Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

Kuna mahali haupo sawa..au sija kuelewa.kwaio tusichepuke au?

Hapa mjadala sio kuchepuka au kutokuchepuka mkuu, tuanza kujadili Hilo tutajaza servers za JF bila kufikia makubaliano. Tupo Kwa mchepukaji anapopunguza maumivu ya usaliti Kwa kuonyesha heshima ya mwenza anapokataa kutumia Kitanda akiwa na mchepuko au kuvua Pete wakati mwili ambao ndio kitendea kazi anaukabidhi Kwa mchepuko.

Hapo ndio swali linakuja, kati ya mwili na Kitanda, kipi ni Cha Thamani Kwa mwenza?
 
Mimi nazani nikitanda.
 
Nadhani logic ni anaweza kurudi ghafla akakukuta
 
Nadhani logic ni anaweza kurudi ghafla akakukuta

Kuna Rafiki yangu yeye alikua anaishi mbali na familia yake, ni msomi mwenye nafasi ya juu kabisa tukiwa nae kazini, hii ilikua ni kanuni yake kwamba hata akipeleka mtu kwake, wanamalizana chumba Cha wageni.
Alikua mtu wa kujali sana Mila na tamaduni zao, ndio Mtu wa kwanza kumuuliza hili swali kwamba kama nafsi inamsuta kuhusu Kitanda, mwili wake sio Bora na Thamani Kwa Mke wake? Alibaki anacheka tu.

Huyu unaona kabisa suala la kurudi ghafla akafumaniwa halipo, Mke wake alikua akiishi nchi nyingine kabisa.
 
Naona umechoka🤣🤣

Hapana, ni busara kuheshimu mitazamo na maoni ya watu. Unajua licha ya kuandika chochote, amechukua muda kuusoma Uzi wako, akaamua kuandika kitu, ni busara kuthamini muda na mchango wake.

Nasubiria lipa namba usijekuwekwa rumande Kwa mangi
 
Pole sana, Umepona au Bado Moyo unajeraha?
 
🤣🤣🤣Mkuki kwa nguruwe
Amna, unajua inabidi NATURE ifanye kazi yake ndio maana waswahili wakasema MAFAHARI wawili hawawezi kaa ZIZI moja. Means wanaume wawili hawawez ishi nyumba moja na Mke mmoja, ila kwa Wanawake hata wawe kumi Mwanaume Mmoja wanaweza ishi.
 
Hapo mimi ninaona inategemeana na dhamiri. Sasa ili dhamiri isikutese unakuta unajisemea aaaah lakini sijatumia kitanda kile kile😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…