Ni dhahiri Mahakama ya Tanzania ni mshirika mkuu wa kutotenda haki nchini

Ni dhahiri Mahakama ya Tanzania ni mshirika mkuu wa kutotenda haki nchini

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na mambo ya kusikitisha sana kutoka kwa mhimili wa mahakama.

Mwendenendo wa Mahakama zetu nchini umekuwa ni mwenendo usio na afya njema katika utoaji wa haki nchini, na kwa bahati mbaya inaonekana mahakama yetu imeridhika na kuridhia hali hii na matokeo yake tunaona leo hii kesi hasa zile zenye maslahi ya kwa watawala zinaamuliwa kiajabu ajabu bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo unaumiza wananchi.

1. Kauli ya Jaji Mkuu kuwataka majaji waamue kesi si kwa kuangalia sheria tu bali waangalie na mihimili mingine inasema nini

Wakati akimuapisha Jaji kiongozi (Mustafa Seyani), Jaji Mkuu alitoa kauli hilo, Hii maana yake nini?, maana yake ni kuwa Majaji sasa wanakwenda kuingiza ndani ya hukumu zao matashi na miongozo ya watawala, miongozo ya watawala. Kwahiyo Jaji mkuu anaagiza mahakama icompromise wajibu wake wa kutafsiri sheria zilizotungwa na bunge na kutenda haki na badala yake majaji waanze kutafsiri sheria katika lenzi ya watawala wanataka nini. Kwa kweli hii kauli na agizo la jaji mkuu ni ya kusikitisha sana. Kiufupi ameiweka mahakama katika nafasi ya kucollaborate kufanya dhulma katika nchi!

2. Kumekuwepo na rushwa ya madaraka kwa majaji

Kipindi cha Magufuli, Hakimu aliyetoa hukumu ya kuwafunga akina Mbowe na Msigwa (kesi ya Akwilina Akwilin) alipandishwa cheo na kuwa Jaji, Hakimu aliyemfunga Sugu alipandishwa cheo na kuwa Jaji. Na hukumu za mahakimu wote hao baadae zilitenguliwa na mahakama za juu, Leo Jaji Seyani akiwa anakaribia kutoa hukumu ya shauri dogo linalohusu wasaidizi wa Mwenyekiti Mbowe katika kesi inayomhusu pia Mwenyekiti Mbowe anapandishwa cheo na kuwa Jaji kiongozi. Hii kama siyo rushwa ni nini?. Hawa Majaji wakiletewa kesi zenye maslahi kwa watawala ambao waliwateua watatenda haki kweli?Mfumo wa mahakama unaoruhusu, kukubali, kushiriki na kubariki teuzi za namna hii kimsingi ni mfumo ambao uko tayari kutumika kuharibu haki nchini

3. Precedence ya hukumu hizi zinazotolewa kuridhisha watawala zitaumiza wananchi kwa miaka mingi ijayo, sijui kama Majaji wetu wanalifahamu hilo.

Leo hii Jaji Seyani anaenda kutoa hukumu, hanukuu kifungu chochote cha sheria kujustify hukumu yake. Anatoa hukumu kwa "kudhani", "kwa maoni yake binafsi", hafanyi reference yoyote. Hii inaweka precedence gani?. Jaji anatoa hukumu bila kuzingatia miongozo na sheria za kipolisi katika ukamataji, uchukuaji wa maelezo, na ushahidi wa wazi wa watuhumiwa kuteswa, na yeye jaji anakiri kuwa kuwa mtuhumiwa anaonekana aliumizwa sana, lakini anatoka hapo anatoa hukumu ya kumnyima haki victim. Hii inaweka precedence gani katika utendaji wa jeshi la polisi?, Maana yake ni kuwa jeshi la polisi litakamata watu, kuwatesa, na mahakama za chini zijazo zitatumia hukumu ya Jaji Seyani kama reference ya kujustify matendo yao. Laiti Jaji Seyani angejua Damage aliyoifanya katika mizania ya haki nchini, basi cheo chake hicho cha Ujaji Kiongozi angeona si lolote si chochote!. Binafamu umri wetu ni mdogo sana, Haya mavyeo ya kukaa nayo muda mchache yanafaa nini halafu unaondoka duniani unaacha precedence za kuumiza watu kwa miaka lukuki?

4. Mahakama imekuwa ikishiriki michezo ya mhimili wa dola kutesa, kupotezea muda watu

Tumeona kesi nyingi zikitajwa tu lakini mashauri hayaanzi, eti ushahidi haujakamilika, kesi zinachukua hata miaka. Mahakama inao uwezo wa kufutilia mbali kesi za namna hiyo. Watu wanaumia, lakini as long as kesi ni za kisiasa, au mhimili wa serikali umeweka mkono wake, Mahakama haifurukuti kutenda haki. Tuliona hilo kwenye kesi ya Masheikh wa uamsho, na zipo kesi nyingi nchini za namna hii. Sasa katika mazingira haya hii mahakama ni ya kuaminika?

HITIMISHO
1. Hatuna mahakama huru Tanzania, ni wajibu wa kila mwananchi anayejielewa kupigani katiba mpya ili ndani yake tupate mfumo wa mahakama ulio huru

2. Ni dhahiri kuna ushirika usio mtakatifu wa mihimili hii mitatu, na kwa bahati mbaya mfumo wa Mahakama nchini umeamua kujidogosha tena wakati mwingine bila sababu za msingi, na hivyo tegemea tu kutotendewa haki iwapo serikali imedhamiria usipate haki. Serikali ikikukamia huna kimbilio

3. Hukumu za hawa majaji, ambao teuzi zao ni za mashakamashaka ni msumali wa moto katika uwanja wa haki nchini. Kamwe hawatokuwa watu wa haki, bali siku zote watalinda maslahi ya waliowateua

4. Jaji Mkuu ameshindwa kuwa mkuki wa haki nchini. Kwa hukumu zote kandamizi, na Maagizo anayoyatoa ya namna kesi ziendeshwe, ni dhahiri hakuna namna haki nchini inaweza kusitawi chini ya uongozi wake au uongozi wa aina yake, Ajitafakari aone mbona wenzie akina cjief justice Nyalali walikuwa hawana mambo kama yake, anashindwa nini kujifunza kutoka kwao?
 
Mkuu acha unafiki.

kwa maoni yako na wafuasi wa Mbowe kwa wao ili waone Haki imetendeka wanataka Mahakama iamue kama wanavyo taka wao.

kinyume chake wanaibuka na madai ya kuchafua vyombo vyetu!! na kudai Mahakama haija tenda haki.

Huo sio utawala wa sheria, utawala wa sheria ni kuheshimu maamuzi yoyote ya Mahakama.

2. Mlitaka Asiteuliwe kuwa Jaji kiongozi eti kisa anasikiliza kesi ya Mbowe?! huo utaratibu wa wapi!! hoja za kitoto kabisa!!

Jaji Siyani ana sifa zote nzuri hata wafuasi wa Mbowe walimsifu sana tena sana sasa kutokana na sifa hizo alizo nazo za uadilifu zimempendeza Mhe. Rais na Kumteua awe msimamizi wa Majaji wote sasa tatizo lipo wapi hapo?!


Ifike mahali Vyombo vyetu vinapaswa kukemea tabia hii ya wafuasi wa Mbowe kutaka kushinikiza Mahakama ziamue kama wanavyotaka wafuasi wa mbowe, hili ni jambo hatari sana ktk utendaji wa Haki.

Mtoa mada uchambuzi wake hauna uthibitisho zaidi ya hisia zenye lengo la kuushinikiza Muhimili wa mahakama kutenda haki kwa jinsi wanavyo taka wao.
Mbowe na genge lake wanataka kuziendesha Mahakama, Polisi na vyombo vingine kwa mbinu za kubeza na kudhihaki n.k, vyombo vyote vinapaswa kuwa Makini sana wa genge hili kamwe wasikubali kuhadaiwa na kauli za genge hili.

Mahakama haiendi hivyo.
 
Mkuu acha unafiki.
kwa maoni yako na wafuasi wa Mbowe kwa wao ili waone Haki imetendeka wanataka Mahakama iamue kama wanavyo taka wao!!
kinyume chake wanaibuka na madai ya kuchafua vyombo vyetu!! na kudai Mahakama haija tenda haki!!.
Huo sio utawala wa sheria, utawala wa sheria ni kuheshimu maamuzi yoyote ya Mahakama.

2. Mlitaka Asiteuliwe kuwa Jaji kiongozi eti kisa anasikiliza kesi ya Mbowe?! huo utaratibu wa wapi!! hoja za kitoto kabisa!!

ifike mahali Vyombo vyetu vinapaswa kukemea tabia hii ya wafuasi wa Mbowe kutaka kushinikiza Mahakama ziamue kama wanavyotaka wafuasi wa mbowe, hili ni jambo hatari sana.
Nadhani hii mada inakuzidi kimo

Tunazungumzia mustakbali wa haki za mamilioni ya Watanzania kutokana na precedence ya hizi kesi.
 
Mkuu acha unafiki.
kwa maoni yako na wafuasi wa Mbowe kwa wao ili waone Haki imetendeka wanataka Mahakama iamue kama wanavyo taka wao!!
kinyume chake wanaibuka na madai ya kuchafua vyombo vyetu!! na kudai Mahakama haija tenda haki!!.
Tanzania ni nchi ngumu sana
 
Nadhani hii mada inakuzidi kimo

Tunazungumzia mustakbali wa haki za mamilioni ya Watanzania kutokana na precedence ya hizi kesi.
Ndugu yangu, umeleta hoja njema sana yakujadilika na ambayo ilistahili hata majaji, mahakimu, mawakili na wajuzi wa katiba na sheria ndio tuwaone hapa wakiweka maoni yao kukuunga mkono au kukupinga kwa hoja za kisheria.

Lakini bahati mbaya kwa JF wapo watu "dhaifu wa akili" kama huyu uliyemjibu wanaopoteza maana ya hoja kuu.

Please usipoteze muda kuwajibu.
 
Lawama zote ziende kwa aliyeleta mfumo wa Sheria na MAHAKAMA.

Siyo mfumo sahihi wa kutenda haki bali kutafsiri kwanini haki mtu /kundi fulani limepewa haki hata kama haikustahili kuhamishiwa kwake.
 
Yawezekana Mbowe ni Gaidi lakini maamuzi ya Jaji Siyani yaliyokosa sapoti ya kifungu chochote cha sheria yanatufanya tuamini Mbowe anaonewa.
 
Mkuu ukiandikaga uzi unaohusu haki za wavaa vibalakashia wenzio wanakukimbia na wengine kukutolea maneno ya kashfa nk. Lkn ukiandika upuuzi kama huu wote wanasogea kuchangia na kukupongeza kwa upuuzi ulioandika. Hapo ndo ujue kuwa unatetea wanafiki wanaojali masilahi yao na sio masilahi ya Taifa. Pole sana kijana kwa kuingizwa chaka na wanasiasa uchwara.
 
Binadamu watu wa ajabu sana.

Kwakuwa hakijatendeka kile ulichotarajia ndo una finalise eti hakuna mahakama nchini na majaji hawafanyi kazi kwa weledi mbona haya hukuyasema kwa kesi ya Sabaya bali mliishia kushangilia na kuisifu mahakama ile ile unayoilalamikia leo?

Tuache unafiki, tuacheni mahakama itimize majukumu yake kama ilivyokuwa kwa kesi nyingine ikiwemo ya Sabaya!

WATU KAMA NYIE KWA UNAFIKI HUU NDIO MNAFANYA HATA JUHUDI ZA KUDAI KATIBA MPYA ZIWE MFU, MNAANGALIA MASLAHI YENU TU NA SI YA UMMA MNATEGEMEA NANI ATAWAUNGA MKONO?

TUTAELEWANA TU!
 
Tuna mahakama ya hovyo kabisa kuwahi kutokea

Ni week moja tu iliyopita, tuliisifu kwa furaha kubwa Mahakama kwa kutenda haki na kufanya kazi kwa weledi kwenye kesi ya Sabaya. Lakini kumbuka kuna upande pia wa watu waliamini hiki unachokisema wewe kwa comment kuhusu hukumu hiyo hiyo ya Sabaya.

Ni kawaida, maamuzi yakiwa si ya kufurahisha upande uupendao kutoa lawama. Tuiachie Mahakama ifanye kazi yake,naamini mbele ya safari kuna maamuzi pia yatatolewa na Mahakama hii hii unayoilaani sasa hivi na yatakufurahisha.
 
Ni week moja tu iliyopita,tuliisifu kwa furaha kubwa Mahakama kwa kutenda haki na kufanya kazi kwa weledi kwenye kesi ya Sabaya.Lakini kumbuka kuna upande pia wa watu waliamini hiki unachokisema wewe kwa comment kuhusu hukumu hiyo hiyo ya Sabaya.

Ni kawaida,maamuzi yakiwa si ya kufurahisha upande uupendao kutoa lawama.Tuiachie Mahakama ifanye kazi yake,naamini mbele ya safari kuna maamuzi pia yatatolewa na Mahakama hii hii unayoilaani sasa hivi na yatakufurahisha.
Matendo ya Sabaya yanaonekana kwenye CCTV camera na yeye anakiri kuwa alikuwa anatumwa na dikteta, pia dharau ambazo alikuwa anaonyesha waziwazi kwa watu kuvamia, kubaka n.k, haya tuambie Mbowe kafanya ugaidi wapi na kachoma kituo kipi cha mafuta?
 
Back
Top Bottom