Nina 3.0 nilihakikisha tu niwezekwenda masters bila usumbufu.
Nina ushuhuda binafsi, ilitolewa quiz kipindi nipo mwaka wa kwanza nikala 2 ya 50 kikaandikiwa 'see me' kisa nilijibu kwa kitabu ambacho hakukitumia lecturer kufundishia, na hapo kozi ni sheria vitabu vingi.
Lecturer nilivyoenda muona akanichana live kuwa anajya kabisa nipo sahihi ila yeye alikuwa anataka kujua wangapi walikuwepo darasani wakati anafundisha, sababu waliokuwepo wangetaja kile kitabu alichotumia kufundishia. Aisee nilichoka nikasema sitakaa niwe serious na elimu ya chuo.
Nikawa naingia seminar tu nikitokanaendelea na mambo yangu, sikuwahi kusoma notes sababu kila kitu kilichofundishwa nilikua nakumbuka kama hadithi vile, nikawa najisomea vitabu ila kwenye mtihani najibu zile hadithi za class nkamaliza na 3.0 yangu mkononi nikaenda law school kukomaa nkatoka chapu nkawaacha wadau wa hadithi za ma lecturer pale.
Elimu ya chuo kikuu TZ ni mzozo sana.