Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?
Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?
Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?
Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?
Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?
Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?
Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
Mkuu, si halali kwa mujibu wa Wazanzibar lakini ni halali kwa mujibu wa katiba ya mpito ya 1964.
Katiba ya 1964 ilisema mambo yote ya Tanganyika yatakuwa ya muungano
Wazanzibar wanasema mambo ya muungano yalikuwa machache ingawa yameongezwa
Kwa mujibu wa Wazanzibar sehemu zote ulizotaja hapo si za muungano. Hoja yao ni kwamba kwa katiba ya mpito Tanganyika ilivaa koti la Muungano. Kitu cha kushangaza waliojificha ndani ya koti la Muungano ni Wazanzbar ambao hunufaika na mambo yale yale wanayolalamika yameongezwa kama ulivyoyataja
Kuteuliwa, hakuna sheria inayomkataza Mzanzibar asiteuliwe kwasababu nafasi 'X' husema kwa 'Mtanzania'
Hapa Wazanzibar wanavua Uzanzibar wao wanavaa Utanzania. Kwa miaka ya nyuma nafasi fulani za Tanganyika waliteuliwa katika spirit ya muungano lakini hawakupewa uongozi kamili
Kugombea: Again Wazanzibar wanapotaka kugombea wanavua Uzanzibar wao wanavaa Utanzania kwahiyo katiba inaruhusu wateuliwe. Ni kama ilivyo ardhi , elimu ya juu n.k. au usimamizi wa Taasisi za Tanganyika
Kodi: Yes,kuna kodi za muungano zinazopelekwa Zanzibar nje ya ile 4.5% ya pato la Tanganyika.
Tanganyika na Taasisi zake zinatoa ajira nyingi kuliko SMZ, hivyo kupunguza mzigo wa ajira Zanzibar.
Mfano, Zanzibar wanapewa 21% ya ajira za muungano wakiwa watu milioni 1.2 tu.
Ikiwa ajira za muungano ni 100,000 tunaongelea 21,000 mara mbili ya ajira za SMZ takribani 10,000.
Jambo la kushangaza kodi wanazolipa zinapelekwa Zanzibar! Yaani wanapewa ajira za bure za Watanganyika halafu SMZ wanalipwa kwa kupewa ajira hizo na kupunguziwa unemployment!
G55 wakati wa Mwinyi waliona upendeleo na matatizo makubwa. Yamerudi sasa hivi kila kitu Zanzibar hata majaji wa mahakama kuu wanateuliwa kutoka Zanzibar , mawaziri, viongozi wa Taasisi n.k.
Warioba kasema ni mambo 7 tu, mengine kila mtu aangalie utaratibu wake.
Watanganyika endeleeni kutoa hisani! kule Zanzibar Rais Mwinyi kasema ninyi ni sawa na wageni wengine