Ni kitu gani unakiona kama udhaifu wako mkubwa hasa kwenye mahusiano?

Ni kitu gani unakiona kama udhaifu wako mkubwa hasa kwenye mahusiano?

Mi sijui udomo zege au ndio udhaifu nikipenda kuhama hilo tawi kazi ipo...hata nikipondewa huyo manzi mbovu akhaaa....
 
Itakucost usipojirekebisha. Wanawake wa kiafrika ukiwa gentleman sana inakula kwako,ugentleman waachie wahindi na wazungu. Huku kwetu watasema amekukamata.

Be careful.
Hilo ndio tatizo, wanawake wa kiafrika ukiwa gentleman ni shida.
 
Siwezi kuomba msamaha kwa maneno kiufupi sina lugha nyembamba ila nikikosea nakuwa mpole bila kusema chochote na sipendi kuzungumzia jambo lilotukorofisha maana linanipa uchungu na kuomba radhi ya mdomoni siwezi bali kwavitendo zaidi.
 
Mimi upole aisee mpaka najichukia siwezi kugombeza hata nipige simu usipokee badae ukipiga siwezi kuuliza eti kwanini hujapokea simu yangu. Ila baya zaidi huwaga siku nikichoka vituko nikasema inatosha hata uje unatambaa yani sibadiligi misimamo.

Sent From Heaven
 
Ndio nilichomaanisha....kwamba mawazo yatawaua....mana inanoga umfanyie mtu kosa akuseme...akasirike kidogo
hahahhahah iyo nafahamu mtu akikusema kidogo inaleta ahueni ila ile kimya yaani ni woga balaa, huwa nawashuhudia wakinikosea wanatetemeka sana ila wala sisemi kitu.
 
Hasira za Haraka aicee pale anaponikosea,

Ila huwa haikai muda mrefu kifuani kwangu kwa kuwa mimi si mpumbavu.


Akikiri tu kukosea napotezea yanaisha na nasahau.
 
hahahhahah iyo nafahamu mtu akikusema kidogo inaleta ahueni ila ile kimya yaani ni woga balaa, huwa nawashuhudia wakinikosea wanatetemeka sana ila wala sisemi kitu.
U see....?

Usiwafanyie hivyo wenzio...utakuja kuua shauri zako
 
Nahisi weakness yangu kubwa huwa siwezi ukicheche kabisa, nikimpenda mmoja ndio basi nashindwa ile tabia ya ki ngedere kuhama hama miti hali inayopelekea usumbufu mtu akishajua nampenda kweli na kumjali sana.
Kweli mkuu umalaya hauna dili wala hauongezi chochote kwenye kipato
 
Kama mm vile yani huwa sioni sababu ya kuwa na wengi nakuwatumia nipendavyo na mbaya zaidi huwa niki care kidogo friendship mtu atawish iwe zaidi ya ivyo. Umalaya sio dili kabisa namwomba Mungu kila leo nije kumpenda mke wangu kwa moyo wote bila makandokando.
 
Kujipendekeza kwa mtu ambae haoni thamani yangu kwake! hii kitu ilinishinda bora nionekane nna kiburi tu.
 
Nimependa Mlivyofunguka, Nimejikuta Natabasamu Kwa Kila Comment Nilosoma.....JF Kamili
 
Mimi ni hasira aiseee kwenye mahusiano mtu akiniudhi tu namtema mda huo huo sinaga mambo ya kubembeleza na sijawahi jutia maamuzi yangu kumwacha mtu nikiwa na hasira na mda mwingine nakuaga cool sna ata nikosewe nakaa kimyaa yani kiufupi SISOMEKI

Mungu Ni Mwema
 
Wivu kama nkimpenda mtu alaf nakua too caring ile kutaka kuchat kila saa kutaka kuwasiliana kila mda inakua kama ni usumbufu kwa mwingne

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi hii inaniboa sana, sms za kila wakati mara; Umeshaamka, unafanya nini, umekula, unakula nini, upo na nani, mbona hujibu sms, umelala au bado n.k yani unakuwa mtumwa wa simu.
 
Mimi udhaifu wangu kiukweli Na ndio uliopelekea Mimi kuyachukia mapenz maana wanatumia nifimbo kunichapa nikipenda mwanaume nampenda kweli Na sijui Na siwezi kuzuia hisia zangu lazima atajua kuwa kweli nampenda yaani pia nina mapungufu ya wivu mama yangu uuuwwwiiii ila ukinivumilia haya unapata Upendo wote nikipenda kiukweli nataka awe huyo huyo sitaki awe namazoea Na wanawake wengine yaani Jamani kiukweli yamenishinda mapenz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom