Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

Kila awamu na marafiki zake...

Awamu ya tano, bega kwa bega na Rwanda...
 
Mutakereka saana,Mama anaupiga mwingi,na siku si nyingi mabomba yetu yatatoa maziwa badala ya maji.
Achieni ngazi Mchuma unaondoka.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Idadi ya watu sidhani kama inaweza kuzuia usiwe chini au tegemezi. Oman wako wachache ila bado tunawategemea kwa baadhi ya vitu. Norway ina watu million 6 ila bado wanatusaidia!!
Yaani wabongo bhana.... mbona kutwa tukiisifia USA, UK na nchi nyingi za Ulaya ambazo zilikuwa ni Wakoloni wetu na hatuoni shida?...
 

Nikusahihishe kidogo. Zanzibar haijawahi kuwa koloni la Oman. Kilichotokea ni Sultan wa Oman Sayyid Said alihamisha makao yake makuu kutoka Oman na kuyaleta Zanzibar mwaka 1840 na alipofariki kwenye miaka ya 1850s Ufalme uligawanywa sehemu mbili yaani Oman na Zanzibar. Kwahiyo dola kongwe ya Zanzibar ilikuwa ni dola huru iliyoenea hadi maziwa makuu ikitambuliwa na mataifa makubwa duniani. Kuiita Znz koloni la Oman ni kuivunjia heshima.
 
Inawezekana anaanda mazingira ya hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa , upinzani ukichukua nchi.
Kwa hiyo upinzani ukichukua nchi priority itakuwa ni visasi badala ya kuwaletea wananchi maendeleo? Kisasi kwa lipi baya walilofanyiwa?
 
Halafu hii kwa mbali inaanza kuleta picha kama Oman ndiyo ilikuwa koloni la Zanzibar kwa sababu Sultani alikuwa anaishi Zanzibar
 
Bora huko mara milionis wananyongwa na kila mmoja anakuwa na ufahamu kama ndugu,rafiki,jamaa amenyongwa ,vipi kwenye nchi watu wanapotea,wanatekwa wanapigwa risasi na watendaji wanaitwa wasiojulikana mpaka imekuwa mazoea . wanaitwa wasiojulikana ili iweje ?
 
Umeongea ukweli mchungu. Tuko busy kuwachukia waarabu wakati wazungu wanafanya kitu kilekile

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Halafu hii kwa mbali inaanza kuleta picha kama Oman ndiyo ilikuwa koloni la Zanzibar kwa sababu Sultani alikuwa anaishi Zanzibar
Zanzibar halikuwa koloni bali ilikuwa ni sehemu ya Ufalme wa Oman toka mwaka 1650 baada ya askari kutoka Oman na wananchi wa Pwani ya Afrika Mashariki kuwafurusha Wareno. Toka hapo Oman ilikuwa na haiba kubwa kwenye maeneo yote ya Pwani ya Afrika Mashariki. Na mwaka 1840 Sultan aliamua kuhamishia makao yake makuu Zanzibar.
 
Huyo mfalme alikuwa anafanya kazi gani km si kutawala?
Huko Zanzibar alitawala kinanguruwe?
 
Dah, mzee unaonekana una ujuaji wa kishamba halafu wa kizamani,unapenda kudakia vitu halafu huna maelezo ya kutosha, kwa kifupi unaendeshwa na mhemko,papara,pupa jumlisha na ushamba, udaku, pamoja na umbeya ndiyo kabisa.
Tangu ulipobadilisha jina la Infantry soldier bado ushamba haujakutoka. Vipi project yako imelipa??
 
Mwinyi kaoa Mwarabu, mwanae Ana mke Mwarabu, karume mke wake mbulushi (wengi wapo Oman) na amemuoa hata kabla ya mapinduzi. Watu wengi influential Bara hili LA Africa wana wake waarabu, juzi tu hapa Alpha Blonde na ubabu wake kaoa Tunisia.

Na Mkuu assume Baba ni Mwarabu na mama Mbantu, mtoto akizaliwa si Ana damu za wote? Ikitokea huyu mtoto kaoa Mwarabu damu ya kibantu haijaoa Mwarabu?

Huko Omani kwa vipindi zaidi ya vitatu watu wenye Asili ya Afrika ni masultan, kuanzia Babu yake Qaboos, baba hadi Qaboos mwenyewe na husikii wa Oman wakilalamika, wameitransform nchi yao toka kuwa Koloni LA Uingereza mpaka Sasa Ina uchumi sawa na Hizo Nchi zaulaya.
 
Oman ina udugu wa damu na Zanzibar (ambayo iko Tanzania) ni zaidi ya hio historia ya ukoloni pekee kwa kulinganisha na uingereza, ujerumani nk. Oman inaposema inataka kusaidia naamini wanalenga haswa kusaidia ndugu zao wa damu.

Maasalaam,
 
Nchi za uarabuni zote sio first world countries ni dependant Kwa mataifa ya magharibi kiuchumi wao..
Aisee.

Nchi za kiarabu hizo zaGulf Zina uchumi wa kujitosheleza, unajua Kampuni moja tu ya Saudia kama Saudi Aramco ina Thamani ya Trilioni 2.4 zakimarekani.

Kwa Hela za madafu dola Trilioni 2.4 ni Budget ya Tanzania miaka zaidi ya 80,

Inachuana na Apple kama kampuni Tajiri duniani then wewe Unasema ni tegemezi?
 
Saud Aramco na Marekeni yumo maana yake ni Saud Arabia and American. Saud arabia wako vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…