Ni dhambi na nuksi kuoa mwanamke alieachika au kuachwa kwa mwanaume mwingine na angali huyo mwanaume yu hai

Ni dhambi na nuksi kuoa mwanamke alieachika au kuachwa kwa mwanaume mwingine na angali huyo mwanaume yu hai

Mkuu uko speed sana hebu tulia tuhabarishe juu ya dhambi na nuksi unazozungumzia.
KWENYE NDOA, WOTE MKE NA MUME WANA MCHANGO KATIKA ANGUKO LAO.
USIJE FIKIRI KWENYE NDOA MWANAMKE NI MTAKATIFU NA MWANAUME NDIO SHETANI SASA.

WANA NDOA WANA MENGI MABAYA WANAFANYIANA KIASI WAKITENGANA NAFSI INA UMA NA KUMSUTA MUHUSIKA.
NA MARA NYINGI MANUNG'UNIKO, NA MACHOZI YA MWENZIO YANAKUWA KIKWAZO KWAKO KWENYE NYANJA ZOTE KAMA MAHUSIANO MAPYA, UCHUMI, IMANI (HAPA KUNA WENGI HASA WANAWAKE WANAKWENDA KUROGA ILI KUHARIBU MAFANIKIO YA MWENZIE).

PIA USISAHAU MAJERAHA YA KUTALIKINA/KUACHANA HAYAMTOKI MTU GHAFLA KAMA CHAFYA!, YANACHUKUA MIKA 10-15 KUJA KUISHA. SASA UNAJIKUTA UKO KWENYE MAHUSIANO NA MAJERUHI
HAWA WENYE KUACHANA LEO, KISHA KUJITUTUMUA KUWAONYESHA WATU MAMBO YAKE SAFI SASA BAADA YA KUACHANA, WALE NI WAGONJWA WA NAFSI.NI DHAIFU MOYONI, STRONG MDOMONI.

KAMA ILIVYO KAWAIDA, KWENYE MAHUSIANO YA SIKU ZA MWANZO UNAWEZA SEMA NI MALAIKA, MWANAMKE/MWANAUME MWENYE KUJITAMBUA. MPAKA UNAJISEMEA HIVI KWA NINI WALITENGANA.!
BAADA YA MUDA UTAKUJA KUJUA KWA NINI MWENZAKO ALISHINDWA
 
Habarini nyote,

Maarifa na ufahamu ni kitu cha bure, napenda kuwajuza ya kwamba haifai kuoa mwanamke alieachika au kuachwa kama mume alokuwa nae bado yupo.

Ni nuksi mbaya na ni dhambi ogopa nuksi.

Itoshe kusema hayo chukueni tahadhari.

Yangu ni hayo tu.
Kauli hiyo inaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti na kuna maoni mbalimbali kuhusu suala hilo. Ni muhimu kuelewa kwamba maisha na uhusiano kati ya watu ni ngumu na kila hali inaweza kuwa tofauti. Kila mtu ana historia yake na sababu zake za kuachika au kuachana na mwenzi wake.

Kuoa au kuwa na uhusiano na mtu aliyekuwa ameachika au kuachwa si lazima iwe nuksi au dhambi. Watu wanaweza kubadilika, kujifunza kutokana na makosa yao, na kuanza upya kwa mafanikio. Ni muhimu kutathmini kwa makini uhusiano wako na mtu huyo na kuelewa changamoto na fursa zinazowezekana.

Katika kila uhusiano, umakini, mawasiliano, na heshima ni muhimu. Kuchukua tahadhari na kufahamu historia ya mtu unayetaka kuanzisha uhusiano naye ni jambo la busara. Lakini jumla ni kwamba hakuna sheria ya moja kwa moja juu ya suala hili, na maamuzi ya kibinafsi huchukuliwa kulingana na hali ya mtu binafsi na maadili
 
Sasa hebu kamata biblia yako tuufunge mjadala huu.

Imekatazwa mwanamke kumwacha mumewe. Ila kama ikitokea kamwacha basi asiolewe tena na endapo atamisi mizagamuo, basi apatane na mumewe. Mume nae kakatazwa kumwacha mkewe. Ni AMRI. (1 Wakorintho 7:10-11)

Luka 16:18 (Nitasoma kwa sauti)
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini"

Kwahiyo ukioa mwanamke aliyeachika ni kweli unatenda dhambi (ya uzinzi, kwa muda wote utakao kuwa nae) ila sio kwamba unapata nuksi kama mleta uzi alivyoongeza.

Ikiwa mwanamke ni mjane, unaruhusiwa kumuoa (1 wokorintho 7:8-9).

NB: Mwanamume unaruhusiwa kumwacha mke wako ikiwa tu 'ni mchepukaji'. Ukimwacha kwa kosa jingine lolote tofauti na hilo basi utamfanya mzinzi (Mathayo 5:32).
Kwahyo obviously utashiriki dhambi yake ya uzinzi huko atakako kwenda, kwa maana umemsababishia wewe🙂
 
Hiyo kitu ipo kiimani zaidi na ndio maana wengi wanampinga mleta uzi. Na zipo jamii ambazo kijana wa kiume ambaye hajawahi kuoa,ni jambo la aibu kwake kumuoa mwanamke ambaye kaachika,kazalishwa ,aliyewahi kuishi na mwanamume kinyumba au aliyefiwa na mume. Sio mwiko lakini ni dosari kubwa na reference mbaya kwa kijana huyo hata atakapokuwa mtu mzima. Kwenye jamii ninakotokea mimi huyo kijana hawezi kumuamkia baba,kaka wala mtu mwanamume mzima yeyote kwake kwa salamu ya ukubwa i.e ya kuwa mwanamume as wanamuona kama bado ni mtoto. Vijana mkubali mkatae kuoa single mother ni dosari kubwa sana.
 
Habarini nyote,

Maarifa na ufahamu ni kitu cha bure, napenda kuwajuza ya kwamba haifai kuoa mwanamke alieachika au kuachwa kama mume alokuwa nae bado yupo.

Ni nuksi mbaya na ni dhambi ogopa nuksi.

Itoshe kusema hayo chukueni tahadhari.

Yangu ni hayo tu.
One man down[emoji1][emoji1]
 
Kweli kichwa moto .....watu wanaachwa kila siku na wanaolewa then life Good tu.

Sema hivi mke mwema au mume mwema aliyepangwa na Mungu huwa hawezi kuachika Over
Kwahiyo hapa unakubali kuwa aliyeachika ni katika hao waovu, yaani sio wema kabisa na kama ni hivyo basi hizo nuksi zipo ndani yao sema kwa nje hatuwezi kuziona
 
Katika Imani na Dini gani ni Dhambi?

Askofu, kuhani, na jamii za wachungaji wao ndio hawatakiwi kuoa Mwanamke asiye Bikra, mjane, au aliyetalakiwa.
Lakini Sisi wengine tunaruhusiwa kuoa ikiwa tuu waliachana Kwa Talaka
 
Kwa waislamu ni lazima akuonyeshe barua ya kuachwa yaani talaka.
Kwa Wakristo unakuwa unamzini mke wa mtu.
Laana ya kutembea na mke wa mtu ni kubwa.
 
Katika Imani na Dini gani ni Dhambi?

Askofu, kuhani, na jamii za wachungaji wao ndio hawatakiwi kuoa Mwanamke asiye Bikra, mjane, au aliyetalakiwa.
Lakini Sisi wengine tunaruhusiwa kuoa ikiwa tuu waliachana Kwa Talaka
Kwa waislamu.
Ukristo hakuna kuoa au kuolewa hadi mmoja afe labda, kuingia kwenye ndoa na mtalaka mnafanya uzinzi.
Kidunia ni sawa kuishi na mwenye talaka
 
Tutaaminije kuwa unayosema ni kweli?, humu jamiiforum mtu akikwazana na Malaya wake huko anakuja kusigina mitandaoni

Huna tofauti na Ile mijimama shapeless inavyowazibia riziki wadada wazuri wenye figure zao mjini utaskia wanaume wote ni mbwaaa
🤣🤣 Umeongea point...siku hizi mtu akiachwa tu anakuja kupoison the well humu...hatupi sababu ya msingi eti dhambi na nuksi
 
Hivi kwanini siku zote ndoa ikivunjika basi mwenye shida ni mwanamke? Ina maana wanaume mmeumbiwa ukamilifu?
Wanasema mwanamke mpumbavu na mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ,so mwanamke mwenye akili na mwerevu hatoruhusu ndoa yake ivunjike kwa namna yoyote ile hivyo wanaume hatuhusiki
 
Hivi kwanini siku zote ndoa ikivunjika basi mwenye shida ni mwanamke? Ina maana wanaume mmeumbiwa ukamilifu?
Wanasema mwanamke mpumbavu na mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ,so mwanamke mwenye akili na mwerevu hatoruhusu ndoa yake ivunjike kwa namna yoyote ile hivyo wanaume hatuhusiki
 
Back
Top Bottom