Ni kitu gani unakiona kama udhaifu wako mkubwa hasa kwenye mahusiano?

Ni kitu gani unakiona kama udhaifu wako mkubwa hasa kwenye mahusiano?

Sio mpk mahusiano ya kimapenzi ila mtu akiniomba msamaha kwa kutamka nisamehe niko dhaifu sana hata kabla hajajielezea Sana akisema tu naomba unisamehe najikuta mdogoo km piriton,, ila mie sijui kuomba msamaha kirahisi rahisi,
 
Kosa moja sikuamini tena na inakuwa imeisha io
Na nisipokuamini hata mzuka wa kukuchakata sina tena
 
Wakuu habari.

Kuna huu msemo kua hakuna aliyekamilika chini ya jua. Hivyo kila mtu ana madhaifu yake, unaweza kua unaujua udhaifu wako au huujui lakini bado utakua na mapungufu flani kadha wa kadha.

Mimi udhaifu wangu mkubwa ni u laissez faire na kua too gentleman. Mimi hua sio mtu wa kutake things serious sana, lakini pia mimi ni mnyenyekevu au mpole sana hasa kwenye mahusiano.

Hadi mama yangu aliwahi kuniambia kua wanawake watakua wananiendesha sana. Mimi hua siwezi kumgombeza mwanamke au kumkemea hata akinikosea.

Binafsi naona udhaifu wangu kwa wanawake umepitiliza kikomo ila sina jinsi ya kufanya, niko mpole sana.

Hayo ndio madhaifu yangu, wewe nini udhaifu wako hasa kwenye mahusiano.

Ahsante.
Mtu akinikosea simwambii umenikosea namchunia mazima mpaka aanze yeye kuniulizauliza
Ila kosa kubwa kadri ya ninavyolitafsiri mimi
 
Nna wivu sana na kulia lia kama mjinga, yaani nikipiga simu usipopokea , ukija kupokea unasikia kilio kuuliza ulikua unafanya nini hukupokea muda wote.ila ukinibembeleza kidogo tu fasta yameshaisha tunaendelea kuongea😂
 
Weakness yangu mm nikimpenda mtu, nampenda Ile saana kupita kiasii, na hii weakness yangu inatumiwa Kam fimbo kuniadhibu pale mwanaume anapojua nimekufa nimeoza , na kwake sipindui, nashindwa nufanyeje ili niweze kupenda kiasii.natamani mm ndo nipendwe kama ninavopenda ,matokeo yake inakuwa vise versa.
 
Nahisi weakness yangu kubwa huwa siwezi ukicheche kabisa, nikimpenda mmoja ndio basi nashindwa ile tabia ya ki ngedere kuhama hama miti hali inayopelekea usumbufu mtu akishajua nampenda kweli na kumjali sana.
Yes na mimi nina hii. Yaani kucheat naona kama ni usumbufu flani. Sipendi maisha ya kujificha ficha na kujibanana misa una watu wengi.

Sema sasa mwanamke akishajua una yeye peke yake visa vinakuwa vingi
 
Weakness yangu kuu,nahua inanigharimu napia nahitaji dawa nihizihapa ,
1.kudhania MTU niliyenae nimwema Sana nahawezi kunifanyia kitu chochote kibaya ktk mahusiano,hii nikote ktk mapenzi nakatika urafiki wakawaida Tu,
2.over expectations,juu yahuyo MTU,
3.napenda Uhuru binafsi sipendi mpenzi wangu,awe namm au kuwasiliana namm kilasekunde ,sipendi kufanyiwa uchunguzi kama kweli nnampenda au laa,nahitaji aniamini nakuniache niflow!
 
Katika jambo linalonishinda kwenye mahusiano ni hilo,la kupigiana simu kila mara,sms kwa wingi,kila unakokuwa location yako iwe inajulikana,ukowapi,unafanya nini umekula,yaan aisee siwezi kabisa.Napenda kuwa huru,kuwa na my own space,mambo ya kugandana kama luba siyawezi,na ndo maana niko singo[emoji2]
Mm nachukiwa nahali hii hua Naona kama ananichunguza as if kunajambo Baya nafanya ,napenda Uhuru binafsi napenda spacing!napenda nimummiss mpenzi wangu
 
Itabidi tumuite daktari wa kutibu hili gonjwa 'wivu ' maana linawatesa wengi ktk mahusiano yenu.
Nimezaa namwanamke anawivu Hadi magomvi yakudhuru mwili,yaani kwaukorofi ule nahalizangu zakutokua namwanamke mmoja ,sidhani kama nitatoboa,
 
Mimi udhaifu wangu ni wivu + hasira mixer kulia yaani nikipiga simu haijapokelewa roho inakua juu akijapokea baadaye naanza hadi kulia nikihisi alikua anachepuka huko then natangaza tuachane tu, baadaye hasira zikiisha ndiyo naanza kujiuliza hivi why nimemwambia tuachane wakati nampenda sana hivi ?narudi namwandikia gazeti la kumuomba msamaha tena na kusisitiza nampenda ni wivu tu wa upendo asiniache. Hamuwezi amini ila niliachwa sababu ya wivu na kulia. Nikabembeleza sana aah hakurudi ng'oo.[emoji848]

Upo kama mkewangu, dawa ya watu kama nyie ni kujishusha zaidi yenu na kubembeleza hata kama kosa ni langu.
 
Mi binafsi pombe,naipenda na yenyewe inanipenda kwanza nimetoka nayo mbali na kama kuniharibia maisha imeshaniharibia sana kiasi kwamba hata nikiiacha sasa hivi haina maana,hebu fikiria toka enzi hizo nanywea hela ya ada ndo nije niiache leo?
 
Yes na mimi nina hii. Yaani kucheat naona kama ni usumbufu flani. Sipendi maisha ya kujificha ficha na kujibanana misa una watu wengi.

Sema sasa mwanamke akishajua una yeye peke yake visa vinakuwa vingi
Drama
Ni nyingi mno
 
Back
Top Bottom