Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Tena mbaya zaidi iwe kwamba wewe baba yako kama alikuwepo hamkuwahi kulala njaa.

Unakuta wewe waweza jikaza ila wife na mtoto wenu kidume usoni ukiwacheki ni dhahiri kabisa njaa imewanyoosha si kidogo.

Unamwaga machozi usiku kimyakimya ili kulinda brand, asubuhi unaamka 12 kamili kucheki vibarua vya kubeba zege (hapo una degree au diploma ya chuo), unazunguka weeee hadi saa sita ni bila bila, mwili unatetemeka balaaa.

Wife akanitumia sms kuwa kakopa chapati 6 kwenye mgahawa uende ule ushushie na maji usije nikazimia mbele za watu.

Soma pia: Umaskini uusikie tu, Kipindi ukiwa ama kwa sasa ukiwa bado katika hali ya umasikini, ni changamoto zipi umepitia
 
Komaa upate kikazi,afu usikae mjini kaa kijijini
 
Nakumbuka kunakipindi,mshua alilazwa km miezi mitatu hivi so mishe zikasimama hapo nikiwa nipo chuo semista ya kwanza,acha kabisa no hela so nikawa na bajeti ya Mia nne kwa siku natembea kutoka mikadi beach mpaka kivukoni natoa Mia mbili navuka unaingia chuo napiga pindi nasepa hakuna mda wa kukaa chuo,hapo nikawa navamia vipindi ili kwa wiki nawahi maliza vipindi,msosi bhana ilikuwa nipige miogo na chai ya kutosha au nisubiri jioni nipige kandoro ya baridi nilale,so ikingia likizo ya kitu km mwezi hivi hiyo Sasa ikawa noma nauli hamna xo nilikuwa napiga maji tu,nikiishiwa nguvu ni kuoga Mara tatu kwa siku nilitakata mzee mpaka wakaanza niuliza wewe VIP likizo hii ukipata mishe nin town lkn ukweli naujua Mimi nilisota Sana
 
Wanawake wengine wajanja, wakiona Maisha magumu, wanazoea nyumba zenye unafuu ukifika pale unasaidia kazikazi, wakipika chakula unakula na mtoto, kama kunachochote kitu unapewa unaondoka jioni, mi nimewakuta Sana home watu wa dizaini hii.
 
Rudi bush angalia mila zenu zipo sawa, kuna kaela huwa unatakiwa kuwapa wazee wako katika kipato chako cha kwanza chochote kile pita kwa shangazi wape chochote, ukiona bado, chungulia kwa babu shida ipo wapi,
SIAMINI KAMA MUNGU AMEUMBA MWANADAMU APATE SHIDA, shida zote huwa tunazikwaa hapahapa duniani.
 
Wife ana akili kuliko wewe.

Unashindwa kukopa?

Halafu mmelala njaa unaamka saa 12 unaona umewahi sana kuamka!!

Pole sana kaka kwa yote lakini, ila pambana sana
 
Umeyaiga haya? Au ndio mwenye shida atajiju.
 
Ulitakiwa umwambie kwanini bado upo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…