Ni jambo gani watu wanalifanya sana lakini wewe huwezi?

Ni jambo gani watu wanalifanya sana lakini wewe huwezi?

Hizo ngazi hizo zinazotembea..nimepanda mara mbili tu. Mara ya kwanza nilisema hebu leo niikabili hii hofu yangu na nitoe ushamba, nikapanda karibu nijikojolee nikashuka na ngazi za kawaida.

Mara ya pili nilikuwa na mtoto hajawahi kupanda akataka tupande sikuwa na jinsi nikajikaza hivyo hivyo natetemeka.
Sitarudia tena.
 
Aisee 🤣
 
Kuanza speech kwa kusema "awali ya yote namshukuru Mnyazi Mungu blah blah..."
Hahahaha umenifanya nimecheka, wanakuwaga wanafiki hao hamna mnyazi wanaemshukuru
 
Tuende sawa.
Kuna baadhi ya mambo ni ya kawaida na yanafanyika kila siku lakini wewe huwezi au hujui namna yakufanya...
Mfano mimi;
1. Zile ngazi mwendo(escalators)siwezi kuzitumia, na sizitumii hata iweje...Siwezi.

2. Kula wali /pilau na ndizi mbivu kwa wakati mmoja....Siwezi.

3. Kumsimamisha mwanamke barabarani/kuomba namba, nilishashindwa....

TTuendel
 
Back
Top Bottom