Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito,nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Mkuu pole sana. Nakuelewa sana hasa kama mke ni mtu mliyekuwa mnaelewana sana. Nakumbuka wife aliwahi kulazwa cku 5 kwangu ilikuwa ni kama miaka 10. Niliteseka sana kukaa nyumba bila mke kwa mwanaume ni mtihan sana.
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito,nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Duh, Mungu wa mbinguni akupe faraja ya kweli. Kuna nyakati ukiwaangalia watoto ndio wanazidi kukumbusha na kuleta maumivu. Mmmmmghhh majaribu mengine, pole sana
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito,nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Duh! Mkuu wote muhimu mno. Labda mke au mme yakuwa nzito sababu ya zile Kuta nne. Wote inauma sis...
 
Vaa viatu vya watoto wako mkuu, waambie ni heri wao wamefiwa na mama yao kuliko wewe uliyefiwa na mke uone kama watakuelewa. Na kama huoni umuhimu wa wazazi basi maisha yako yalikuwa boarding school.

Pole sana mke anauma hasa ukiwaangalia watoto wanapomkosa mama yao. Ila jitahidi kuwa strong maisha yaendelee kwa faida ya watoto vinginevyo utawaacha kwenye ulimwengu wa peke yao.
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito,nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Kama mwezi hivi tangu afariki, nilikuwa namwona, kumbe kichaa changu tu.

Pole sana, yasikie tu kwa jirani.
 
Juzi kuna clip nilikuwa nasikiliza inasema hivi

In life you must remember 3 things.

1. Remember all the people you love, they will once die, so show them love before they die.

Aliongea ya 2 na ya 3 ila hii iliniuma sana.

nikapiga picha family yangu nikamuwaza mama nilijikuta nalia nikampigia mama akapokea huku ananiimbia ( mara nyingi anafanyaga hivyo)
Nikajisemea dah ipo siku sitokuwepo au yeye hatokuwepo.
Nikawa namsikiliza tu na nyimbo zake,mara akaita, weee dada mbona naimba mwenyewe uko kimya? Nikamjibu mama niko busy nikasikia sonyo refuuuu nfyuuuxxxxxx! Kama ulikuwa busy kwa nini ulinipigia?
Akasusa akakata simu kisa alivyokuwa ananiimbia sikumpokea kwa kuimba 🤣🤣🤣🤣
Ati haya yote kuna siku hayatakuwepo dah.

Kumbe alikuwa amejiunga dk zake 300 na zinakaribia kuisha muda wake🤣

Amewapigia wadogo zangu wengine hawapokei.
Mara naona ananipigia lawama kibao.

" nilijiunga dk zangu zinakaribia kuisha muda wake nawapigia akina fulani wote hawapokei ipo siku watanikumbuka, ipo siku hawataona no ya mama akiwapigia simu, siku nikifa ndo watajua umuhimu wa simu zangu😅

Nikamuuliza kwani ulitaka kuwaambia nini? eti kuwasalimia tu😅 " najua mwanangu wewe hukaagi mbali na simu yako ukimaliza kazi zako nipigie" nikajua huyu hana lolote ana umbea wa huko kijijini kwetu anataka kutusimulia.

Anyway mleta mada pole sana ila na mzazi ana nafasi yake muhumu hasa ukiwa nae karibu.
 
Back
Top Bottom