Ni dhahiri Mahakama ya Tanzania ni mshirika mkuu wa kutotenda haki nchini

Ni dhahiri Mahakama ya Tanzania ni mshirika mkuu wa kutotenda haki nchini

Wewe ni wale wafuasi wa yule Makengeza aliyeko mahabusu! Acheni unafiki ni lini binadamu akatoa haki? Juzi hapa Sabaya afungwa miaka 30! Ok hakuna tatizo nyinyi kikundi cha Chagadema mnakuja kusema tena leo mahakama haitoi haki? Juzi mmeshinda mnakuvywa bia mbaya wenu kafungwa! Mbowe sisemi kama ni gaidi iachieni nafasi mahakama kama ilivyokuwa kwa Sabaya!
kwel ww nguchiro
 
Niseme ukweli, binafsi bado naiamini mahakama ya rufaa kwenye kutoa maamuzi ya haki, mpaka pale watakapofanya vinginevyo ndio imani yangu kwao itaondoka.
mbowe anakula miaka ya maisha, BELIEVE ME /NOT. anavuna alichokipanda,ukimchezea Simba mzee sharubu vya kutosha mwisho hatakuvumilia atalala mbele na wewe!!

baada ya hukumu ya gaidi mbowe,tunafunga season,inayoitwa the last crime in Tanzania!! Halafu tunaanza na maisha mapya kabisaa,na utulivu mpya kabisaa,siasa mpya kabisaaa!!
 
Shortly mifumo yote inabidi ifumuliwe(katiba mpya)ukizingatia katika mihimili yote miwili iliyobakia hakuna mhimili unaoweza kuijia juu serikali iliyojichimbia chini,ikiwa mihimili hiyo yenyewe inahitaji kuwezeshwa na serikali katika kutimiza majukumu yao.
 
Hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na mambo ya kusikitisha sana kutoka kwa mhimili wa mahakama.

Mwendenendo wa Mahakama zetu nchini umekuwa ni mwenendo usio na afya njema katika utoaji wa haki nchini, na kwa bahati mbaya inaonekana mahakama yetu imeridhika na kuridhia hali hii na matokeo yake tunaona leo hii kesi hasa zile zenye maslahi ya kwa watawala zinaamuliwa kiajabu ajabu bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo unaumiza wananchi.

1. Kauli ya Jaji Mkuu kuwataka majaji waamue kesi si kwa kuangalia sheria tu bali waangalie na mihimili mingine inasema nini

Wakati akimuapisha Jaji kiongozi (Mustafa Seyani), Jaji Mkuu alitoa kauli hilo, Hii maana yake nini?, maana yake ni kuwa Majaji sasa wanakwenda kuingiza ndani ya hukumu zao matashi na miongozo ya watawala, miongozo ya watawala. Kwahiyo Jaji mkuu anaagiza mahakama icompromise wajibu wake wa kutafsiri sheria zilizotungwa na bunge na kutenda haki na badala yake majaji waanze kutafsiri sheria katika lenzi ya watawala wanataka nini. Kwa kweli hii kauli na agizo la jaji mkuu ni ya kusikitisha sana. Kiufupi ameiweka mahakama katika nafasi ya kucollaborate kufanya dhulma katika nchi!

2. Kumekuwepo na rushwa ya madaraka kwa majaji

Kipindi cha Magufuli, Hakimu aliyetoa hukumu ya kuwafunga akina Mbowe na Msigwa (kesi ya Akwilina Akwilin) alipandishwa cheo na kuwa Jaji, Hakimu aliyemfunga Sugu alipandishwa cheo na kuwa Jaji. Na hukumu za mahakimu wote hao baadae zilitenguliwa na mahakama za juu, Leo Jaji Seyani akiwa anakaribia kutoa hukumu ya shauri dogo linalohusu wasaidizi wa Mwenyekiti Mbowe katika kesi inayomhusu pia Mwenyekiti Mbowe anapandishwa cheo na kuwa Jaji kiongozi. Hii kama siyo rushwa ni nini?. Hawa Majaji wakiletewa kesi zenye maslahi kwa watawala ambao waliwateua watatenda haki kweli?Mfumo wa mahakama unaoruhusu, kukubali, kushiriki na kubariki teuzi za namna hii kimsingi ni mfumo ambao uko tayari kutumika kuharibu haki nchini

3. Precedence ya hukumu hizi zinazotolewa kuridhisha watawala zitaumiza wananchi kwa miaka mingi ijayo, sijui kama Majaji wetu wanalifahamu hilo.

Leo hii Jaji Seyani anaenda kutoa hukumu, hanukuu kifungu chochote cha sheria kujustify hukumu yake. Anatoa hukumu kwa "kudhani", "kwa maoni yake binafsi", hafanyi reference yoyote. Hii inaweka precedence gani?. Jaji anatoa hukumu bila kuzingatia miongozo na sheria za kipolisi katika ukamataji, uchukuaji wa maelezo, na ushahidi wa wazi wa watuhumiwa kuteswa, na yeye jaji anakiri kuwa kuwa mtuhumiwa anaonekana aliumizwa sana, lakini anatoka hapo anatoa hukumu ya kumnyima haki victim. Hii inaweka precedence gani katika utendaji wa jeshi la polisi?, Maana yake ni kuwa jeshi la polisi litakamata watu, kuwatesa, na mahakama za chini zijazo zitatumia hukumu ya Jaji Seyani kama reference ya kujustify matendo yao. Laiti Jaji Seyani angejua Damage aliyoifanya katika mizania ya haki nchini, basi cheo chake hicho cha Ujaji Kiongozi angeona si lolote si chochote!. Binafamu umri wetu ni mdogo sana, Haya mavyeo ya kukaa nayo muda mchache yanafaa nini halafu unaondoka duniani unaacha precedence za kuumiza watu kwa miaka lukuki?

4. Mahakama imekuwa ikishiriki michezo ya mhimili wa dola kutesa, kupotezea muda watu

Tumeona kesi nyingi zikitajwa tu lakini mashauri hayaanzi, eti ushahidi haujakamilika, kesi zinachukua hata miaka. Mahakama inao uwezo wa kufutilia mbali kesi za namna hiyo. Watu wanaumia, lakini as long as kesi ni za kisiasa, au mhimili wa serikali umeweka mkono wake, Mahakama haifurukuti kutenda haki. Tuliona hilo kwenye kesi ya Masheikh wa uamsho, na zipo kesi nyingi nchini za namna hii. Sasa katika mazingira haya hii mahakama ni ya kuaminika?

HITIMISHO
1. Hatuna mahakama huru Tanzania, ni wajibu wa kila mwananchi anayejielewa kupigani katiba mpya ili ndani yake tupate mfumo wa mahakama ulio huru

2. Ni dhahiri kuna ushirika usio mtakatifu wa mihimili hii mitatu, na kwa bahati mbaya mfumo wa Mahakama nchini umeamua kujidogosha tena wakati mwingine bila sababu za msingi, na hivyo tegemea tu kutotendewa haki iwapo serikali imedhamiria usipate haki. Serikali ikikukamia huna kimbilio

3. Hukumu za hawa majaji, ambao teuzi zao ni za mashakamashaka ni msumali wa moto katika uwanja wa haki nchini. Kamwe hawatokuwa watu wa haki, bali siku zote watalinda maslahi ya waliowateua

4. Jaji Mkuu ameshindwa kuwa mkuki wa haki nchini. Kwa hukumu zote kandamizi, na Maagizo anayoyatoa ya namna kesi ziendeshwe, ni dhahiri hakuna namna haki nchini inaweza kusitawi chini ya uongozi wake au uongozi wa aina yake, Ajitafakari aone mbona wenzie akina cjief justice Nyalali walikuwa hawana mambo kama yake, anashindwa nini kujifunza kutoka kwao?
Asante kwa waraka wako mrefu kupita kiasi. Nimesoma nusu tu nitamalizia baadae.
 
Yote yatafika mwisho siku tukiumia wote kama taifa
 
Matendo ya Sabaya yanaonekana kwenye CCTV camera na yeye anakiri kuwa alikuwa anatumwa na dikteta, pia dharau ambazo alikuwa anaonyesha waziwazi kwa watu kuvamia, kubaka n.k, haya tuambie Mbowe kafanya ugaidi wapi na kachoma kituo kipi cha mafuta?
Hahaha. Ugaidi tusubiri mwisho wa kesi kwani tutaelezwa na waliosema Gaidi . Kesi ya ugaidi inaendelea.
 
Kwahiyo waliofurahia kifungo cha Sabaya hawakuwa sahihi maana huenda kaonewa au sio?
Sabaya aliumiza watu na hata sizimizi anajua hilo halina ubishi na mawakili wake hawakuwa na pingamizi na huku hiyo .

Utolewaji wa hukumu ilivyokuwa kwa Sabaya na hapo nitofauti mbona jaji hakuonesha vipengele vya sheria bali anasema kwa uono wangu nihivi na hivi. Ndio sheria ya hukumu inavyotaka?

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Mimi mbona nikishashtuka mda mrefu,humu jf Kuna watu wapo kwenye paylor kila mwezi ,ili tu kupotosha ,na kutaka kushinikiza mahakama iamue jinsi watakavyo kuhusu kesi ya ugaidi ya mbowe!!.
Paylor ndio kitu gani?
 
Mkuu acha unafiki.

kwa maoni yako na wafuasi wa Mbowe kwa wao ili waone Haki imetendeka wanataka Mahakama iamue kama wanavyo taka wao.

kinyume chake wanaibuka na madai ya kuchafua vyombo vyetu!! na kudai Mahakama haija tenda haki.

Huo sio utawala wa sheria, utawala wa sheria ni kuheshimu maamuzi yoyote ya Mahakama.

2. Mlitaka Asiteuliwe kuwa Jaji kiongozi eti kisa anasikiliza kesi ya Mbowe?! huo utaratibu wa wapi!! hoja za kitoto kabisa!!

Jaji Siyani ana sifa zote nzuri hata wafuasi wa Mbowe walimsifu sana tena sana sasa kutokana na sifa hizo alizo nazo za uadilifu zimempendeza Mhe. Rais na Kumteua awe msimamizi wa Majaji wote sasa tatizo lipo wapi hapo?!


Ifike mahali Vyombo vyetu vinapaswa kukemea tabia hii ya wafuasi wa Mbowe kutaka kushinikiza Mahakama ziamue kama wanavyotaka wafuasi wa mbowe, hili ni jambo hatari sana ktk utendaji wa Haki.

Mtoa mada uchambuzi wake hauna uthibitisho zaidi ya hisia zenye lengo la kuushinikiza Muhimili wa mahakama kutenda haki kwa jinsi wanavyo taka wao.
Mbowe na genge lake wanataka kuziendesha Mahakama, Polisi na vyombo vingine kwa mbinu za kubeza na kudhihaki n.k, vyombo vyote vinapaswa kuwa Makini sana wa genge hili kamwe wasikubali kuhadaiwa na kauli za genge hili.

Mahakama haiendi hivyo.
Sasa wewe Kama una akili timamu, umewahi wapi duniani kusomwa hukumu bila kifungu chochote cha sheria kunukuliwa?
 
Hapa umeonesha ujinga wako wa kutozingatia kile unachosoma. Hebu soma vizur post yang afu urudi kwenye huu utumbo ulioweka hapa. Boganza anasema kuwa kuna wakati mahakamani kunaweza kukosekana haki ndio maana na mimi nikashangaa watu kufurahia hukumu ya sabaya bila kujua kuwa haki ilitendeka au haikutendeka kumuhukumu. Afu ww na kiwewe cha mahaba yako kwa Mbowe umekimbilia kupost yale yale niliyomaanisha. Sasa hii ni akili au matope!!

Ndege Dudumizi siyo fair kuni redirect kwenye utumbo wako, huo baki nao mwenyewe!
 
Jamaa ameeleza vizuri hapo juu japo unajaribu kupambana naye kama kawaida..

Unafikiri mahakama ifanye nini ili wewe uone imetenda haki...maana mtazamo ninaouona hapa ili mahakama iwe imetenda haki lazima Mbowe aachiwe na asipoachiwa mahakama itakuwa bado haijatenda haki kwako...

Sheria ni taalum, mahakamani kuna majaji na mawakili wa pande zote wanachuana kwa kutumia taaluma zao, hebu tuache taaluma zao zifanye kazi na mwisho wa siku zitatoa majibu... kila upande unatafuta haki ni jukumu la mawakili kuonyeshana uwezo wa kupanga na kupangua hoja na mwisho wa siku jaji au majaji watatoa hukuma...

Tusiwe na hizi hulka za kuamini tuko sahihi muda wote na wao ni waonevu na
 
tunapolalamika kila siku tunaonewa inapita na siku zinaenda hatuchukui hatua zozote kuna mahala watu tunaweza kuamini hamuonewi bali ndio haki yenu..

Mfano mkionewa mkapeleka mashitaka mahakama ya Africa, mkaenda UN pale kulalamika, mkawa mnafungua makesi kila siku hapahapa, mkaandamana mkapigwa mkaumizwa watu wakafa lakini mkidai haki....hakuna haki inayokuja kwa kulialia na kutia huruma pasipo kuipigania..
 
Binadamu watu wa ajabu sana.

Kwakuwa hakijatendeka kile ulichotarajia ndo una finalise eti hakuna mahakama nchini na majaji hawafanyi kazi kwa weledi mbona haya hukuyasema kwa kesi ya Sabaya bali mliishia kushangilia na kuisifu mahakama ile ile unayoilalamikia leo?

Tuache unafiki, tuacheni mahakama itimize majukumu yake kama ilivyokuwa kwa kesi nyingine ikiwemo ya Sabaya!

WATU KAMA NYIE KWA UNAFIKI HUU NDIO MNAFANYA HATA JUHUDI ZA KUDAI KATIBA MPYA ZIWE MFU, MNAANGALIA MASLAHI YENU TU NA SI YA UMMA MNATEGEMEA NANI ATAWAUNGA MKONO?

TUTAELEWANA TU!
Nadhani binadamu wa ajabu utakuwa wewe usiye jaribu kutumia akili alizokupa muumba wako bali unatumia hisia na ushabiki wako maandazi.
Hivi unawezaje kulinganisha watu hawa, Mbowe na Sabaya?
Hata katika hali ya kawaida, weka uchama pembeni nenda kwenye maisha ya kawaida. Wale watu walio kuwa wanalalamika kutendwa ukatili na dhuluma, kubakwa, kuporwa mali zao, kupigiliwa misumari miguuni na kukatwa masikio hukuona? Sabaya aliyotenda yalikuwa ni mambo ya wasaidizi wa Amini kule Uganda wewe unaona kawaida? Mtu akikuita jina baya mfano mpumbavu utamshangaa wakati unatetea upumbavu?
Nenda kwa Mbowe, hivi zaidi ya hao Polisi kusema alipanga ugaidi nani umewahi msikia akilalamika kutendewa baya na Mbowe? Acha ushabiki usio tija mkuu! Kwa Sabaya ukimtetea lazima uonekane mjinga maana hata waliokuwa wanamlinda na kumtuma wamejitenga naye, wewe ni nani wakusimama na kumtetea jangili kama Sabaya?
Kafungwa tena na mahakama za ccm, ana kesi nyingine kisha ana kesi nyingine Moshi. Na wapo wasio taka kuharibu majina yao wangemfungulia mashtaka kama Nandy lakini wanaogopa kuharibu Brand zao. Bado wamuona mtu huyo?
Simama kwenye ukweli utaheshimika bwana Lucas Philipo
 
Hata ww huoni kwamba mtu kateswa namna hiyo je angekuwa ndugu yako ungeona uamuzi wa mahakama uko swwa? Ww hata kama ni mnufaika wa mfumo uliopo lkn haki za watu ni jambo la msingi, huyo mtuhumiwa alivyoteswa namna hiyo je haki yake anapata wapi na je angeteswa ndugu yako ungesema nn juu ya haki? Tuache kuwa wajinga kiasi hiki
 
Back
Top Bottom