Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Kila jambo lina mwanzo na mwisho kikubwa usiache kusali usiache kupambana kuwa na Imani tu yataisha siku nzuri na zenye furaha zinakuja
Kitu kingine nilicho kigundua baadhi ya magonjwa ikizingatia lishe hutayaona kabisa jitahidi mkeo Apate lishe Bora kadri unavyoweza ili wanao wachanga wawe na afya baadhi ya magonjwa hutayaona
Pole Kwa kupatwa na changamoto hauko peke yako Kila mtu anapata changamoto m/mungu atakuvusha salama
 
sawa sawa. Asante
 
Hakuna Mungu wa kukutatulia matatizo yako.

Chanzo cha matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Na wakutatua matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kumsaidia kiumbe chochote kile kwenye matatizo.
Sawa.
 
Ukishaleta mtoto kwenye hii dunia au kuwa na familia wakati uwezo wako bado ni wa mpeche mpeche, Matatizo na umaskini lazima vikutwange kisawasawa.

Hadi akili ikukae sawa sawa.

Kabla ya kuleta kiumbe kwenye hii dunia hakikisha utaweza kukihudumia mahitaji yake yote pamoja na kujihudumia wewe binafsi.
Ingelikuwa ndio hivyo huku Africa watu wachache wangezaa. Usimkatishe tamaa mwenzio kama huwezi kumtia moyo basi
 
Duniani Kuna Changamoto sana, kuna wakati unapitia Changamoto kubwa unatamani hata Kuitelekeza Familia.

Kuna wakati nilikuwa Nikiona watu hasa wanaume wametelekeza familia nilikuwa sielewi kabisa ila Ukubwa Huu una mafundisho mengi sana.

Nimekaa nimewaza sana, nimepitia Changamoto nyingi sana Tangu mwezi wa saba Nimeuza baadhi ya Mali zangu hadi sasa Hivi nimesihiwa kabisa ni kama matatizo yanaitana Likiisha hili linafuata Lingine.

Imefika wakati sasa Nikitazama watoto wangu wachanga Roho inaniuma sana maana ninawaza Vitu ambavyo Viko nje kabisa .

Unakopa hadi unaogopa Kukopa au Kuomba tena, unadhalilika.

Umasikini ni Mbaya sana, Umasikini ni fedheha na Aibu Kubwa.

Hivi ni nji gani unayoweza Kuitumia au unaweza kufanya nini unapopitia kwenye Changamoto Kama Hizi.

Ni jambo gani la hekima sana unaloweza kufanya Ili upite salama kwenye Kipindi cha aina Hii.
Pole sana mkuu yatapita.

Hapa nilipo natamani nipotee kabisa, nitokomee kusikojulikana nisahau kila kitu nikaanze maisha upya kabisa.
 
Omba Mungu.
Uvumilivu.
Fanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa.
Heshimu Kila unayekutana naye.
 
  • Maisha ni changamoto, na dunia haina huruma na mtu​
  • Hakikisha yeyote anayeishi hapo kwako, kuna sababu ya msingi ya kuwepo; vinginevyo usilee tegemezi asiyezalisha hapo ndani.​
  • kama una watu, buni biashara ndogondogo wazifanye; zingine haziiitaji ata 50,000. i,e watembeze karanga, maandazi, barafu, juisi, kahawa n.k​
 
Kama unaamini kuwa Mungu yupo basi hebu ongeza ibada. Amka usiku mlilie Mungu ataleta wepesi. Mwenyezi Mungu hujibu dua za watu.
Usikate tamaa kwani hata sisi tunapitia misukosuko haupo mwenyewe. Mimi huu mwaka wa pili nipo kwenye mtihani mzito japo to be honest bado ninaweza kuilisha familia lakini kutokana na hali hii kuna watu wamesimama shule sbb nimeshindwa kuwalipia ada.

QURAN 94: 5-6
"Hakika baada ya dhiki huja faraji. Na kwa hakika baada ya dhiki huja faraji."
 
Muhimu kabisa.
 
Tuko pamoja mtaalam. Hatuna Budi kuendeleza mapambano
 
Cheka sana
Kejeli sana
Simulia sana
Ila usiombe yakukute
Ukifikia kipindi hiki kigumu faraja Pekee inatoka kwa mke labda na wazazi pekee
Mimi mke wangu alikua anashangaa kila mvua ikinyesha usiku Mimi ndio wa kwanza kwenda kukinga maji hata iwe saa ngapi mpaka ananiuliza hivi wewe hulali?
Kweli nilikua silali hata ustuke saa tano usiku basi huwezi kupata usingizi mpaka majogoo yanawika.
Hakuna kitu kinatia uchungu kama kuona watoto wako wamelala kitandani lakini baba yao hujawaandalia future yao yoyote
Mtoa post kama mkeo yuko pamoja na wewe kipindi hiki kigumu unachopitia ni ushindi tosha
Mungu akupe subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu unachopitia
 
Back
Top Bottom