Ni kama Dotto Biteko kaanza kupewa heshima zaidi ya uwaziri mkuu kuzidi Majaliwa, hii haiwezi kuleta msuguano?


Je unajua walinzi wa PM wapo wangapi mpaka unaona kuwa VPM anaulinzi mkali kuliko? Au umewaona hao wenye suti ndiyo ukajua ni walinzi wote ? nimeangalia clip haraka nimwaona kama 6 wengine hapo siyo lazima wawe ni walinzi kuna katibu wake . Pili unapozungumzia ulinzi inategemea pia ni mazingira yapi na siyo lazima wote wavae suti kama ulivyofikiria. Sasa niambie PM anakwenda JNICC unadhani watakuwa walinzi 10 tu? PM anaenda Ofisini kwake unategemea atakuwa na walinzi 20? PM ananeda sehemu yenye mkusanyiko Mkubwa unategemea awe na walinzi 10?

Pili ulinzi unashirikisha hata polisina kikosi cha ulinzi wa viongozi. Kuna advance team ambao siyo rahisi kuwajua so usije dhania kuwa sijui ulinzi wa huyu ni mkubwa kamzidi huyu hakuna anayejua.
Nimeona hii topic leo imetrend sana , ila kumbuka huyu ni Naibu waziri mkuu kutokana na cheo chake anastahili ulinzi.
 
Hakuna msuguwano, nahisi hali ya kiafya ya Majaliwa siyo nzuri, anahitaji sana usaidizi.
 
Huu mchezo ni mbinu ya kutupata sisi wa kanda ya ziwa lakini tuna akili nyingi kuliko waliobuni hii mbinu ya kitoto,kifupi ni kuwa hatudanganyiki. Haya matusi na dharau toka Zanzibar yamezidi kutufumbua macho Watanganyika.
 
Ni utapanyaji wa fedha za umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…