Kwani hujui kama Netanyahu katokea IDF? Tena akiwa ni kamanda? Mwache aendelee kuwatumikia wananchi, walau yeye anajulikana anapoishi. Nasrallah maisha yake yamegeukia kwenye mahandaki kama panya hata hotuba zake anafanya kwa "video", uoga umemjaa kwasavabu anaujua uwezo wa Israel
Yapo mengi ambayo Waarabu wamejifunza katika Vita Vya Siku Sita 1967 na Yom Kippur 1973.
Nimejaaliwa kuiona Bar Lev Line Sinai nikiwa katika boat Suez Canal.
Katika Vita Vya Siku Sita majeshi ya Israel yalifika hadi hapo na ni ukingo linapoanza Jangwa la Sinai.
Israel ilisimama hapo baada ya majeshi ya Waarabu kusalimu amri.
Israel ikajenga ukuta wa mchanga kujikinga na mashambulizi ikiwa Misri itataka kufanya hivyo na pia kuonyesha kuwa ardhi yote nyuma ya Bar Lev Line ni ardhi iliyotekwa iko chini ya himaya ya Israel.
Bar Lev alikuwa kamanda katika jeshi la Israel.
Nimesafiri kwa njia ya barabara ya jangwani kutoka Cairo hadi Alexandria na kwa macho yangu nimeziona kambi za jeshi la Misri ndani ya jangwa hilo.
Swali nililojiuliza ni kuwa vipi jeshi kubwa kama hili litashindwa na kanchi kadogo kama Israel?
Katika Vita Vya Yom Kippur mwaka wa 1973 inasemekana Anwar Sadat Rais wa Misri alimsaliti Hafidh Al Assad wa Syria kwa kusimamisha vikosi vyake visisonge mbele hii ikawa kama kajitoa katika mapambano.
Kisa hiki kakieleza Mohamed Heikal katika kitabu chake, "The Road to Ramadan," na uamuzi huo wa Sadat ndiyo uliofanya apitishiwe hukumu ya kuuawa na askari wake mwenyewe.
Vinginevyo kama Misri ingebaki vitani matokeo ya vita vya 1973 yangekuwa mengine.
Vita hii ya 1973 kilichojitokeza ni kuwa majeshi ya Israel yanashindika.
Hassan Nasrala aliingia katika vita vile vya 2006 akijua kuwa IDF hawawezi kuhimili kwanza vita vya muda mrefu na pili askari wake wanakiogopa kifo.
Askari wa Hizbullah wanaingia vitani kwenda kufa si kurejea majumbani kwao wakiwa wazima.
Taarifa za kiintelijensia baada ya vita vile zimeeleza mengi na kubwa na hili lilishuhudiwa na ulimwengu ni baada ya kusimamisha mapigano askari wa Israel walikuwa katika "retreat," wakirudi kwao wameinamisha vichwa vyao chini.
Hawakurejea Israel kwa shangwe kama ilivyozoeleka.
Na pigo kubwa lilikuwa siku ya kubadilishana mateka Israel ikipokea majeneza ya askari wao waliouawa.
Kibri cha Wayahudi kimepunguzwa pakubwa na Hizbullah kutokana na vita vile vya 2006.
Yapo mengi sana katika historia yamapambano ya Hizbullah na Israel kwani ni wao ndiyo waliowatoa Lebanon waliyokuwa wameikalia pasi na haki.