Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Tatizo lako ni yale maagano ya kuungana na kuwa mwili mmoja, utabakije nusu mwili? Hivyo mme au mke ni muhimu zaidi.
 
Kweli kabisaa ila ni depression anayopitia inamfanya aseme huo ujingaa ila mzazi anaumaa hata kama iwe unajitegemea kimaishaa.
 
Pole sana mkuu...!
 
Maumivu ya kuondokewa na mzazi hayapimiki aisee, binafsi yananitafuna ndani kwa ndani, sijawahi kupata relief.
Mama yangu haipiti siku sijamuwazaaa..[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] Hapana aiseee kifo kitu kibayaa sanaa
 
Umemaliza.
 
Haya ndo matatizo ya kuwa na mke mmoja, ungekuwa na mke wa pili au hata mchepuko huenda usingeathirika kwa kiwango kikubwa.

Wazungu wametuharibia sana na tamaduni zao za mke mmoja kuja kuzipandikiza kwetu kupitia dini na kupitia sheria za ndoa.

Wanaume wajue kwamba wao wanaathirika zaidi kumpoteza mwenza kuliko wanawake wanavyoathirika kumpoteza mme.

Kwa hiyo tamaduni zetu zilitoa mwanya wa mwanaume kujilinda na hali hiyo kwa kuwa na mke zaidi ya mmoja na hata itakapotokea mke ni mjamzito au ni mgonjwa bado mwanaume hawezi kuathirika kwani mke mwingine yupo.

Haya tuendelee kufuata mambo ya kizungu, imagine huyu mtu mwaka wa nne bado ameshindwa kukaa sawa.​
 
Watoto wakikua wataelewa , halafu kwao ni rahisi sana ku move on,
Kuna baadhi yetu wanawake zetu ni mihimili flani ya mipango yetu , akiondoka unakuta hata baadhi ya mambo yanafeli.
Imagine mke anajua hadi biashara zako na wadeni wako na hadi mambo sensitive halafu aondoke ndo kinachompata mtoa mada , ni hali ngumu sana .
 
Nikweli kabisa, mtu akishapata mwenza kaoa au kuolewa ule ukaribu wa ndugu au wazazi hupungua hata mawasiliano hupungua, mzazi utawaailiana naye mara 1 au 2 kwa siku lakini mpenzi hata mara mia na haukinai kabisa.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hapa nimekuelewa

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Polee kwani bado hujapata mke? Si umeshaoa ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…