Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Mkuu mkuu usikufuru kama hauoni umuhimu wa mzazi potezea na sio kuanza kumuombea kifo kisa mtu uliyekutana nae ukubwani. Mzazi ana umuhimu wake na mke,mume ana umuhimu wake pia. Jambo usilolijua au kulifahamu asilimia kubwa ya wanawake wapo tayari kumpoteza Mume na sio mtoto au mzazi wazazi wake.

Pole kwa msiba
Maneno mazito hayo!

Mkuu natambua upweke ndio janga kubwa KWA sisi wanaume!

Mwanamke yupo tayari aishi na WATOTO wake kama tu mwanamme umeshajenga nyumba !

WANAWAKE ni wabinafsi sana huku wanamme tukisumbuliwa na tamaa!!!!

Jamaa atafute mwanamke mwingine tu!!!!
 
Kama bado wazazi wako wapo hai, endelea kuwaombea sana Mwenyezi Mungu azidi kuwatunza,, baraka walizobeba wazazi wako kwenye maisha yako ni kubwa sana,, all in all pole sana kwa kilichokutokea.
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito, nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni, nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
huezi kupata ahueni mpaka upate replacement yake, huezi
 
Pole sana mkuu Mungu akupe amani ya moyo wako.

Ila hapo kwa wazazi umezingua kdogo ma'ke wanasemaga mama na baba ndio Mungu wako wa pili baada ya Mungu wa mbinguni.
Wazazi Ni Bora kuliko hata wanao.
 
Juzi kuna clip nilikuwa nasikiliza inasema hivi

In life you must remember 3 things.

1. Remember all the people you love, they will once die, so show them love before they die.

Aliongea ya 2 na ya 3 ila hii iliniuma sana.

nikapiga picha family yangu nikamuwaza mama nilijikuta nalia nikampigia mama akapokea huku ananiimbia ( mara nyingi anafanyaga hivyo)
Nikajisemea dah ipo siku sitokuwepo au yeye hatokuwepo.
Nikawa namsikiliza tu na nyimbo zake,mara akaita, weee dada mbona naimba mwenyewe uko kimya? Nikamjibu mama niko busy nikasikia sonyo refuuuu nfyuuuxxxxxx! Kama ulikuwa busy kwa nini ulinipigia?
Akasusa akakata simu kisa alivyokuwa ananiimbia sikumpokea kwa kuimba [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ati haya yote kuna siku hayatakuwepo dah.

Kumbe alikuwa amejiunga dk zake 300 na zinakaribia kuisha muda wake[emoji1787]

Amewapigia wadogo zangu wengine hawapokei.
Mara naona ananipigia lawama kibao.

" nilijiunga dk zangu zinakaribia kuisha muda wake nawapigia akina fulani wote hawapokei ipo siku watanikumbuka, ipo siku hawataona no ya mama akiwapigia simu, siku nikifa ndo watajua umuhimu wa simu zangu[emoji28]

Nikamuuliza kwani ulitaka kuwaambia nini? eti kuwasalimia tu[emoji28] " najua mwanangu wewe hukaagi mbali na simu yako ukimaliza kazi zako nipigie" nikajua huyu hana lolote ana umbea wa huko kijijini kwetu anataka kutusimulia.

Anyway mleta mada pole sana ila na mzazi ana nafasi yake muhumu hasa ukiwa nae karibu.
Baba yupo wapi?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito, nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni, nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Pole sana
 
Kifo ni Kifo ni mtu alieondoka ambae hutokuja kuonana nae tena

huo uafadhali unatokea wapi sasa na wewe mkuu,kweli ushavurugika

afya yako ya akili inahtaji msaada mkuu,sikulaumu hata kidogo ila naweza

kusema wewe ni mgonjwa kama wagonjwa wengine unahtaji msaada na uangalizi wa karibu sana,sikupuuzi Mkuu.
 
Back
Top Bottom