Dah
Kweli Kadafi (Yafeu Fula) aliuawa miezi kama nane hivi baada ya kufa binamu yake Tupac... Alipigwa risasi ya kichwa na mdogo wa Napoleon japo kuna conspiracy kibao moja wapo ikiwa yeye kujua identity ya assassin wa Tupac.
Kundi halijafa bado kuna active member wawili Young Noble na E. D. I. Mean ambao wanaendeleza legacy ya Outlawz na Pac, Hussein Fatal alifariki mwaka jana mwezi wa saba kwa ajali ya gari, Napoleon amekua ustaadh kaslimu na kamrudia Allah na sasa ni motivational speaker akitumia maisha yake kuwaelimisha watu madhara ya gangs, gang related violence including driveby shootings nk ,yule cousin wa Tupac Kastro yupo anaendelea na movement lakini kama solo artist, Komani(Mopreme Shakur) kaka yake Tupac nae anaimba bado kama solo artist, Mussolini (Big Syke) amefariki mwaka huu tarehe 5 December na Storm yule dada kasikika kwenye wimbo kama Thug passion na black Jesus kaolewa na analea familia japo kua bado ni Outlaw damuni.
Mkuu umenikosha sana.... Kiufupi nakubaliana na 2pac kwamba ain't nothing like old school hip-hop... Napenda sana oldies kuliko kila kitu.2pac anabaki kuwa best rapper na my favorite MC of all the time,umenikumbusha storm alikuwa kwenye album ya all eyez on me pamoja na member wengine wa outlawz.
Hakuna album ya 2pac ambayo sina pia hakuna nyimbo ambayo utaitaja nisiijue... I got much love for him.
Mkuu nikukumbushe kidogo na crew kama N.W.A iliyoconsist DJ yella,Dr Dre,Eazy E,Mc ren na ice cube... Kundi jingine gangstarr nikimuongelea MC guru na DJ premier.... Jingine lost boyz,naughty by nature,erick b and rakim,boogie down production,tribe called quest,Geto boyz hapa una mkuta baba la baba Scarface.
Usiku ndo nasikiliza hizo Ngoma mpaka asubuhi.nikiwaongezea na outkast,dilated people,leaders of the new school,Run Dmc,Salt N Pepa,D La Soul,Sugar hill gang hapa unakikuta kitu cha rappers delight na makundi mengine kibao nikiyataja ntajaza bila kumsahau will Smith alikua akijiita fresh prince.
Mimi niwa 96 lakin huu mziki ndo umenikaa akilini.
Duh umenifanya niongee mengi sana.