Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Nissan Patrol Y62 V8 , Ya petrol, 2017, ina five years sasa nimenunua mpya Nissan pale 124,700USD, SASA ina kilometa 102345.
Imeshuka thamani nimepewa offer 100M. Tu.
Na hilux 2017 imekost hadi Dar 48,258usd.
Crown imecost 10,9450Usd.

Nauza nissan ni PM njoo ulipe uchukue full documents. Mbadala inakuja Toyota prado 2021 - 87,000usd. Nimenunua via finance.
Na Pick UP Nissan used Td42 36,000usd.
Sasa unashangaa nini ???
Mi mwenyewe na ndoto one year or two nimiliki 300series Dola 167,000.
Kwa sasa siwezi na meengi ya kufanya.
BMWx5 nilinunua 85M Tshs. Ilisumbua sana nikauza baada ya three years 37M.
Eti mimi nadai si dai na kwa umri wangu sikumbuki gari nilizonunua na kuuza.
Sasa najenga zaidi umri umesogea watoto majukumu nikiyamaliza Insha Allah in 2yrs or before my dream car Toyota land Cruiser Vxr 300series ntanunua.
Muda huu uwezo wangu Prado 2021 Diisel Fully loaded.
USIPATE SHIDA MUNGU AKUONDOLEE HUSDA NA MASHAKA.
Nauza hiyo Nissan Y62 Ipo bompa njoo pm
Tufanye biashara ana kwa ana at my office.

Kila lililo jema kwako mkuu
 
Wana Jf salaam,

Ikiwa ni weekend tulivu kabisa.
Kama tujuavyo, kumiliki gari sasa hivi ni miongoni mwa vitu vya muhimu sana.

Wamiliki wapya wanaongezeka kila kukicha, na kwa bahati mbaya wengi hujikuta wanamiliki magari ambayo baadae yanakuja kuwapa changamoto na kujutia kabisa, hiyo inatokea mara nyingi kama kipato cha mmiliki hakiendani na aina ya gari analomiliki.

Leo tuambiane ukweli, pengine kupitia uzi huu utakuwa msaada kwa mtu au watu kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye dunia ya umiliki wa gari.

Ni gari gani ambayo hauwezi kumshauri mtu kununua na ni kwanini?

Probox
 
Naweza kuitambua vipi Nissan trail toleo la kwanza na pili
Njia rahisi kujua ni hii, kizazi cha kwanza dashboard yake speedometer zipo katikati kama ist,vitz na Rumion. Kizazi cha pili speedometer wameirudisha nyuma ya usukani halafu body yake imeshiba shiba. Mimi naipenda hii ya pili kwasababu sizipendi gari zenye speedometer katikati watu wote mnaona nini kinaendelea kwa dereva
 
Mkuu usijidanganye na cc 1490 za subaru ukadhani ziko sawa na za IST.

Cc za gari zinaweza kutumika ku determine power na ulaji mafuta wa gari, ila sio kigezo pekee cha ku determine hizo.

Kuna vitu vingi sana vina determine na inabidi uwe unalijua gari moja moja na mifuno yake ndipo utaweza kujua ipi unakula zaidi.

Factors ni kama hizi
  • type ya engine
  • mwaka wa gari
  • aina ya mafuta inayotumia
  • technology iliotumika

Mfano mdogo tu, kuna gari inaitwa Mazda rx 8, hii gari ina cc1300 tu, ila ndugu ya tu usijidanganye ukaifukuzia ikakukalisha wewe na cc2500 za brevis yako. Na inabugia mafuta kuliko hata toyota za Cc2500. Why? Sababu inatumia rotary engine tofauti na za toyota.

Turudi katika ulinganisho wako, Subaru wanatumia boxer engine, ni powerful na zinabwia mafuta ukilinganisha na cc za engine za toyota.

Yaani ukiweka subaru ya cc1490, 1990 zinabwia wese na powerful zaidi ya toyota za same engine size

Mfano mimi natumia Volkswagen polo ina cc 1380 tu, ila kanakunywa mafuta vizuri na kanakimbia kuliko hata IST ya 1490, na hata baadhi ya magari ya cc2000+ nawakalisha vizuri tu

I hope umenipata hapo
Hizo hesabu zimekaaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana Jf salaam,

Ikiwa ni weekend tulivu kabisa.
Kama tujuavyo, kumiliki gari sasa hivi ni miongoni mwa vitu vya muhimu sana.

Wamiliki wapya wanaongezeka kila kukicha, na kwa bahati mbaya wengi hujikuta wanamiliki magari ambayo baadae yanakuja kuwapa changamoto na kujutia kabisa, hiyo inatokea mara nyingi kama kipato cha mmiliki hakiendani na aina ya gari analomiliki.

Leo tuambiane ukweli, pengine kupitia uzi huu utakuwa msaada kwa mtu au watu kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye dunia ya umiliki wa gari.

Ni gari gani ambayo hauwezi kumshauri mtu kununua na ni kwanini?
1. Range rovers- haya magari si imara na yatakugharimu kiasi kikubwa kutengeneza. Na pia thamani yake inashuka haraka sana pale tu linapoanza kutumika. Mbadala wa hili unaweza kumiliki landcruiser 200series (maararufu kama v8)

2. Mazda rx8- sababu ya kuepuka haya magari ni kwamba; yanatumia mfumo tofauti wa engine hivo basi kuna uhaba wa mafundi wanaoweza kutengeneza. Engine yake haina pistons, haina cylinders, haina valve, zina kula sana mafuta.
Aina ya engine zinazotumia zinaitwa wankel au rotary Wankel engine - Wikipedia

Sasa unaweza ukajiuliza kwanini hizi engine walizitumia? Sababu ni kwamba ni engine ndogo na zinatoa nguvu kubwa kulinganisha na uzito wake (power to weight ratio) ivo ni nzuri na zinafaa zaid kwa magari ya michezo (sports cars)

Screenshot_20220830-105447_Chrome.jpg
 
Kiujumla magari mengi ya ulaya hassa uingereza na ujerumani karibu yoote yanakuwa over Engineared ! Wanazingatia saana usalama na comfort ya gari, vile vile yanakuwa yametembea saana kilometa nyiingi, likiisha warranty wanauza.
Kwa namna hiyo kununua yaliyotumika used, kuwa na changa moto nyiingi saana na kati ya gari kumi saba hazifiki miaka mitatu Bongo, ununue iliyo kuwa bado ina upya itakupa muda kiasi, nimemiliki nyiingi tu kweli likiwa used na model chini ya miaka 13 hazifai. Bora kuanzia 2015 ambazo ni za gjhali saana. Sishauri mtu mwenye kipato chochote kununua gari ya zamani mno za Europe ni pasua kichwa.
Kwa mjapan Nissan nyiingi zinafanana spare parts zake tabu na bei juu mfano. Namiliki Nissan Patrol y62 ya 2017 - gari V8 ina nafasi ina nguvu nilinunua mpya sasa inasoma laki km kwenye Dash board ilipofika kM 92,000 ilisumbua sana senser, ignition coils,plugs,rejeta, fuel pump n.k. nilisimamisha miezi mitatu nakusanya nguvu kuagiza spare na ufundi wa uhakika limegharinu zaidi ya milioni 27. Kwa sasa lipo saafi illa sishauri kuwa mtu awe nalo labda uwe na uwezo wa pesa, natumia kwa safari sasa sana na lipo saafi na lina bugia wese balaa gari ya starehe na nguvu.
Nimenunua gari mbili hilux 2017 used na harrier 2008 used yaani na enjoy hamna shida natumia killa siku na masafa mafupi mambo safi na wife nimemchukukia Crown Athletic 2010 ( alikuwa na Bmw x5 ilitushinda) ana enjoy na kwa sasa hata pesa zinabaki na mjengo wetu unaelekea kwisha bado kidogo.
Nimemiliki namshukuru mungu gari nyiingi aina nyiingi , Gari ni Toyota kwa Africs.
Nissan naitangaza hakuna mteja na mpango wa kuliuza lipo safi sasa hata offer niliyopeea ya Mill 100 bora kuliko likianza matatizo.
Nimeagiza Toyota Prado Diesel litafika mwishoni mwa mwaka kwa njia ya finance la mwaka 2021 ni mara dufu bora.
Kuna jamaa yangu analo la 2016 hadi leo KM 278,780 hamna shida ni Breki na service tu.
Kwa uchache Bongo ni Toyota hata ukiwa na pesa vipi zingine ni majanga tu.
We ni Mhaya?🤣🤣samahani lakini
 
Back
Top Bottom