Ni kipi humfanya mtu kupata GPA ndogo chuoni? Kati ya mwenye GPA ndogo na kubwa ni yupi ana uwezo mkubwa?

Ni kipi humfanya mtu kupata GPA ndogo chuoni? Kati ya mwenye GPA ndogo na kubwa ni yupi ana uwezo mkubwa?

Kikwete alikuwa na GPA ya 2.5 lakini amekuwa raisi Tanzania.Tunao viongozi wetu wengi na wafaham wana GPA ndogo sana
Kuwa Rai's Sio kigezo kwamba Uwe Na GPA kubwa, subir siku msukuma au Kibajaji waje kuwa Rai's ndio utaelewa somo.
 
Nina 3.0 nilihakikisha tu niwezekwenda masters bila usumbufu.

Nina ushuhuda binafsi, ilitolewa quiz kipindi nipo mwaka wa kwanza nikala 2 ya 50 kikaandikiwa 'see me' kisa nilijibu kwa kitabu ambacho hakukitumia lecturer kufundishia, na hapo kozi ni sheria vitabu vingi.

Lecturer nilivyoenda muona akanichana live kuwa anajya kabisa nipo sahihi ila yeye alikuwa anataka kujua wangapi walikuwepo darasani wakati anafundisha, sababu waliokuwepo wangetaja kile kitabu alichotumia kufundishia. Aisee nilichoka nikasema sitakaa niwe serious na elimu ya chuo.

Nikawa naingia seminar tu nikitokanaendelea na mambo yangu, sikuwahi kusoma notes sababu kila kitu kilichofundishwa nilikua nakumbuka kama hadithi vile, nikawa najisomea vitabu ila kwenye mtihani najibu zile hadithi za class nkamaliza na 3.0 yangu mkononi nikaenda law school kukomaa nkatoka chapu nkawaacha wadau wa hadithi za ma lecturer pale.

Elimu ya chuo kikuu TZ ni mzozo sana.
Umechomoa pale Lawa school dah!! We ni mwamba ,Kuna watu wako na GPA za hatar ila wanazungusha hawagraduate kila siku kuangukia pua kama wa CPA🤣🤣
 
Kwa ninavyofahamu mimi ni kuwa watu wengi wenye GPA za 2.0 - 3.4 hawa watu huwa wana akili sana ila kinachowafelisha ni kutoku copy na ku paste alichofundisha lecturer. Hawa huwa hawakariri na waadhiri wwngi wanataka mtu akariri mawazo yao

Binafsi nikiwa kwenye nafasi ya kuajiri siwezi kuajiri mtu mwenye GPA kuanzia 3.5 - 5 sababu nafahamu kabisa hao ni watu wa kukariri mambo, mifano ipo.

Nimewahi kuwa kwenye panel ya interview mahali alikuja mtu ana GPA 4.8 ya Social work akawa hajui uhusiano uliopo kati ya sheria na mambo ya social work. Alinisikitisha sana, akazidiwa na mtu mwenye diploma ya social work mwenye GPA ya 2.4 iliyomzuia kwenda degree imagine.

Na hapo watu walikuwa wameweka matumaini kwa yule mwenye GPA kali ambayo angeweza kuwa tutor wa huyu wa Diploma kama angeenda kuwa mkufunzi. Ilisikitisha sana maana hadi kazi alikosa akapata yule wa diploma ya GPA ya 2.4

Pia nmesoma na watu wana GPA kubwa ila hakuna kitu.

Huku Tz ukitengamuda ukawa unajisomea vitabu unaweza kuwa na maarifa makubwa kuliko hata watu wenye masters zao na ukawakalisha kwenye kuelezea mambo.
Kaka hujakosea hata kidogo
 
Ata hapo SUA kunawatu WanaGPA nzuri ila sasa kufanya vitendo ndio issue ,kumbe wanaingia na kartasi wengine wanaficha chooni wengine kwenye nguo za ndani aisee
 
Back
Top Bottom