Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

KIKI CORAL

Senior Member
Joined
May 10, 2023
Posts
183
Reaction score
313
Duniani Kuna Changamoto sana, kuna wakati unapitia Changamoto kubwa unatamani hata Kuitelekeza Familia.

Kuna wakati nilikuwa Nikiona watu hasa wanaume wametelekeza familia nilikuwa sielewi kabisa ila Ukubwa Huu una mafundisho mengi sana.

Nimekaa nimewaza sana, nimepitia Changamoto nyingi sana Tangu mwezi wa saba Nimeuza baadhi ya Mali zangu hadi sasa Hivi nimesihiwa kabisa ni kama matatizo yanaitana Likiisha hili linafuata Lingine.

Imefika wakati sasa Nikitazama watoto wangu wachanga Roho inaniuma sana maana ninawaza Vitu ambavyo Viko nje kabisa .

Unakopa hadi unaogopa Kukopa au Kuomba tena, unadhalilika.

Umasikini ni Mbaya sana, Umasikini ni fedheha na Aibu Kubwa.



Hivi ni nji gani unayoweza Kuitumia au unaweza kufanya nini unapopitia kwenye Changamoto Kama Hizi.

Ni jambo gani la hekima sana unaloweza kufanya Ili upite salama kwenye Kipindi cha aina Hii.
 
Kukaa kimya bila kutangaza matatizo yako kwa watu,
Ukipata nafasi nenda kakae baharini utazame mawimbi ya bahari kwa afya ya akili yako,
Nilichogundua kwenye maisha kuna vitu lazima upitie hata iweje na unavyojaribu kukwepa ndo inakua mbaya zaidi so just face it,nakuhakikishia hakuna kinachodumu hayo yote yatapita itabaki tu story!
 
Kukaa kimya bila kutangaza matatizo yako kwa watu,
Ukipata nafasi nenda kakae baharini utazame mawimbi ya bahari kwa afya ya akili yako,
Nilichogundua kwenye maisha kuna vitu lazima upitie hata iweje na unavyojaribu kukwepa ndo inakua mbaya zaidi so just face it,nakuhakikishia hakuna kinachodumu hayo yote yatapita itabaki tu story!
Asante.
 
Ukipitia kipindi ambacho juhudi na maarifa ya kibinadamu vimeshindwa mwite Mungu.
Ikiwezekana jifungie mahali umwite Mungu.
Hiyo ndio njia pekee ya kutoka kwenye jambo lililokwama kibinadamu
Wafilipi 4 : 6

Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
For read more download the Bible using this link:
Swahili English Bible - Apps on Google Play
 
Ukipitia kipindi ambacho juhudi na maarifa ya kibinadamu vimeshindwa mwite Mungu.
Ikiwezekana jifungie mahali umwite Mungu.
Hiyo ndio njia pekee ya kutoka kwenye jambo lililokwama kibinadamu
shukran kwa Ushauri. Mungu tunamwita sana Mkuu ila mambo yanazidi kuongezeka kila siku vitu vipya
 
Kwanza kama unamuamini Mungu ni hatua ya kwanza na nzuri sana,naamini kabisa mtu ambaye hamuamini mungu huwa anakata tamaa mapema na kuona hana njia na nuru mbele yake,nimewahi kusikia mmasai anajinyonga kwa sababu mifugo yote imekufa, kwake yeye mifugo ndio mungu wake,kwahiyo hakuna maisha pasina ng'ombe

Ninachotaka kusema ukiamini kuna nguvu ambayo wanasayansi wanaita nature na sisi wengine tunaita Mungu muweza basi kuna faraja kubwa sana unaipata kwa kujua kuna mwenye uwezo wa kumaliza changamoto zangu

Kwenye vitabu vitakatifu Mungu anasema mnadhani mtaingia tu peponi tu kwasababu mmesema mmemuamini Mungu? Hakika mtajaribiwa kwa upungufu wa mali na watu na njaa na hofu,ila wape habari njema wenye kusubiri

kwahiyo ndugu yangu hiyo ni mitihani ambayo walipata hata umma zilizo pita huko,hata manabii na mitume nao walijaribiwa pia,tena wao mitihani yao ilikuwa mizito sana

Hiyo ni sehemu ya maisha ambayo sote hupitia kwa namna tofauti na kwa viwango tofauti,huwa sioni haya kutoa mifano yangu binafsi,kuna kipindi ilibidi familia iende kwao hali ilikuwa mbaya sana, tena ilikuwa kipindi cha ramadhani,futari yangu ni ya kuvizia msikitini tena sahani moja mnakula watu wawili

Ebu fikiria umefunga hlf jioni unakula sahani moja watu wawili na kesho unafunga tena,hapo daku hakuna hakika kilikuwa kipindi kigumu sana,lkn nilimwamini Mungu na hayo yakapita

Kwahiyo kikubwa bro hauko peke yako,ni sehemu ya maisha,muombe sana Mungu na kutaka msaada wake,usione aibu wa haya kuomba msaada katika kipindi hiki kigumu,kukosa sio uzembe wako ila kuna nyakati maisha huwa hivyo

Najua vile unavyohisi najua hata usingizi wako ni shida na huenda ukishtuka usingizini unaweza usilale tena kwani hujui watoto wako watakula nini,nimepitia hayo nayajua vizur sana

Usikate tamaa kamwe na swali sana na kusali hakika yupo ambaye kwa namna na uwezo wake atakutoa katika hiyo changamoto

Asante
 
Vipi kuhusu mkeo ?
mmeungana kwenye haya mapito au nae kakikumbia?
kama mpo pamoja mpaka mida hii na misukosuko yote hiyo mshukuru Mungu sana.

Panga na mkeo Nini mnaweza Fanya,mkeo anaweza anzisha biashara ndogo kama kukaanga maandazi,chapati akazungusha na wewe kuwa tayari kufanya kazi ambazo hukuzizoea jua hiki ni kipindi cha kudharirika uza hata genge Kwa kipindi hiki huku ukiaikilizia issue za maana huku mke nae anapambana mtatoboa kipindi hicho kigumu,maisha ndio yalivyo Yana ups and. downs .
 
Back
Top Bottom