View attachment 370942 View attachment 370941
Hii nimeiona kwenye Group la WhatsApp,imetokea mitaa ya Segerea Dsm...Jamaa walikuja usiku wa kiza kinene,wakapiga dawa dirishani wakaanza kupakuwa kitu kimoja baada ya kingine!!Chumbani walishindwa kuingia ikabidi watumie hilo "jaro" kupakuwa simu kitandani.
Wakazungukia kwa wapangaji wengine wakakomba kila kitu.Wakapakuwa kiporo cha ubwabwa wa kipaimara wakala,wakafungua friji wakanywa juice yote na matunda.Wakaenda na bafani wakaoga na kujisaidia bila kuflash ...wakafungua TV ukutani ya nchi 32 na mziki sebuleni...baada ya hapo wakakojolea kwenye vikombe na masufulia,ajabu ni kuwa haya yote yanatokea hakuna hata aliyeamka.
Walioibiwa wamekuja kuamshwa saa tano asubuhi,maana gari ya shule "school bus" ilikuja kuwabeba watoto ikapiga sana honi bila mafanikio...aliyekuja kustua majirani ni Mama msaidizi wa kazi ambaye huwa anasidia kazi na kurudi nyumbani.Watoto wamelazwa chini jamaa wamebeba mashuka na mito.
Hivi hawa jamaa dawa yao nini??Maana imekuwa kero sana kwa sasa....Yaani wameiba na kumpaka mtu white dent eneo la "mtaro wa maji machafu" halafu wakatoweka....sio haki kabisaaaaaa