Ni juhudi gani zifanyike, ili kumzuia Makonda asiendelee kumdhalilisha Mwenyekiti Mbowe kupitia mikutano ya kisiasa?

Ni juhudi gani zifanyike, ili kumzuia Makonda asiendelee kumdhalilisha Mwenyekiti Mbowe kupitia mikutano ya kisiasa?

Ni vizuri kukaa kimya kulinda heshima ndogo uliyobaki nayo.acha uzuzu,huyo makonda anasemaje kuhusu katiba mpya na tume huru ya uchaguzi??
1. Makonda amekuja kukumbushia, na kusimamia ilani ya chama chake.

2. Makonda anaongelea kuhusu miundombinu ya umeme, maji, barabara, shule, hospital, ajira na mambo muhimu yanayohusu maisha ya moja kwa moja ya mtanzania au binadamu yoyote.

Wapinzani wao wanapigania tu tumehuru, na katiba mpya ili waingie madarakani kuifaidi nchi. Hayo mengine yanayohusu maisha ya watanzania wengine ambao sio familia zao hayawahusu.
 
Amewekwa ili kuwahadaa wasukuma
Kwahiyo hilo la kuwahadaa wasukuma, ndo limesababisha mwamba aache kuendelea na program zake za mikutano ghafla?

Au ameacha kuendelea kutokana na yale madai ya kutafuna mamilioni ya chama kwa kisingizio cha kukodisha chopa ya kuzungukia mikutanoni?
 
Kama huzijui siasa ndo hizo sasa wewe jichanganye uone utakavyotolewa udhu.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Hakika kuna mambo ambayo yanaendelea katika faifa letu. Mambo ambayo yanadhalilisha, yanaumiza na kumvunjia heshima mtu ambae alikuwa anaonekana ana hadhi ya juu kichama, na kisiasa.

Kwa vile huyu anaedhalilishwa na kuvunjiwa heshima hana uwezo, wala ujanja wa kujitetea, acha basi sisi wengine tuje kutafuta watu ambao wataingia kazini kumtetea kiongozi huyo mkubwa wa kisiasa nchini.


Ni hivi ndugu zangu.., kabla ya katibu mwenezi wa CCM ndugu Paul Christian Makonda kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, kulikuwa na mikutano fulani ya hadhara iliyokuwa inafanywa na mwenyekiti wa Chadema taifa ndugu Freeman Mbowe.

Mikutano hiyo ilipewa jina la operation nini sijui, na ilitangazwa sana na chawa wake mwaminifu ambae sina haja ya kumtaja. Japo mikutano hiyo ilifanyika viwanjani na mitandaoni, lakini haikuonekana kuwashawishi watu wengi kuifatilia, na badala yake mwenyekiti alikuwa akijikuta anakusanya watoto wadogo na baadhi ya wanachama wake waliokosa shughuli za kufanya.

Kwa kutambua hali hiyo ilibidi mwenyekiti aongeze juhudi za kufanya mikutano yake kwa njia ya chopa, ili kuwavuta watoto na wale ambao walikuwa wanakwenda kushangaa chombo hicho cha mzungu kinavyoshuka, na kupaa angani bila kushikiliwa na kitu chochote chini.

Mikutano hiyo ya mwenyekiti ilikoma ghafla baada ya katibu mwenezi wa CCM ndugu Paul Makonda kuapishwa na kuapa kula sahani moja na mwenyekiti huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini.

Ikumbukwe kuwa raisi Samia na Makonda waliahidi kumsaidia mwenyekiti huyo kwa hali na mali ili aweze kutimiza malengo yake ya mikutano, ila kwa ahadi ya kula nae sahani moja. Akimaanisha kwamba kila atapofika Mbowe, na yeye (Makonda) atatia mguu kusafisha uchafu utakaokuwa umeachwa na Mbowe alaf wawaachie wanachi wenyewe wachague pumba na mchele.

Sasa inasikitisha kuona Mbowe amefyata, na kuogopa kuendelea na mikutano kwa visingizio visivyokuwa na maana. Mara adai anasubiri vibali vya mamlaka ya hali ya hewa, mara mvua zinanyesha kana kwamba yeye maisha yake yote hutembelea chopa tu, hawezi kutumia gari kama wenzake kina Lisu, Makonda nk.

Mikutano miwili mitatu ya Makonda imeshamvunja nguvu mwenyekiti hadi kuamua kumsubiri Lisu arudi wapambane na mtu mmoja, je hiyo 2024 na 2025, si hali itakuwa mbaya kama pale mwembe yanga au mbagala!
Maneno yamekuwa mengi sana na naona makonda kaja na upepo na anaogopwa na kila mtu, kama Rais anaona anadhalilishwa si amtoe aweke mwingine kwani kuna ubaya na katu hutokuka kusikia makonda analamba miguu ya mtu ni mtu na nusu, anajiamini kwa kila kitu.
 
Huoni Lissu katua, ni mkakati tu kuacha harufu ya kijana mchafu ipite.

Kijana Hana ADABU, anataka kuwa juu ya yote, hakitangazi chama Wala kumsafisha mkt, anatafuta sifa binafsi.
Makonda ameonesha kumuunga mkono kwa dhati raisi Samia kwa kuwambia wana Geita kwamba "anaempinga raisi Samia anampinga Magufuli".

Hivyo kwa vile wana Geita walimsapoti raisi Magufuli enzi za uhai wake, basi wamsapoti pia na raisi Samia.

Hii ni tofauti na Lisu ambae toka kipindi kile cha uchaguzi mkuu aliporudi kugombea uraisi kupitia chama chake, alitumia muda mwingi kuelezea matatizo yake binafsi ya kupigwa risasi, sijui kunyimwa stahiki zake za ubunge nk, huku akisahau kwamba wananchi huwa wanafika katika mikutano ya vyama kusikiliza sera na njia mbadala za kutatua kero zao. Sio kila kukicha kuzungumzia habari za kupigwa risasi na kutaka uraia pacha uruhusiwe ili iwe rahisi watoto wake waliopo uhaibuni nao waje kugombea na nyinyi kina kabwela mbaki kuwa chawa wa mitandaoni tu, sio kupewa nafasi ya kugombea.
 
Chawa wake yule Erythrocyte anasemaje?
Chawa wake kwa sasa hana kazi yoyote. Yeye hulipwa pale tu mwenyekiti anapokuwa katika mikutano, au kuzunguka yake ya hapa na pale ya kisiasa.

Sasa kwa vile mwenyekiti amestuck, basi usitarajie kupata taarifa yoyote kutoka kwa chawa huyo, maana hata hela ya bando kuipata ni shida.
 
Makonda ameonesha kumuunga mkono kwa dhati raisi Samia kwa kuwambia wana Geita kwamba "anaempiga raisi Samia anampinga Magufuli" .
Hivyo kwa vile wana Geita walimsapoti raisi Magufuli enzi za uhai wake, basi wamsapoti pia na raisi Samia.

Hii ni tofauti na Lisu ambae toka kipindi kile cha uchaguzi mkuu aliporudi kugombea uraisi kupitia chama chake, alitumia muda mwingi kuelezea matatizo yake binafsi ya kupigwa risasi, sijui kunyimwa stahiki zake za ubunge nk, huku akisahau kwamba wananchi huwa wanafika katika mikutano ya vyama kusikiliza sera na njia mbadala za kutatua kero zao. Sio kila kukicha kuzungumzia habari za kupigwa risasi na kutaka uraia pacha uruhusiwe ili iwe rahisi watoto wake waliopo uhaibuni nao waje kugombea na nyinyi kina kabwela mbaki kuwa chawa wa mitandaoni tu, sio kupewa nafasi ya kugombea.
Sijamtaja mm,

Pia mjue, wananchi Si wajinga.

Magu hakuuza bandari, mnalo.

Tusubiri.
 
Maneno yamekuwa mengi sana na naona makonda kaja na upepo na anaogopwa na kila mtu, kama Rais anaona anadhalilishwa si amtoe aweke mwingine kwani kuna ubaya na katu hutokuka kusikia makonda analamba miguu ya mtu ni mtu na nusu, anajiamini kwa kila kitu.
Naona kuna tofauti kubwa kati ya kiswahili cha Burundi na Tanzania, ndio maana imekuwa shida kuelewa nilichoandika.

Subiri warundi wenzako walioishi Tanzania, watapita kukufahamisha vizuri kilichoandikwa.

Kwa sasa hauelewi na wala haueleweki.
 
Chadema wajinga walionywa kuwa hawataweza kukubalika kama wataendelea kumchafua Magufuli ona sasa Makonda anavyokubalika Kwa kutumia jina la shujaa
Walifikiri siasa za majitaka (kuchafua majina ya watu) zilizowatoa mwaka 2006 hadi 2015, bado zingewatoa tena na sasa.

Bahati nzuri miaka inavyokwenda na mambo yanabadilika. Wale waliounga juhudi siasa za majitaka wengi wao sio wapiga kura tena wala wafuatilia siasa kutokana na lile tukio la 2015. Hivyo sasa hivi kuna new generation ambayo haina muda wa kukiunga mkono chama kupitia siasa majitaka, bali wanaunga mkono chama kupitia sera na mipango madhubuti ya kutatua kero zao.
 
kwamba wewe una ufahamu ama ndo kujidai kuwaza ki GT kumbe uharo tu

mkakati gani, ana kipi cha maana zaidi ya upumbavu
Kila mtu anauona ukweli, lkn anakwepa kuukubali ili asionekane mstaliti wa kambi (chama)

Kitendo cha mwenyekiti kustopisha operation zake ghafla baada ya Makonda kuapishwa, na kuahidi kula nae sahani moja kinamdhalilisha, kinamshushia heshima na kumfanya mwenyekiti aonekane ameisha kisiasa ndomaana anakwepa kuendelea na mikutano yake kama alivyokuwa amepanga.

Kwa kauli hiyo ya Makonda, Mbowe alitakiwa aendelee na mikutano yake ili kuuonesha umma wa watanzania kuwa Makonda si lolote, si chochote. Lakini sio kujificha, kunywea na kuja na hoja za hovyo kwa kuwaangushia jumba bovu mamlaka inayohusika na mambo ya hali ya hewa nk.
 

Attachments

  • Screenshot_20231112-071835.png
    Screenshot_20231112-071835.png
    196.7 KB · Views: 1
Kuwa Mwanaharakati/Mtetea Haki za Wanyonge Yakupasa Uwe Umejitoa Kweli Kweli Usiwe na Cha Kupoteza Hata Kifo. Kizazi hiki hakuna tena wale wanaume wa shoka kina Ernesto Che Guevara, Martin Lumumba, Malcolm X na wengineo waliojitolea maisha yao kuipambania Afrika. Wanaharakati tuliokuwa nao sasa Ni Uchwara wapo kimaslai zaidi alafu Waoga kama Kunguru. Pathetic
 
Back
Top Bottom