VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,492
- 1,466
- Thread starter
-
- #41
Tafuta pia:ile movie inasisimua sometimes in April chini ya Idris Elba na Carole ๐ฅ
Nilifurahi kuwa Masisi,nikarud Bigobwe,sikuona tofauti...Nikasema Rwanda ni Kongo na Kongo ni Rwanda. ,,Africa ni MojaDuh! kwa kifupi, zamani wanyarwanda waliishi kwa umoja. Wazungu walivyokuja, wakajaribu kuvunja ule muungano,wakashindwa. Badae wakagundua kuwa, wakitumia mfumo wa devide and rule, wanaweza. Ndipo matabaka yakaanzishwa na wabelgiji, huku yakishika nafasi ya makabila ya awali wanyarwanda waliyokuwa na yo. Waliowaita watutsi, kwa kuwa walikuwa wana mali, walipewa pia nafasi za uongozi.
Waliopewa kuitwa wahutu, ilitokana na uwezo wao kiuchumi. Mtutsi alikuwa anaweza kuwa mhutu, endapo angefilisika, na mhutu kuwa mtutsi, kama akijipata.
Baada ya kuwa na mfumo huu kwa muda mrefu, ulifanikiwa. Ndipo hapa watu walianza kupelekwa DRC,kwa ajili ya kazi kwenye mashamba ya miwa na kahawa ya wakoloni(Hapa siingii sana, ila nakuonyesha tu uhusiano wa watutsi wa Congo na Rwanda). Kipindi hicho, wanahamishwa, Rwanda ilikuwa inafika maeneo yale, kabla hazijaitwa nchi. Mipaka iliyokuja kuchorwa na wazungu, ndo iliacha sehemu ya Rwanda huko DRC, ikiwa na watu wale wale.
Baada ya kupata uhuru,kutoka kwa wabelgiji, Wahutu wakaona hatuwezi kuendelea kuongozwa, mbelgiji akamugeukia mhutu na kumtupa mtutsi.
Kipindi chote hicho,watutsi ndo walikuwa wasomi na watawala. Wahutu wakaona kutokana na umoja walio nao, hapo ni miaka ya 1956, waanze kuwaondoa kuanzia wale ambao walikuwa na elimu, kwa madai kuwa watakuja kuwageuka na kutaka kujipa madaraka tena.
Mwaka 1959, mauaji kama yale ya mwaka 1994 dhidi ya watutsi, yalifanyika,ndo ikawa mwanzo wa watutsi kukimbilia nchi jirani.
Haikuishia hapo, ndipo wakimbizi wakaingia jeshini nchini Uganda(Hawa ndo walikuja kuwa kundi la RPA), ambayo ni RDF ya sasa.
Baada ya kuwa na uzoefu wa kutosha, mwaka 1990 ndipo walipofanya jaribio la kuiondoa serikali madarakani(Ikiongozwa na Juvenal Habyarimana,ambae ni mhutu). MAkubaliano ya Arusha, aliyaisaini kwa shinikizo, na ndipo inaposemekana kikawa chanzo cha kundi lake kumuua.
Mauaji yake, hayakutegemea vita vitakuja kuchukua muda. Kitendo hicho, tarehe 7 April,1994, mida ya saa nne usiku, ndipo ndege iliyombeba na raisi wa Burundi,ilipodunguliwa, ikikalibia uwanja wa ndege,umbali kama wa Kilometa 3 tu kutua. Cha kushangaza, ndege ile ilienda kuanguka nyumbani kabisa kwa rais huyo Habyarimana.
Mida hiyo hiyo, ndipo mauaji dhidi ya watutsi yakaanza rasmi.
Lakini huko nyuma, mashuleni, kulikuwaga na sensa. Wanafunzi wanaulizwa makabila yao, na kuandaliwa orodha. Wanyarwanda walikuwa na Vitambulisho vinavyoonyesha uraia wao. Hivyo, aliekuwa haonekani kuwa mtutsi kwa sura, kama kitambulisho chake kimeandikwa ni mtutsi, nae aliuawa. Waliuwawa pia wahutu ambao hawakutaka kujiingiza katika mauwaji hayo, wengine waliwaficha watutsi.
Kuna watu pia wanadai wahutu waliokufa. Ni kweli, wapo, kwa kuuliwa na wenzao, wengine kwa kisasi cha waliouliwa ndugu zao.
Ni stori ndefu sana, hapo nimefupisha
Hawachangamani hao, unawajua watutsi vizuri!?Ila kwa sasa hivi Familia nyingi zimechanganyana baadhi ndio wanabaki wao kama wao
Siyo kulazimishwa. Inaitwa hivo kwa sababu walengwa wa mauaji walikuwa watutsi. Kwa maana, watusti wasingeuwawa, hata hao wahutu wasingekufa.Kwanini kila maadhimisho yanayofanyika ni watutsi na hakuna wahutu wala watwa??Swala la pili kwanini mnalazimisha kuwa ni mauaji ya watutsi wakati waliouwawa ni watustsi na wahutu?
Hata kuoana wanaowana mkuuIla kwa sasa hivi Familia nyingi zimechanganyana baadhi ndio wanabaki wao kama wao
KAribu na wewe uuliwe.Mi naomba muendelee kuuana tu!!
Mimi sina undungu na nyie makatili warefu! Kagame akifa naomba muuuane kama mende tenaKAribu na wewe uuliwe.
Cjaelewa nini mkuu. Nauliza mbona idara na taasisi na kurugenz karibu zote zinaendeshwa na watutsi? Au nikuwekee picha na kazi zao hapaNamba 2 itakuwa hujaielewa
And you perish....Ni kumwachia MUNGU.
Aliyeanzisha mauaji ni Paul Kagame na kikundi chake cha RPF kwa kudungua ndege ya Habyarimana iliyombeba pia Rais wa Burundi Ntaryamirwa.Leo hii, kwa mara ya 31, ni kipindi ambacho nchi ya Rwanda inakumbuka mauaji dhidi ya watutsi nchini humo, yaliyofanyika rasmi mwaka 1994, April 7. Mauaji haya, kwa wengi wanayahusisha na kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa imebeba rais wa Rwanda wa kipindi hicho, Juvenal Habyarimana, na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.
Kama una swali lolote linalokupa utata kuhusu mauwaji haya, usisite kuuliza. Ntajibu kadri nijuavyo.
Tarehe kama ya leo, ndipo wanajeshi wa nchi ya Ubelgiji waliokuwa Rwanda, waliwakimbia watutsi waliokuwa wamekimbilia katika kambi yao, na kuwaacha mikononi mwa wauwaji.
Kwa namna Kagame anavyowatenga Wahutu kwenye ngazi za uongozi naamini mauaji yatakuja rudia tena. Ngoja Kagame atoke madarakani au auaweMwenyezi MUNGU. Asaidie mauaji haya, ya kutisha yasije kujirudia tena.
Muuaji si ndio yule ToluMauaji haya, kwa wengi wanayahusisha na kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa imebeba rais wa Rwanda wa kipindi hicho, Juvenal Habyarimana, na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.
AMANI iliyopo kuna "wajinga" wanatamani "KUKINUKISHA"..........Ndo maisha, tunawakumbusha na nyie kuwa kuna ujinga mwingine ukipenya, ni kiama, hivyo, amani mliyo nayo isije wafanya mjisahau
Uzuri wewe unaelewa.Wanyarwanda wana shida kubwa ya chuki iliyokithirii mfano hata humu unaweza kuona through their writings na cha ajabu wanaonekana kujuana. Ikiwa hali itaendelea hivi amani itabaki kutamkwa tuu mdomoni na sio moyoni wala kwa vitendo. Mfano ๐น๐ฟ kuna warwanda na waburundi chungu mbovu wauutu na watusi and they will never accept their own origin sasa unajiuliza wataishi vipi pamoja? Halafu humu ujinga ni mwingi genocide sio suala la mtu kama watu wavoandika hapa huu ni utafiti unaoshirikisha vyanzo tofauti ukishirkiana na United Nations (UN). Kuna genocide kibao zimekatilwa na dunia sababu hazina vigezo ni World Wide inatambulika hivyo sababu hao watusi were targeted. Poleni sana suala la ukabila linakiwa kupigwa vita bila kuoneana haya.