Duh! kwa kifupi, zamani wanyarwanda waliishi kwa umoja. Wazungu walivyokuja, wakajaribu kuvunja ule muungano,wakashindwa. Badae wakagundua kuwa, wakitumia mfumo wa devide and rule, wanaweza. Ndipo matabaka yakaanzishwa na wabelgiji, huku yakishika nafasi ya makabila ya awali wanyarwanda waliyokuwa na yo. Waliowaita watutsi, kwa kuwa walikuwa wana mali, walipewa pia nafasi za uongozi.
Waliopewa kuitwa wahutu, ilitokana na uwezo wao kiuchumi. Mtutsi alikuwa anaweza kuwa mhutu, endapo angefilisika, na mhutu kuwa mtutsi, kama akijipata.
Baada ya kuwa na mfumo huu kwa muda mrefu, ulifanikiwa. Ndipo hapa watu walianza kupelekwa DRC,kwa ajili ya kazi kwenye mashamba ya miwa na kahawa ya wakoloni(Hapa siingii sana, ila nakuonyesha tu uhusiano wa watutsi wa Congo na Rwanda). Kipindi hicho, wanahamishwa, Rwanda ilikuwa inafika maeneo yale, kabla hazijaitwa nchi. Mipaka iliyokuja kuchorwa na wazungu, ndo iliacha sehemu ya Rwanda huko DRC, ikiwa na watu wale wale.
Baada ya kupata uhuru,kutoka kwa wabelgiji, Wahutu wakaona hatuwezi kuendelea kuongozwa, mbelgiji akamugeukia mhutu na kumtupa mtutsi.
Kipindi chote hicho,watutsi ndo walikuwa wasomi na watawala. Wahutu wakaona kutokana na umoja walio nao, hapo ni miaka ya 1956, waanze kuwaondoa kuanzia wale ambao walikuwa na elimu, kwa madai kuwa watakuja kuwageuka na kutaka kujipa madaraka tena.
Mwaka 1959, mauaji kama yale ya mwaka 1994 dhidi ya watutsi, yalifanyika,ndo ikawa mwanzo wa watutsi kukimbilia nchi jirani.
Haikuishia hapo, ndipo wakimbizi wakaingia jeshini nchini Uganda(Hawa ndo walikuja kuwa kundi la RPA), ambayo ni RDF ya sasa.
Baada ya kuwa na uzoefu wa kutosha, mwaka 1990 ndipo walipofanya jaribio la kuiondoa serikali madarakani(Ikiongozwa na Juvenal Habyarimana,ambae ni mhutu). MAkubaliano ya Arusha, aliyaisaini kwa shinikizo, na ndipo inaposemekana kikawa chanzo cha kundi lake kumuua.
Mauaji yake, hayakutegemea vita vitakuja kuchukua muda. Kitendo hicho, tarehe 7 April,1994, mida ya saa nne usiku, ndipo ndege iliyombeba na raisi wa Burundi,ilipodunguliwa, ikikalibia uwanja wa ndege,umbali kama wa Kilometa 3 tu kutua. Cha kushangaza, ndege ile ilienda kuanguka nyumbani kabisa kwa rais huyo Habyarimana.
Mida hiyo hiyo, ndipo mauaji dhidi ya watutsi yakaanza rasmi.
Lakini huko nyuma, mashuleni, kulikuwaga na sensa. Wanafunzi wanaulizwa makabila yao, na kuandaliwa orodha. Wanyarwanda walikuwa na Vitambulisho vinavyoonyesha uraia wao. Hivyo, aliekuwa haonekani kuwa mtutsi kwa sura, kama kitambulisho chake kimeandikwa ni mtutsi, nae aliuawa. Waliuwawa pia wahutu ambao hawakutaka kujiingiza katika mauwaji hayo, wengine waliwaficha watutsi.
Kuna watu pia wanadai wahutu waliokufa. Ni kweli, wapo, kwa kuuliwa na wenzao, wengine kwa kisasi cha waliouliwa ndugu zao.
Ni stori ndefu sana, hapo nimefupisha