Ni jinsi gani Hezbollah iliweza kushinda vita dhidi ya Israel? (2006)

Ni jinsi gani Hezbollah iliweza kushinda vita dhidi ya Israel? (2006)

Mbna 2006 alirusha bila UN mngekiona chamoto zaidi yapale.
Hiyo UN nani aliwalazimisha kusaini, mgegoma. Mkataba walisaini wote afu unasema bila UN kuingilia Israel angeona cha moto, kwanini Hezb isingeukataa.

Chukua hiyo [emoji652]
images%20-%202020-06-07T110011.265.jpg
 
Upuuzi mtu.. hakuna vita ambayo israel imewahi kushinda.

Vita 2006 ilikua ni stargically kuua uchumi wa lebanon ambapo hadi leo lebanon haijaamka bado inajijenga.. na ndio sababu hezbollah hadi leo hawadhubutu kuanzisha vita na israel pamoja na mauaji ya viongozi wao yanayo fanywa na israel.

Hii ni vita iliyojulikana kama July War au 2006 Lebanon war unakuwa hujakosea kabisa, vita hii ilichukua takribani siku 34 tu, ni muda mchache tu, lakini kuna mengi ya kufahamu juu ya hii vita, naomba uketi usome kwa makini mwanzo mwisho.

CHANZO CHA VITA
Israel ilikuwa na wafungwa(Lebanese Prisoners) akiwemo Samir Al-Quntar na ndugu zake, Hezbollhah walikuwa wanahitaji wafungwa hao waachiliwe ki diplomasia na wapelekwe Lebanon, Israel ilikataa kata kata.

Lebanon ilishavunja sheria mara 100 katika kuvuka blue line kati ya mwaka 2000-2006 ni katika wakati huo huo Israel alivunja sheria mara 11,782 katika anga,maji na ardhini kwa kuvuka blue line.

Blue Line
ni alama ya mpaka kati ya Lebanon na Israeli iliyowekwa na Umoja wa Mataifa mnamo 7 Juni 2000 kwa madhumuni ya kuamua ikiwa Israeli imejiondoa kabisa kutoka Lebanon.

Ni jinsi gani sasa Hezbollah watafanikisha kuwapata wafungwa wao? Njia ilikuwa ni moja tu, kuwakamata askari wa Israel(IDF), ndipo ikaandaliwa operation iliyojulikana kwa jina la Operation truthful promise, nia ikiwa ni kukamata askari wa IDF ili waje wabadilishane na wafungwa wa Lebanese waliokuwa wanashikiliwa na Israel hapo baadae.

Operation Truthful promise au Hezbollah cross border raid kwa jina lingine, ndipo ilipofanyika mnamo tarehe 12 July 2006.
Shambulizi hili ni pale Hezbollah waliporusha maroketi katika sehemu mbali mbali ndani ya Israel wakitumia rockets zijulikanazo kama Kayusha, walivuka Blue Line na kuingia Israel wakipiga ambush Humvee za IDF mbili zilizokuwa mpakani kabisa mwa Israel karibu na uzio na kuzilipua kwa Anti Tank Guided Missile(ATGM), hii ilipelekea askari wawili(2) wa IDF kutekwa nyara, watatu(3) waliuawa pale pale, Pia katika jaribio lililofeli la askari wa Israel kwenda kuwaokoa wenzao, askari watano(5) waliuawa katika jaribio hilo la uokoaji nchini Lebanon.

Hezbollah ilidai wafungwa wake waachiliwe kwa kubadilishana na wafungwa wa IDF ambao walikuwa ni mateka nchini Lebanon, Israel wakajibu hapana haiwezekani kwa wakati huo prime minister wa Israel alikuwa Ehud Olmert.

Baada ya Israel kukataa ilikuwa wazi vita inakwenda kutokea.
Ndipo waziri mkuu wa Israel akasema "Lebanon italipa kwa kitu walichofanya" na pia bwa Ehud Olmert alisisitiza "Lebanon itegemee maumiu makali sana na tutafika mbali zaidi"

View attachment 1469714

Naam yalikuwa ni maneno ya bwana Ehud Olmert waziri mkuu wa Israel, hakika Hezbollah alikuwa amegusa pabaya, sasa kinachokwenda kutokea unakijua, unajua Israel ilishapigana vita ya siku 6 na na kuwa mshindi dhidi ya Egypt,Syria na Jordan? na sasa wanakwenda kukabiliana na Hezbollah kikundi kidogo cha wanamgambo? keti hapo hapo uendelee kusoma.

Ni katika siku hio hio (12 Julai 2006), Baraza la Mawaziri liliamua kumpa mamlaka Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi na manaibu wao kutekeleza mpango mzima waliokuwa wamepanga dhidi ya kuishambulia vibaya Lebanon, Waziri mkuu akasema katika shambulio hilo inabidi wasishambulie makazi ya watu, Kamanda wa jeshi la anga Israel Dan Halutz alisema "Ikiwa askari wa Israel hawatorudishwa, tutarudisha saa ya Lebanon miaka 20 nyuma"

Pia mkuu wa jeshi la Israel upande wa kaskazini alisema "Hii ni vita kati ya Israel na Lebanon, sasa tushambulie wapi? kama wapo Lebanon, tutapiga Lebanon haijalishi wapo sehemu gani, iwe kusini au Hezbollah walipo."

Pia Serikali za AMerika, Uingereza, Ujerumani, Australia, na Canada zilidai ni haki ya Israeli kujilinda. Serikali ya Amerika ilijibu zaidi kwa kuidhinisha ombi la Israeli la kupatiwa Guided Missiles zenye accuracy ya hali ya juu.

Upande wa Hezbollah sasa kiongozi wao bwana Hassan Nasrallah alisema "Israeli wamevunja mpango wa zamani wa kuwaachilia wafungwa hawa, na kwa kuwa diplomasia imeshindwa, vurugu ndio chaguo pekee lililobaki". Nasrallah alitangaza kwamba "hakuna operesheni ya kijeshi itakayoweza kuwaokoa wafungwa hawa ... Njia pekee, kama nilivyoonyesha, ni ile ya mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja na kubadilishana wafungwa".

View attachment 1469718

VITA INAANZA
Na vita ikatangazwa rasmi, ni tarehe 12 julai 2006, Wakati wa siku ya kwanza ya Vita, Jeshi la Anga la Israeli, jeshi la maji walifanya mashambulio zaidi ya 100 dhidi ya kambi za Hezbollah kusini mwa Lebanon, kati yao makao makuu ya mkoa huko Ya'tar. Madaraja matano ya kupita kwenye mito ya Litani na Zahrani pia yakaharibiwa, iliripotiwa kumzuia Hezbollah kuhamisha askari waliotekwa nyara.

Naam hakika Israel ilishambulia kwa nguvu haswa toka angani na ardhini, ilikuwa si mchezo.

Mashambulio kutoka ardhini, baharini na angani yaliendelea katika siku inayofuatia. Miongoni mwa sehemu zilizopigwa yalikuwa makao makuu ya Hezbollah katika vitongoji vya kusini vya Beirut na vile vile ofisi na nyumba za uongozi, kituo cha Televisheni cha al-Manar na kituo cha redio cha al-Nour, runways na depo za mafuta za Uwanja wa ndege wa kimataifa Rafic Hariri Beirut. Vile vile vilivyolengwa ni kambi za Hezbollah, depo na madaraja, barabara na vituo vya petroli kusini mwa Lebanon. Raia 44 waliuawa kwa siku hio. sio mchezo.

Israel hakuishia hapo, Jeshi la Anga la Israeli katika usiku wa manane, 13 Julai, lilishambulia na kuharibu roketi launchers 59 ambazo zilikuwa ni medium range ziitwazo Fajr zilizowekwa kusini mwa Lebanon. Operesheni inadaiwa ilichukua tu dakika 34 kutekeleza lakini ilikuwa matokeo ya miaka sita ya kukusanya akili na kupanga. Kati ya nusu na theluthi mbili ya uwezo wa roketi wa Hezbollah wa wastani IDF ilidai kuwa umefutwa. Kulingana na waandishi wa habari wa Israel Amos Harel na Avi Issacharoff operesheni hiyo ilikuwa "hatua ya kijeshi ya kuvutia zaidi ya Israeli" na "pigo kubwa kwa Hezbollah". Katika siku iliyofuatia IAF ilishambulia na kuharibu sehemu kubwa ya makombora marefu ya Hezbollah Zelzal-2.

"Makombora yote ya masafa marefu yameharibiwa,"Kamanda Halutz alisema na pia aliiambia serikali ya Israeli, "tumeshinda vita."

Ni katika siku za mwanzoni kabisa jeshi la Israel walisema wamemaliza kambi zote za Hezbollah kwa mashambulizi na wamepiga launchers za Kayusha rockets, walisema Hezbollah sio kitu na vita inaisha mapema kabisa.

Kufikia siku ya nne ya vita IDF ilikuwa haioni pa kupiga kwani targets zote 83 kwenye orodha zilikuwa zimeshapigwa.
Sehemu kubwa za miundombinu ya raia ya Lebanon ziliharibiwa, pamoja na barabara urefu wa kilomita 640, madaraja 73, na sehemu nyingine kama vile uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut Rafic Hariri, bandari, vyanzo na vituo vya matibabu ya maji taka, vyanzo vya umeme, vituo vya mafuta 25, sehemu 900 za kibiashara, shule 350 na hospitali mbili, nyumba 15,000 ziliharibiwa vibaya na Nyumba zaidi ya 130,000 ziliharibiwa kiasi.

Hezbollah inajibu.
Kituo cha Televisheni cha Hezbollah al-Manar kilionya jamii za Kiarabu na Kiebrania juu ya shambulio la roketi baadaye. Vile vile Hezbollah ilituma ujumbe wa maandishi kuonya wakaazi wa Israeli waondoke katika nyumba zao ili wasipatwe na shambulio roketi.

Hakika vita imesimama sasa, sasa ni kupiga nikupige.
Tofauti na Israel ilipodhani kuimaliza Hezbollah, kumbe ndio kwanza kama ni movie ya Titanic bado watu walikuwa hawajaingia hata melini kuanza safari. tuendelee.........

Kikosi cha roketi cha Hezbollah kilirusha kati ya makombora 3,970 na 4,228 kwa kiwango cha zaidi ya makombora 100 kwa siku, kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu Vita vya Iran na Iraqi. Karibu 95% ya hayo yalikuwa ni makombora ya 122mm( Katyusha) kombora hizo zilikuwa zina vichwa vya kilo 30, na zilikuwa zinasafiri hadi km 30 . Takriban 23% ya makombora haya yaligonga miji na maeneo yaliyojengwa kaskazini mwa Israeli, wakati mabaki yaligonga maeneo ya wazi.

Miji iliyopigwa ilikuwa Haifa, Hadera, Nazareti, Tiberia, Nahariya, Safi, Shaghur, Afula, Kiryat Shmona, Beit She'an, Karmiel, Acre, na Ma'alot-Tarshiha, na miji kadhaa, kibbutzim, moshavim, na Vijiji vya Druze na Benki ya kaskazini magharibi pia ilipigwa.

Labda niweke mambo sawa hizi rockets za Katyusha katika mapigano ya nyuma zilitumika sana, hivyo hata kipindi IDF inakwenda kumtandika Hezbollah waliona hizo kombora sio kitu na walijua ndio kitu Hezbollah ndicho walichokuwa wakitegemea zaidi, kumbe haikuwa hivyo.

Hezbollah toka mara ya kwanza kwenye ile mission yao Operation truthful promise walianza kurusha hizo Katyusha ambapo hazikuua raia yeyote yule Israel, roketi hizi zilikuwa ni za ki zamani hivyo Hezbollah walizitumia kuwa pumbaza Israel na Israel wakapumbazika kweli.
Japo Mashambulio ya roketi ya Hezbollah pia yalilenga na kufanikiwa kupiga kambi za jeshi nchini Israeli.hata hivyo uongozi wa jeshi la Israel ulikuwa mkali sana na marufuku kabisa kwa vyombo vya habari vya Israeli kuripoti matukio kama haya. Agizo la wakati wa vita kwa vyombo vya habari lilisema kwamba "Uongozi wa Jeshi hatakubali ripoti za Hezbollah kupiga makombora katika kambi za IDF na au vifaa vya jeshi."

Naam kwa kutumia mbinu mpya na mikakati, silaha mpya na advanced kabisa, Hezbollah ndipo ilipogeuza mchezo mzima juu chini na chini juu. Ni vita ambayo Hezbollah waliita "surprises".
Ndipo Hassan Nasrallah akasema "ile surprise ambayo tumeahidi ndio inaanza"

Surprise ya kwanza kutoka Hezbollah.

Kuna meli(Warship) moja ya ya Israel ambayo ni very powerful according to IDF, ilijulikana kama Hanit, nadhani unaelewa unaposikia warship, ni meli ya kivita na ina uwezo mkubwa wa kuzuia missiles na kushambulia.Ni moja ya meli iliyotumika pia kushambulia, kumbuka Israel ilishambulia toka angani, majini na ardhini, na silaha ilikuwa ikiogopeka majini ilikuwa ni hii Hanit warship.

Hanit ilipigwa kombora linalofahamika kwa jina la C-802 lililo tengenezwa China na kuwa modified na Iran, range yake ni km 120, mpaka hapo Israel ilifahamu fika kwamba sasa meli zake hazina maana tena mbele ya Hezbollah pia Israel ilifahamu fika sasa ndio imeanza kuona vita halisi.

Katika shambulio hilo askari wanne waliuawa waliokuwa katika meli hio Staff Sergeant Tal Amgar, Corporal Shai Atas, Sergeant Yaniv Hershkovitz, na First Sergeant Dov Steinshuss.

2_wa.jpg

1_wa.jpg

3_wa.jpg

Surprise ya pili.
Wakati huu Hezbolla walipanga mashambulizi dhidi ya mji wa Haifa, Israel ikiwa inategemea Hezbolla bado atakuwa anatumia Katyusha misssiles, kumbe haikuwa hivyo, na hapo ndipo surprise ya pili ikatokea, ulikuwa ni wakati Israel kukutana na surprise ya pili.

Ndipo kombora aina Zelzal-2 na aina ntingine za kombora toka Iran zikaanza kumiminika kwa wingi ndani ya Israel, kombora hizi zilikuwa zinafika sehemu yeyote Israel na pia zilikuwa zinabeba warhead yenye mlipuko wa hali ya juu takribani kilo 600.
Ndivyo vita ilivyoendelea

Haifa ni mji muhimu sana katika uchumi wa taifa la Israel, na sasa Israel ilibidi iseme kwa kitu walichofanya Hezbollah juu ya kushambulia haifa hakika ni strategy ya hatari sana waliotumia tokana na makazi ya watu, lakini Israel pia ilipiga makazi ya watu.

Hezbollah ikiwa inalenga sehemu muhimu na za ki uchumi vita iliendelea, Israel alikuwa akipiga kofi Hezbollah anarudisha vile vile na vita ikaendelea

Haifa hakika ilishambuliwa, power plant,barabara, majengo, hata magari yalikuwa yanawaka moto tu , raia walikufa wengi, kambi za jeshi zilipigwa.

Haifa ikawa target ya Hezbollah, Israel ikaona hali ni mbaya, kwa sababu walichokuwa wakifanya Hezbollah ilikuwa ni kulipiza kama Israel inavyopiga makazi ya Lebanon na wao wanapiga Haifa city.

Ni wakati huo Israel ikaona Hezbollah hataki mchezo na hapo Israel akaogopa kuipiga Beirut kwa kujua kwamba Tel-Aviv ingepata mvua ya makombora, na utakuwa mwanzo wa kuipoteza Tel-Aviv.

Hakuna asiyejua kwamba USA na Israel hawawezi kabisa kuwa na diplomasia na kundi kama Hezbollah pia wanajulikana kwa uvunjifu wa amani na kukiuka haki za binadamu hasa kwa nchi zetu tusiojiweza.

Kwa maana diplomasia ilifeli mwanzoni hivyo njia pekee ili uweze kusikilizana nao ni kutumia nguvu, naam Haifa iliendelea kumiminiwa missiles.

Mnamo Julai 16, wafanyakazi wanane wa Reli ya Israeli waliuawa kwa kupigwa na roketi kwenye kituo cha treni. Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alisema hapo awali Hezbollah ilikuwa inalenga makombora yake kwenye "vituo vya kijeshi tu". Lakini kwa kuwa Israeli, alisema, amepiga raia basi Hezbollah hakuwa na chaguo ila kujibu kwa kulenga miji ya Israeli.

F060813ff02-640x400.jpg

Haifa.

13assess600.jpg

Haifa Israel.
Hezbollah ikawa inajikadiria tu irushe missile ngapi kama Israel akiwashambulia. Umoja wa mataifa ukaanza kufanya mazungumo juu ya kukatishwa vita hivyo, wakati mwanzoni wali support, so Israel ana hali mbaya, lakini UN haikufanikisha hilo jambo mara moja,

Surprise ya tatu.
Kuna Tanks zilikuwa zinajulikana kama merkava tanks za 4th generation, hakika zilisifiwa kwa nguvu, uwezo wa kupambana, maneuvers, pia timu za waliokuwa waki operate hizi tanks walijulikana kama the best ones katika mafunzo duniani.

Pia zilisifika kuwa ni hatari zaidi duniani na very powerful, kwa uwezo wake mkubwa wa hizi tanks katika mapambano au aina yeyote ya battle field IDF waliikubali sana Merkava.

Licha ya sifa zote hizo ilizonazo Hezbollah iliweza kujua weakness zake na kuweza kuwashangaza IDF, yeah ni surprise nyingine, pia walikuwa wana silaha kwa ajili ya kuhakikisha Merkava ina baki chuma chakavu.

Ilikuwa ni Anti Tank Missile toka Russia na hapo kulikuwa na Milan pamoja na Kornet, vitu ambavyo IDF waliona sasa maji yamezidi unga, katika shambulio baya kutokea ni baada ya Hezbollah kuipiga tank huko Hujeir, hakika hakuna aliyepona, crew nzima waliisha pale pale.

Pia Abram Tank ya USA ilipigwa pia.
Kama tanks za kawaida kama Merkava za mwanzoni almost zaidi ya 50 ziliharibiwa.
Pia katika missiles hizo walikuta missile za Iranian Made.

Kama kawaida vita ya ana kwa ana ilikuwepo(ardhini)/(ground war).

Kwa kutumia jeshi dogo lililoiva kisawa sawa, Hezbollah hakika hawa askari wake wa ardhini walikuwa highly trained(mafunzo ya hali ya juu), pia walikuwa na vifaa vyote vya kisasa kama jeshi la Israel kama vile night goggles,vifaa vya mawasiliano na pia wakati mwingine walionekana wakiwa na uniforms kama za IDF, na vifaa vya kivita vya kisasa kabisa.

Askari mmoja wa Israeli ambaye alishiriki katika vita hio alisema kuwa "wapiganaji wa Hezbollah huwezi kuwafananisha na Hamas au Wapalestina, wameiva na wana mafunzo ya hali ya juu. Hakika sote tulishangazwa".

Harakati za kusimamisha vita
Wakati jeshi la IDF likiwa linakumbana na mbinu mpya za kijeshi pia kichapo kikali, UN wakaona ni wakati wa kusimamisha vita kwani Israel wapo vibaya mpaka hapo, na jeshi la Hezbillah morali ya vita ndio kwanza kama wanaanza, hakika ipo wazi ni katika wakati huu, IDF mashambulizi yao ni ya kusua sua kwa sababu zifuatazo.

1-Wanaogopa kuendelea kupiga miji kama Beirut kwa sababu Hezbollah tayari wana missiles za kufika Tel-Aviv hivyo wangejibu , hivyo vita inge changamka.

2-Israel walishambulia targets zaidi ya 100 za Hezbollah, lakini kinyume na walivyotegemea hakika jeshi la Hezbollah lilikuwa na nguvu bado na mirindimo iliendelea, ipo wazi niliandika ilifikia kipindi Israel wakaanza kukuna vichwa ni wapi wapige tena.

3-Israel walikuwa wameshambulia kwa nguvu sana mwanzoni, hivyo ni katika wakati huu silaha zao zilitumika nyingi sana na nyingine ziliharibiwa,hivyo kulikuwa na upungufu wa silaha tofauti na mwanzoni,ukizingatia kuna kambi zilipigwa na wanajaeshi wa IDF kuuliwa, vifaa vya vita kama ile meli ya Hanit iliyopigwa, kwani tokea baharini walirusha shells 2500 kuelekea Lebanon.

Mazungumzo ya kusimamisha vita hayakufanyika kwa mara moja, yaliendelea kwa wiki kadhaa kwa pande mbili kushindwa kuelewana,UN ikiwa mpatanishi , kutokuelewana huko ni pamoja na Lebanon kusema vita isimame pasipo masharti yeyote wakati huo Israel iliomba kuwe na masharti kuhusu kuachiliwa kwa IDF soldiers wawili.

Hata hivyo harakati za kusimamisha vita zikiongozwa na UK na US zilicheleweshwa makusudi wakijua labda Hezbollah inaweza kuwa defeated, lakini haikuwa hivyo, na ipo wazi vita ilisimamishwa kwa kuwa walijua Hezbollah kuwa defeated ni ngumu sasa na matokeo yatakuwa mabaya.

Ni julai 25 bibi Condoleeza Rice alikutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert katika harakati za kuzuia vita alisikika akisema "Tunaposhughulika na hali za sasa, tunahitaji kila wakati kujitambua na kuangalia ni aina gani ya Mashariki ya Kati tunajaribu kujenga. Ni wakati wa Mashariki ya Kati mpya"

english_mediacenter_events_publishingimages_7de0dc36e168457796a28ac4d0acce26condbig2.jpg

Yalikuwa ni maneno ya busara toka kwa Secretary of state of US bi Condoleeza Rice baada ya kichapo heavy toka kwa Hezbollah pia waziri Olmert aliongelea wakati mgumu wanaokutana nao alisikika akizungumzia jinsi vita ilivyo waweka wanachi wa Israel zaidi ya 1.5 million katika hali mbaya, kazi zikiwa zimesimama hivyo ni jukumu lao kuwasaidia.

Katika hotuba hio waziri Olmert alizungumza wazi kwamba walikuwa wanahitaji suluhisho kusimamisha vita, Hakika kipigo heavy kiliwafanya Israel wafuate matakwa ya Hezbollah bila wao kupenda.

Baada ya pande mbili zote kuridhiana na Israel kuomba wanajeshi wake waachiliwe, Israel na Hezbiollah walisimamisha vita kwa usimamizi wa UN(US), ilikuwa ni saa 2 asubuhi ya 14 august 2006 vita ilisimama rasmi huku Hezbollah ikiwa imefanikiwa pakubwa kwa jambo walilokuwa wanahitaji, wafungwa wa Hezbollah akiwemo bwana Samir Al-Quntar kuachiwa na ndugu zake, vile vile Israel walikabidhiwa askari wao na vita ikawa imesimama.

Hakika hakuna aliyeamini kama Hezbollah angefanya jambo hilo, inasemekana kwamba licha ya Israel kupiga kituo cha television cha Lebanon kwa jina la Al-Manar ilichukua dakika mbili tu wakarudi hewani.

Wakati wa vita Jeshi la Anga la Israeli ilifanya combat missions 11,897, ambapo ilikuwa zaidi ya idadi ya ya Vita vya Oktoba 1973 (11,223) na mara mbili katika Vita vya Kwanza vya Lebanon (6,052).

Wanajeshi wa Israeli walirusha makombora 170,000, zaidi ya mara mbili ya idadi katika Vita vya Oktoba 1973. Afisa mwandamizi katika IDF Armored Corps aliiambia gazeti la Haaretz kwamba atashangaa ikiwa ikitokea kwamba hata wapiganaji watano wa Hezbollah wameuawa na mikombora 170,000.

Kulingana na matokeo ya upelelezi wa kijeshi wa baada ya vita uchunguzi wa kambi ya IDF ulifanikiwa kuharibu Katyusha rockets 100 kati ya 12,000. Tofauti na jeshi la Israel walivyodhani.

Maafisa wa Amerika walidai kwamba Waisraeli hawakufanikiwa katika ufanisi wa vita vya anga dhidi ya Hezbollah na walionyesha kutofaulu kupiga kwa kiongozi yeyote wa Hezbollah licha ya kuteremsha tani 23 za mabomu kwenye makao yake makuu.

Kulingana na mchambuzi wa kijeshi William Arkin alisema kuna ushahidi mdogo kwamba Jeshi la Anga la Israeli lilifanikikwa kidogo sana katika madai ya kuangamiza roketi za masafa marefu na mafupi katika siku za kwanza za vita. Alitupilia mbali madai yote kama "upuuzi" na "hadithi".

Katika kumbukumbu ya miaka sita ya vita vya Lebanon Hezbollah mwenyekiti Hassan Nasrallah alidai kuwa Hezbollah alijua kuwa Waisraeli walikuwa wakikusanya taarifa za kiintelejensia dhidi ya makombora yao yalipo na walifanikiwa kuyahamisha bila kugunduliwa. Maeneo mengi yaliyoshambuliwa na jeshi la anga la Israeli kwa hivyo yalikuwa tupu.

Hata hivyo Israel walidai katika vita hivyo Iran ilihusika kutoa msaada wa vifaa mbali mbali pia Gazeti la Israel la Haaretz lilielezea Hezbollah kuwa ilifundishwa, pia walikuwa na ujuzi,walijipanga vizuri, na pia silaha za kisasa kutoka majeshi ya Syria, Iran, Russia, na China.

Hassan Nasrallah alishawahi kusikika akisema kuwa wana makombora ya kuirudisha Israel nyuma kwenye zama za mawe.

Naama na hapo ndio mwisho wa vita hii ambayo askari 121 wa IDF waliuawa, helicopters ziliharibiwa, meli, vifaru nauharibifu mkubwa wa miundo mbinu.

Pia jeshi la Hezbollah walipoteza askari wao 250.

Hakika kikundi kidogo kabisa cha jeshi la Hezbollah kiliweza kuihangaisha nchi ya Israel na kuishinda katika vita Israel, mpaka Israel kuona vita imekuwa chungu licha ya kutumia uwezo wake,intelejensia, pia kutumia jeshi la anga, ardhi na maji kuipiga Hezbollah, je swali langu.

Israel itaweza ku defeat Iran ambapo ndio walioipatia Hezbollah mafunzo ya kijeshi,silaha na mbinu? kila siku naona watu wana linganisha Iran na Israel.

khamsrallamani-e1569711056798.jpg

Khamenei,Nasrallah kiongozi wa Hezbollah na Qasim Suleimani (enzi za uhai wake).

MWISHO
 
Upuuzi mtu.. hakuna vita ambayo israel imewahi kushinda.

Vita 2006 ilikua ni stargically kuua uchumi wa lebanon ambapo hadi leo lebanon haijaamka bado inajijenga.. na ndio sababu hezbollah hadi leo hawadhubutu kuanzisha vita na israel pamoja na mauaji ya viongozi wao yanayo fanywa na israel.
Si kweli, soma chanzo cha vita mbona uzi nimeweka hapo.
 
Hehehehe

Kama unajidanganya kama kunasiku ISRAEL walilala ama walijisahau katika suala zima lakulinda usalama wataifa lao pole saba MKUU tena sana

Israel hajawahi kujisahau katika suala hili nasidhanii kama itatokea siku atajisahau

Kama walitokea kuzidiwa kwenye intelijensia nawanamgambo halafu mnawapa sifa mnazo wapa pia poleni sana

Kilamuda najaribu kuwapa jambo ambalo lipo wazi kwanini ISRAEL kapigwa nakwanini wanamgambo wameshinda

Achana na yom kapur tunaongelea 2006

ISRAEL waliwapelekea hasara hizbullah sana ila hizbullah walifikia malengo yao kamili sababu walikua wanataka wakamate wanajeshi wa ISRAEL nawalifanikiwa nawakataka wabadilishane wafungwa pia wakafanikiwa

Utasemaje hajapigwa nawanamgambo ?!

Jamaa walutumia ndege wakatumia meli wakatumia vifaru wakatumia kila kitu walibakisha atomic tu

Najamaa walivyoona hali si haki wakajiuzulu nakufukuzana kazi kwa aibu nahasara walozipata [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
ni kweli israel hajawahi kujisahau kwenye suala la intelijinsia na ndio maana nikasema israel anasurvive pale mashariki ya kati sababu ya nguvu yake ya intelijinsia kwani ndio inaplay part kubwa sana kuliko hata nguvu yake ya kijeshi.

pili suala la kutojua intelijinsia yote ya hezbola hilo ni suala ambalo linaweza kuwepo kwani kuzidiana uwanjani hua kunakuwepo hata timu mbili zinapokua zinacheza hua zinazidiana ufundi na ndio maana zote zinaweza kufungana magoli sema hua kunakua na mshindi wa jumla anayechukua point, mfano timu inaweza fungwa goli tatu kwa moja haimaanishi ile iloyofungwa haijawa na ufundi kushindwa ile ingine lazima nayo ilikua na ufundi wake wa ziada na ndio maana iliweza kufunga lile goli moja.

tatu hezbolah sio wanamgambo kama unavyotudanganya yule ni muiran kamili aliyepo lebanon sasa ili ujue kwamba israel amemzidi akili muiran baada ya perfomance aliyoionesha kwenye vita hiyo ndo akatengeneza proxy kule syria kwa hyo iran na hezbolah nguvu yao ya kupigana wakaihamishia syria na sio israel tena. narudia tena hapo mwenye akili nani?

syria ndio ilikua kiungo ama daraja kwa iran kuweka infuence yake lebanin, kwa hyo israel akaja na strategy ya kuvunja vunja daraja, ambalo ni syria, sasa hivi syria kabaki magofu tupu mpaka pesa anatengenezewa na urusi. myahudi sio kama unavyomfikiria wewe. jamaa pale middle east huwezi kuwafanya chochote
 
pia nikusahihishe hapo lengo la hezbolah na iran ni kuifuta israel hapo middle east na sio kuachiwa kwa mateka wao, mbona israel anao mateka wengi tu na bado anawashikilia na hezbolah wengine amewafanyia assasination? kwa nini hezbolah basi hawajaanzisha vita ingine ya kulipiza kisasi baada ya kuuliwa kwa yule mughnyeh na mtoto wake? unaambiwa yule chief commander alikua ni very bright so ilikua ni pigo sana kwa hezbolah, na nafasi yake mpaka tunavyoongea hapa haijapatikana, kwenye ile nafasi nasrala kaweka watu watatu kuziba pengo la mtu mmoja, so kama sababu ya hezbolah kuanzisha vita ilikua ni mateka basi alivyouliwa jamaa walitakiwa kuanzisha vita inginee kali zaidi.kwa hyo hapo hezbolah kwa israel bado sana...
 
Mkuu vita chanzo chake ni Hezbollah kutaka wafungwa wake wa kilebanon.
Israel ikakataa.
Hezbollah wakateka askari wawili wa IDF.
Israel akaonya askari waachiwe kabla haja toa kichapo kikali.
Hezbollah wakasema tunachotaka ni wafungwa.
Israel ikaingia vitani, siku ya nne wakasema wameimaliza Hezbollah.

Kumbe Hezbollah ilihamisha silaha na kila kitu, Israel ilikuwa inashambulia nothing.
Hezbollah ikaanza kutoa dozi.
Israel ikaomba umoja wa mataifa uingilie kati kwani vita imewazidia.

Israel hatimaye wakakubali kuachia wafungwa.

Hezbollah ikatembea kifua mbele huku akisema Sikh nyingine usirudie.
😂😂😂😂
Nani mshindi hapo?
Jibu ni Hezbollah

Kwa sababu.
1- Israel imekubali kuachia wafungwa.
2- Israel imezidiwa intelejensia, kumbuka kuna silaha walikuwa nazo Hezbollah, Israel imewachukua miaka 6 kujua zilipo, siku wanaenda kipiga walitumia dk 34 kupiga, kumbe Hezbollah walisha hamisha siku nyingi.
Takribani target zote Israel walichengwa(targets 83).

3-Israel gharama waliyotumia kwenye hio vita ni kubwa kuliko Hezbollah, ndege za kivita, warships, Tanks, n.k lakini walitulizwa. Tanks zilipigwa, warship iliharibiwa n.k
mkuu chanzo cha vita israel na hezbolah sio hicho fuatilia historia kwa nini hezbolah ilianzishwa, hezbolah ilianzishwa ili kupambana na israel bada ya israel kuteka maeneo ya southern lebanon, na vita zao zipo kidini zaidi so usifikiri wataacha kupigana leo wala kesho, hyo sijui kuachia wafungwa ni danganya toto .

na lengo la hezbolah na washia wenzake wote ni kuifuta israel, yani siku hezbolah akiifuta israel ndo atasema sasa kashinda vita, na ndio mana iran ahangaika ili apate nyuklia halafu afunge kwenye makombora halafu awapatie hao "vichaa" halafu ndo uone moto wake, kama unasema hiyo ya mwaka 2006 ilikua ni vita basi hujawahi ona vita wewe. hapo ni walikua wanasalimiana tu.
 
ni kweli israel hajawahi kujisahau kwenye suala la intelijinsia na ndio maana nikasema israel anasurvive pale mashariki ya kati sababu ya nguvu yake ya intelijinsia kwani ndio inaplay part kubwa sana kuliko hata nguvu yake ya kijeshi.

pili suala la kutojua intelijinsia yote ya hezbola hilo ni suala ambalo linaweza kuwepo kwani kuzidiana uwanjani hua kunakuwepo hata timu mbili zinapokua zinacheza hua zinazidiana ufundi na ndio maana zote zinaweza kufungana magoli sema hua kunakua na mshindi wa jumla anayechukua point, mfano timu inaweza fungwa goli tatu kwa moja haimaanishi ile iloyofungwa haijawa na ufundi kushindwa ile ingine lazima nayo ilikua na ufundi wake wa ziada na ndio maana iliweza kufunga lile goli moja.

tatu hezbolah sio wanamgambo kama unavyotudanganya yule ni muiran kamili aliyepo lebanon sasa ili ujue kwamba israel amemzidi akili muiran baada ya perfomance aliyoionesha kwenye vita hiyo ndo akatengeneza proxy kule syria kwa hyo iran na hezbolah nguvu yao ya kupigana wakaihamishia syria na sio israel tena. narudia tena hapo mwenye akili nani?

syria ndio ilikua kiungo ama daraja kwa iran kuweka infuence yake lebanin, kwa hyo israel akaja na strategy ya kuvunja vunja daraja, ambalo ni syria, sasa hivi syria kabaki magofu tupu mpaka pesa anatengenezewa na urusi. myahudi sio kama unavyomfikiria wewe. jamaa pale middle east huwezi kuwafanya chochote
Kwani HIZBU imekufa ?!

Mwenye akili IRAN sababu kaweka proxy puani kabisa kwahuyo myahudi hata ikitokea vita na IRAN sasa hivi ISRAEL itabidi apigane kwanza na HIZBU HAMAS na JIHAD ISLAM wapale GHAZA kabla yakuja kukutana namkubwa wao IRAN

ISRAEL kama anaakili kubwa kama IRAN akaanzishe wanamgambo wake mpakani mwa IRAN kama walivyofanya IRAN mpakani mwake[emoji23]

ISRAEL ana akili nae [emoji23]

Pia hakuna nchi inayoitambua HIZBULLAH kama ni IRAN labda nchi wewe wale niwanamgambo nawatabakia kua wanamgambo
 
Mbona hueleweki chanzo hasa cha second Lebanon war in 2006 ndio nazungumzia wewe unazungumzia chanzo cha Hezbollah kuanzishwa.
Sikuelewi.
 
Proxy wa Israel wanaitwaje?
Walianza operation zao lini?
Mkubwa wao nani?
Wana achievement IPI?
Kwa maana nijuavyo US na Israel mpaka sasa mission failed.Syria sio Libya, Iran imeweka ngumu wanadunda.
Syria inarudi.
 
Ni sawa Iran kaweka Proxy kwenye mipaka yote ya Israel, ila swali ni je mbona Iran haanzishi hyo vita.? HA HA HAA... Israel keshaanzisha vita Syri a, hawezi kwenda kuanzisha iRAN sababu yeye anadeal na wale maadui zake wanaomzunguka, SERA YA ISRAEL NI KUJILINDA DHIDI YA MAADUI WANAOMZUNGUKA NA SIO KUANZISHA VITA, NA NDIO MAANA KILA SIKU ANAUA WAIRAN NA HEZBOLAH WALIOPO NCHINI SYRIA KWA MUDA ANAOTAKA YEYE NA HAKUNA ANAYEMFANYA KITU

Iran’s Generals Are Dying in Syria

Iran: List of IRGC commanders killed in Syria - NCRI

Kama Iran angekua ana akili ina maana proxy wake ambae ni hezbolah angekua keshaivunja vunja israel kama proxy wa Israel walivyoivunja vunja syria, Nasralah kabaki tu kurusha makombora na kujificha kujificha kwenye mahandaki, sasa hapo mwenye akili nani?
 
kama huwajui proxy wa Israel, walianza lini? Mkubwa wao nani? nenda kamuulize Bashir Assad atakupa jibu kamili.

Eti SYRIA inarudi? HA HA HAA..SYRIA ile ndo kwisha habari yake sio ya leo wala kesho, na Wamshukuru sana Mrusi maana hezbolah na Iran walikalishwa chini mpaka wakaomba poo

Syria’s ruined cities will need decades, not years, to recover from war
https://www.washingtonpost.com/news...l-need-decades-not-years-to-recover-from-war/

"Even with heroic assumptions, Syria will remain weak in the near- and mid-term, and probably even a decade out or more"

Can Syria return to the regional stage?
 
Mbona hueleweki chanzo hasa cha second Lebanon war in 2006 ndio nazungumzia wewe unazungumzia chanzo cha Hezbollah kuanzishwa.
Sikuelewi.
chanzo cha
Mbona hueleweki chanzo hasa cha second Lebanon war in 2006 ndio nazungumzia wewe unazungumzia chanzo cha Hezbollah kuanzishwa.
Sikuelewi.
chanzo cha hezbolah kunzishwa ndicho kilicholeta hiyo vita, kama huelewi tulia taratibu tu dozi itakuingia...kumbuka dozi ni mara tatu kwa siku.
 
kama huwajui proxy wa Israel, walianza lini? Mkubwa wao nani? nenda kamuulize Bashir Assad atakupa jibu kamili.

Eti SYRIA inarudi? HA HA HAA..SYRIA ile ndo kwisha habari yake sio ya leo wala kesho, na Wamshukuru sana Mrusi maana hezbolah na Iran walikalishwa chini mpaka wakaomba poo

Syria’s ruined cities will need decades, not years, to recover from war
https://www.washingtonpost.com/news...l-need-decades-not-years-to-recover-from-war/

"Even with heroic assumptions, Syria will remain weak in the near- and mid-term, and probably even a decade out or more"

Can Syria return to the regional stage?
Nimekuuliza proxy wa Israel ni nani hapo Syria? Naomba jibu acha janja janja.
Nimekuuliza wamefanikisha lipi hapo Syria?
Mkubwa wao nani?
Wameanzishwa lini?

Hezbollah infos zao zipo mwanzo mwisho.
Iran walikalishwa chini lini na Israel?
Kwenye vita ya mwaka 1980 - 1988 Mbona USSR,US,Europe,Saudia,Israel e.t.c walikuwa wanampa support Iraq na bado walifeli? Iraq kuzidiwa wakaanza kupiga sumu.
UN wakaingilia kati.

USSR walikuwa na nguvu kuliko hii Russia ya sasa.
Iran achana nayo , alipewa support na Syria na Libya tu.
It doesn't matter Russia atakuwa upande gani but Iran kumtuliza Israel middle east ni uwezo wa Iran na proxy wake.

Israel na uoga wao wa kufanya mashambulizi ya kuvizia kama Al shabaab, hawana tofauti na fisi wanao kaa pembeni kuvizia nyama aliyowinda simba.
 
chanzo cha

chanzo cha hezbolah kunzishwa ndicho kilicholeta hiyo vita, kama huelewi tulia taratibu tu dozi itakuingia...kumbuka dozi ni mara tatu kwa siku.
One more question, hivi kwa nini Israel inakubali Ku recruit askari mashoga na Netanyahu anaya tetea?
 
Ni sawa Iran kaweka Proxy kwenye mipaka yote ya Israel, ila swali ni je mbona Iran haanzishi hyo vita.? HA HA HAA... Israel keshaanzisha vita Syri a, hawezi kwenda kuanzisha iRAN sababu yeye anadeal na wale maadui zake wanaomzunguka, SERA YA ISRAEL NI KUJILINDA DHIDI YA MAADUI WANAOMZUNGUKA NA SIO KUANZISHA VITA, NA NDIO MAANA KILA SIKU ANAUA WAIRAN NA HEZBOLAH WALIOPO NCHINI SYRIA KWA MUDA ANAOTAKA YEYE NA HAKUNA ANAYEMFANYA KITU

Iran’s Generals Are Dying in Syria

Iran: List of IRGC commanders killed in Syria - NCRI

Kama Iran angekua ana akili ina maana proxy wake ambae ni hezbolah angekua keshaivunja vunja israel kama proxy wa Israel walivyoivunja vunja syria, Nasralah kabaki tu kurusha makombora na kujificha kujificha kwenye mahandaki, sasa hapo mwenye akili nani?
Yaani shoga wampige Iran?
Haupo Serious.
Commanders wa Iran kufa ni matokeo ya vita.
Haya wamewaua kwani wameshinda?
Wamemtoa Assad madarakani?
Hata kama Syria ikichukua miaka 100 itarudi tu.
 
Hkika middle east kuna vikundi vingi ambavyo ni vi tiifu kwa Iran mojawapo ni Hezbollah kwa ujumla askari hao kwa ujumla katika vikosi hivyo ni zaidi ya 500,000.Hakika vita ikitokea na Iran ikavipa vifaa na mafunzo waliyowapatia Hezbollah, basi Israel itamalizwa na proxies kabla ya Iran yenyewe, kwani active personel Israel ni kama 170,000.
Hakika Israel itakuwa Ghost City.

Nawaonea huruma Israel, maana hawa Hizbulah walipo Syria kwasasa, wakija kurudi nyumbani na uzoefu mpya wa vita pengine na vifa avipyaa watakuw amoto wakuotea mbali zaidi.
 
One more question, hivi kwa nini Israel inakubali Ku recruit askari mashoga na Netanyahu anaya tetea?
ha haa haa... unachange topic... ushahamia kwa mashoga sasa mashoga wapo kila sehemu..hata iran wapo. point yako hapa ni nini?
hili hapa chini ni shoga la kiiran
1591604454536.png

1591604525983.png
 
Nawaonea huruma Israel, maana hawa Hizbulah walipo Syria kwasasa, wakija kurudi nyumbani na uzoefu mpya wa vita pengine na vifa avipyaa watakuw amoto wakuotea mbali zaidi.
watarudije wakati wanakufa kila siku huko syria? au unaongelea mizimu yao?
 
Yaani shoga wampige Iran?
Haupo Serious.
Commanders wa Iran kufa ni matokeo ya vita.
Haya wamewaua kwani wameshinda?
Wamemtoa Assad madarakani?
Hata kama Syria ikichukua miaka 100 itarudi tu.
ha ha haaa... iran yenyewe ina mashoga kibao.
Iran na hezbolah vita ile walishindwa vibaya sana na walichinjwa kama kuku urusi ndo akaenda kuwatetea... isingekua urusi sasa hivi IS wangekua wako tehran wanakula "tigo" ya ayatolah
 
Back
Top Bottom