya kasahau kila kitu ila najua nafsi yake inamsuta kila akiniona.
 
Kufulia sio poa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…