Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Kuna mwanajeshi mmoja yeye alikuwa akilala pikipiki yake anaitoa upepo alafu anaimwaga wese lote, sasa siku nahiyo wanyama wakatinga ndani, wakampulizia dawa kama kawaida yao, Walipofika kwenye Honda wakakuta haina upepo, jamaa wakatafuta pump, wakajaza, wakaenda kutafuta mafuta wakaweka, wakaiwasha wakala kona, jamaa asubuhi anaamka anakuta alama za matairi tu, ndio baadhi ya majirani wakasema usiku tulisikia pikipiki ikiwashwa ndani mwako....
 
Nakumbuka jirani yetu walishamliza kwa style hi yani walikomba mpaka chaga za vitanda wakamuandikia ukutani "LALA UNONO" yeye na mama watoto wake na watoto pia walishtuka saa 4 asubuhi wamelazwa sakafuni wakiwa na nguo walizovaa tu zingine wameondoka nazo,Jirani alichanganyikiwa akawa kama chizi vile mana wale wezi walikuja na Gari kubeba
 
Dawa ni kuweka maji Sebureni katika beseni kila ukilala ile dawa ikipulizwa inaishia ktk maji hata chumbani fanya hivyo kiasi kidogo cha maji kiwe wazi wakipuliza utaona Rangi ya hiyo dawa au povu limejaa katika beseni hilo..
 
Nyia rahisi ya kuwazuia ni kuwa na nyumba yenye madirisha ya vioo ili wakianza kuvunja kioo uweze kuwasikia na kuamka na kingine hakikisha ukilala hufungulii radio/mziki kwa saut kubwa kwani itakufnya usisikie wkti wanavunja kioo cha dirisha lko
 
Pole sana, hao wezi wako ni balaaa
 
Hahaha nasikia wanakugusagusa na limjiti kwanza Shuwain sana hahaha
Wapo wanaozungushia nyumba yako na udongo wa makaburini. Ukilala haustuki mpaka wakitoka mlango wa nyumba yako, mengine ni imani za kishirikina
 

Wezi si watabiri kujua nani ana home theater na TVs za nguvu, unao wakaribisha ndani ndio ufanya michongo ya kukuibia!!

Ndio maana siku hizi nyumba anahakikisha kuna chumba cha family huko nfiko unaweka vitu vya gharama, kwenye sebure anaweka vitu vya kawaida visivyo vya gharama na huko ndiko unawakaribisha wageni siyo chumba cha familia - wakati mwingine ni vizuri kutumia common sense.

Nimewashauri tena kwamba fungeni electronic alarms zenye kutoa mlio mkali ambao unaweza kuwamusha majirani na aizimiki mpaka u- reset mwenyewe, kuna sensors za infrared zina uwezo wa kutambua warm blooded animals wakiwemo wanadamu mita ishirini/thelathini/ kabla hafika nyumbani kwako hata ikiwa giza totoro, kuna sensor zinatambua mtu akivunja kioo cha dirisha hata akitumia dawa za ........ nk.
 
Kaka kuna watu na shunguri zao aisee. Mie nlikuwaga mbishi kama wewe, kuna mzee mtaan aliibiwa bajaj kwake aisee. Wezi walikuja ucku wakafungua get wakaiba bajaj.

Yule mzee hakwenda kushtak hata polisi. Ila baada ya siku kama mbili hivi wale wezi walirudisha bajaj huku wanaikokota.

Yule mzee hakushtuka aliwafungulia geti wakapak bajaj akamwambia mkewe awape naul wakaenda. Hata hawakuguswa wale wezi.

Kuna watu na shughuri zao
 
Nyia rahisi ya kuwazuia ni kuwa na nyumba yenye madirisha ya vioo ili wakianza kuvunja kioo uweze kuwasikia na kuamka na kingine hakikisha ukilala hufungulii radio/mziki kwa saut kubwa kwani itakufnya usisikie wkti wanavunja kioo cha dirisha lko

Mkuu kuna madawa ya kupukutisha kioo bila ya wewe kusikia, si chemistry tu - vioo asilimia kubwa ya mali ghafi ni mchanga wa baharini - wanatumia madawa si nyundo wala jiwe kwa hiyo usitegemee kusikia sauti yoyote - chunga sana.
 
Hakikisha unakuwa na chombo chenye maji chumbani/vyumbani mfano maji kwenye ndoo.ikipulizwa hiyo dawa inakwenda kwenye maji.maji yakikosekana inakimbilia sehemu za unyevunyevu kama puani.utakuwa umeibiwa
 
Bwana MUNGU asipoilinda nyumba, wailindao wakesha bure Zaburin127. Dawa yangu ni Zaburn121, nitayainua macho yangu niitazame milima, msaada wangu utatoka wapi?Msaada wangu u katika BWANA aliyezifanya mbingu na nchi.
 
Akikamatwa mwizi ni kumyanganya tu silaha kama alivyoagiza kamanda wetu mpendwa. Hii nimeipenda sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…