Licha ya umasikini wetu wa taifa hapakosekani kundi la watu wenye nafuu, Tukigusia makabila yenye asili ya hapa kwetu, jamaa wapo mbali mno.
Kunaweza kuwa na makabila yanayowafatia ila ni gepu refu mno.
1.Elimu: Hawa watu wamesoma sana na shule zipo huko kwao tangu zamani sana, sehem zao kuna shule nyingi sana, hapa wenzao ni wahaya lakini tatizo wahaya wana shule chache sana huko kwao na sehemu waliyosifika ni kwenye elimu tu.
Biashara - Ni kama kipaji chao cha asili hata kwa ambao wameishia darasa la 7 wapo wanaofanya makubwa, ukija kwa wasomi nako wamejaa wamefungua makampuni, najua kuna wanaofatia wapo wakinga, waha, wasukuma, n.k ila wameachwa mbali sana.
siasa - ukiachana na ccm hawa ndio waasisi wakubwa wa vyama vingi maarufu vya upinzani kuanzia tlp, nccr, chadema, vyote vina asili ya wachaga,
kuendeleza na kujenga kwao hawana mpinzani, nimeona makabila mengine wengine wanajaribu jaribu wanajenga nyumba za kisasa huko vijijini kwao ila unakuta kijiji kizima nyumba hizo zinahesabika,
Kwenye system na political positions hawajajaa sana
ila kila ofisi wamejaa, mashirika ya uma na kimataifa wapo.
kuridhika kwa wachaga ni ngumu sana, mtu alieridhika mara nyingi huonyesha majigambo na sifa, kuna baadhi ya watu wakipata hela basi wataanza laki si pesa, ist gari za watoto, n.k kwa wachaga mtu anaweza kuwa na pesa kibao ila bado ana nidhamu ya pesa laki 1 anaipangia bajeti, ataendesha hata passo ilimradi ajenge kwao nyumba nzuri, n.k.
Ni nadra sana kusikia mambo ya uchawi uchagani kwamba flani kamtupia jini jirani kisa mtoto wake kapata kazi, kurogana kisa ndugu kapiga hatua, n.k. uchawi ni adui mkubwa sana wa maendeleo na kwa kiasi kikubwa wamejitahidi kuukwepa, just imagine nina rafiki yangu wa huko Geita vijijini alitaka kuwajengea wazazi nyumba ya kisasa, watakataa, mwengine rafiki wa Njombe aliniambia huko kijijini kwao hata kuweka bati ni ishu nzito kwasababu majirani wanaweza kuchukia maendeleo wanaroga.
Wanaheshimu mila na desturi zao: kifupi wanajua wapi wametoka na wapi wanaenda, wachaga ikifika december kuna mtu asiejua balaa lao ? huwa ni kama waisrael wa sehem mbali mbali wanarudi kwao, hii pia inafanyika na kabila lililofanikiwa zaidi Nigeria waigbo hurudi kwao kila mwisho wa mwaka.
..........................
Kwa wengi unaweza kukuta kwenye elimu wapo ila kwengine zero
wengine unaweza kuta wanajitahidi biashara ila huko kwao hakutamaniki na elim bado sana
n.k.