Ni jambo gani watu wanalifanya sana lakini wewe huwezi?

Siwezi kunywa maji moja kwa moja yaani ile unaweka glass au chupa mdomoni for a while maji yaishe sijawahi kuweza aisee,.
Na kila mtu ananishangaaga na sijui kwanini siwezi na nyie mnawezaje kwanza huwa naona kama nabanwa pumzi
 
Kukaa bar kunywa pombe huku unaangalia mipira na kukesha mpaka asubuhi. Siwezi hiki kitu japo pombe natumia lakini ikifka saa nne usiku nikiwa nje ya ghetto langu huwa nakuwa sina amani. Bora niagize vitu vyangu nijifungie ndani niwe nashusha mdogo mdogo huku nafanya kazi zangu.
 
Siwezi kunywa maji moja kwa moja yaani ile unaweka glass au chupa mdomoni for a while maji yaishe sijawahi kuweza aisee,.
Na kila mtu ananishangaaga na sijui kwanini siwezi na nyie mnawezaje kwanza huwa naona kama nabanwa pumzi
True True!!
 
Kushabikia mpira wa simba na yanga, inanishangaza kila watu unaokutana nao ni masuala ya simba na yanga tu. Najiuliza hawa watu hawanaga content nyingine? Watu wale wale mada zile zile kila siku.

Mimi siwezi.
Hapo nimo
 
Kuuza nyumba yangu niweke mtaji wote kwenye biashara!
Kuna risk takers nawajuwa na wameweza na sasa wana senti ile mbaya! Nawaonea wivu na kuwa heshimu kwa ujasiri wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…