Ni kituko kuingia mkataba wa USD billion 42 za mkopo kwa ajili ya mradi mmoja tu wa kutengeneza natural gas refinery

U
Mfano dangote amejenga oil refinery ya usd billion 18

Minaamini oil refinery ni affordable kuliko hata natura gas refinery

Na oil refinery inakupa LPG na pia bomba la mafuta la uganda litaishia Tanga kwa hiyo kupata crude oil itakua ni rahisi
Unaujua utajiri wa dangote kiasi gani na una uhakika anaweza kukopeshwa hyoo pesa...ushapitia taasisi wanaotoa mikopo kiasi hiko vigezo vyao??.
 
Miradi mikubwa duniani inafanywa na mikopo ya bank na sehemu nyingine kama ulikua hulijui ni michache sana inafanywa bila mkopo

Utajiri wa dangote hata hujafika usd billion 18 hizo fedha anazitolea wapi kama sio mkopo mambo mengine yanahitaji matumizi ya akili tu
 
For your information, dangote amekopa pesa isiyozidi USD 5.5B...hizo pesa ulizosema wametoa/wamekopa shareholders wengine.. hawezi kopeshwa hyo pesa yote dangote kwa uwezo wake.. taratibu za mikopo taasisi kubwa zina mengi na utaratibu wake,kajifunze boss
 
Point ni amekopa mbona unapenda ligi za kitoto sana
Unafikiri usd billion 5 ni ndogo
 
Unazijua lakini usd Bilioni 42 wewe, nani atukopeshe hio hela? Toka Nchi ipate Uhuru maraisi wote 6 kwa Ujumla wamekopa $34B usd halafu unasema kuna mkopo wa $42B usd?
Inakopwa vizuri tu, sio kukopa kwa mara moja. Unafahamu kiasi ambacho tumekopa kwa miaka mitano? Btw tatizo halipo hapo tatizo ni lile lile la siku zote, baada ya mradi serikali anachukua nini kutoka kwa makampuni yanayofanya extraction?

Mkataba ungekua umeshakua finalised, NWM baada ya kuingia hiyo nafasi as a minister pia ndio aligomea baadhi ya terms ambazo awali zilikua zimekubaliwa na aliyepita JM
 
Kwani hizo pesa si zipo kwenye gesi? Zitarudi kupitia gesi. Na wanaokopa si ni makampuni ya gesi yenyewe.
Mradi unategemea kuzalisha for 30 years, percent ya tutachopata hakilingani ndio maana mazungumzo yamesimama

Makampuni yanakopa unajua dhamana ni nani? Hizo financial terms ndio zimechelewesha hadi leo hapo ndio kwenye mvutano, serikali ikikubali tu imeliwa

Walichotaka kufanya ni Kama kile walichotaka kuja nacho wale wa EPC+F kwenye ujenzi wa barabara. Yaani serikali inaenda kumkopea mlandarasi binafsi, anajenga alafu anakija tena kuidai serikali kwa alochojenga kupitia mkopo wa serikali. Mbarawa hili alifeli sana.
 
Tanzania bado haija-sini mkataba wa kujenga natural gas refinery ila uko mezani mpaka sahivi

Mwanasheria wa serikali alitaka mazungumzo zaidi juu ya mkataba kwa sababu kuna mambo bado kama serikali hajaridhika nayo

Wito ni huu tunaomba serikali isi-sini huo mkataba iangalie option nyingine billion 42 ni nyingi sana kwa mradi mmoja tu na kwa nchi maskini kama Tanzania

Mfano usd billion 42 unaweza tengeneza miradi ifuatayo na itakua na faida kubwa sana
  • Aluminium smelter
  • Copper smelter
  • Pig iron smelter
  • Glass smelter
  • Spinning
  • Paper pulp
  • Oil refinery
  • Petrochemical plant
Pamoja na kuamsha swala muhimu katika mada yako, lakini inaonyesha unachanganya mambo.
Uwekezaji katika mradi huo siyo MKOPO kwa serikali..

Lakini ninakubaliana na wewe juu ya hicho kiasi cha Bilioni $42; ambacho kimeongezeka maradufu toka kiasi cha mwanzo bila kuwepo maelezo yanayo eleweka. Hizi ni njama za hao wawekezaji ili waweze kuvuna faida zaidi katika uwekezaji wao.

Huko kuchelewa unako kuzungumzia wewe, ni pamoja na uhusika wa siasa. Huyo Wakili wa Serikali aliye pelekwa hapo hivi karibuni ni maandalizi ya kuusukuma mradi huo, mara tu mambo ya kisiasa yatakapo kuwa yamepita hapo 2025.

Tutapigwa sana kama taifa baada ya 'Chura Kiziwi' kunyakuwa kwa nguvu kubaki madarakani, siyo tu kwenye mradi huo pekee.

Lakini si unajuwa kuwa Ntorya tayari ilikwisha chukuliwa na waomani. Unajuwa masharti yake yapoje huko? Hiyo ndiyo namna 'Chura Kiziwi' alivyo amua kulinajisi taifa hili, kimya kimya. Hataki kelele.
 
Hiyo miradi uliyoitaja hapo ipo kwa reserve kiasi gani katika nchi yetu ukilinganisha na gesi?
 
Inakopwa vizuri tu, sio kukopa kwa mara moja. Unafahamu kiasi ambacho tumekopa kwa miaka mitano? Btw tatizo halipo hapo tatizo ni lile lile la siku zote, baada ya mradi serikali anachukua nini kutoka kwa makampuni yanayofanya extraction?

Mkataba ungekua umeshakua finalised, NWM baada ya kuingia hiyo nafasi as a minister pia ndio aligomea baadhi ya terms ambazo awali zilikua zimekubaliwa na aliyepita JM
Achana Na miaka 5 toka nchi ipate uhuru Jumlisha Alichokopa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi Samia haifiki Dola Bilioni 42. Sgr na Stiglers zimetutoa kijasho miradi ya 3.6B usd tukahaha hadi kuchukua mikopo ya Riba kubwa. 42B usd zipo nje ya uwezo wetu let's be realistic.
 
Tanzania bado haija-sini mkataba wa kujenga natural gas refinery ila uko mezani mpaka sahivi

Mwanasheria wa serikali alitaka mazungumzo zaidi juu ya mkataba kwa sababu kuna mambo bado kama serikali hajaridhika nayo

Wito ni huu tunaomba serikali isi-sini huo mkataba iangalie option nyingine billion 42 ni nyingi sana kwa mradi mmoja tu na kwa nchi maskini kama Tanzania

Mfano usd billion 42 unaweza tengeneza miradi ifuatayo na itakua na faida kubwa sana
  • Aluminium smelter
  • Copper smelter
  • Pig iron smelter
  • Glass smelter
  • Spinning
  • Paper pulp
  • Oil refinery
  • Petrochemical plant
Sasa hivi Mwana Sheria WA Sirikali ni Nani?? Na yupi aliyetaka mzunguko zaidi ? Na yupi wapi sasa
 
Mkuu pole sana kwa kusoma masomo ya sayansi!!

Umekuja na mada nzuri sana, but maelezo hayajitoshelezi.

Umeandika as if kila mtu anaelewa kwamba Kuna mradi umekwama.
Usipofanya hivyo utapata wachangiaji wachache.

Jazia nyama.

1.Mradi tarajali uko mkoa Gani, na una ujazo cubic meter milioni ngapi, or trion ngapi.

2.Mradi uko mezani Toka lini??
Nini sababu za kukwama kutosainiwa.

3.Ni taifa gani na Kampuni ambayo inataka kutekeleza mradi???

4.Miradi mbadala uwekezaji wake shilingi ngapi?? na tija yake ikoje??

Aksante 🙏🙏
Namsaidia kujibu
1) mradi upo lindi - likongo, ujazo milion tons per year

2) mradi mezani toka enzi ya JK, wakati wa magu negotiation ilifanyika lakini inashindikana, 2021 wakati wa SSH imawa resumed na kila kitu kikaenda sawa, but after NWM appointment akasanua jambo, hapo ndio ukakwama hadi Leo hii

3) kampuni ni Equinor(formerly Statoil), Shell. Wengine ni partners Exxon, pavilion,tpdc n.k

4) Hilo anajua huyo aliyoandika
 
Achana Na miaka 5 toka nchi ipate uhuru Jumlisha Alichokopa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi Samia haifiki Dola Bilioni 42. Sgr na Stiglers zimetutoa kijasho miradi ya 3.6B usd tukahaha hadi kuchukua mikopo ya Riba kubwa. 42B usd zipo nje ya uwezo wetu let's be realistic.
Mambo hayapo hivyo ndio maana nimekuuliza unajua kwa miaka ya karibuni tumekopa kiaso gani? Unapaswa kujua hiyo $42bil haikopwi mwaka mmoja au miwili
 
Mimi naongea najuwa ni kweli gharama kubwa sana lakini sio 42B na uhakika na hilo ila sio pesa ya kitoto.
Usibishe jambo usilolijua

Mradi ni wa dola bil 42. Wala sio uongo.
Ni zaidi ya Trillioni 100.
 
Lakini mpaka sasa tunasafirisha makinikia kwenda nje inamaana kweli tunakosa 42 bilioni ya kutengeneza iyo smelter.
Lugha gongana? Hapo inazungumzwa LNG plant

Pia sio bil 42 ni dola bil 42(trillion 100+)
 
Kinyume cha hapo ni kutupigia kelele kama nzi wa chooni
Hakika.
Ndiyo maana tukawa na 'Chura Kiziwi', na kumbe washauri wake wakuu ndiyo nyinyi!

Fanya mambo gizani ili uepukane na "nzi wa chooni". That's the type of arrogance you think is going to work for you!
 
Pamoja na kuamsha swala muhimu katika mada yako, lakini inaonyesha unachanganya mambo.
Uwekezaji katika mradi huo siyo MKOPO kwa serikali..

Lakini ninakubaliana na wewe juu ya hicho kiasi cha Bilioni $42; ambacho kimeongezeka maradufu toka kiasi cha mwanzo bila kuwepo maelezo yanayo eleweka. Hizi ni njama za hao wawekezaji ili waweze kuvuna faida zaidi katika uwekezaji wao.

Huko kuchelewa unako kuzungumzia wewe, ni pamoja na uhusika wa siasa. Huyo Wakili wa Serikali aliye pelekwa hapo hivi karibuni ni maandalizi ya kuusukuma mradi huo, mara tu mambo ya kisiasa yatakapo kuwa yamepita hapo 2025.

Tutapigwa sana kama taifa baada ya 'Chura Kiziwi' kunyakuwa kwa nguvu kubaki madarakani, siyo tu kwenye mradi huo pekee.

Lakini si unajuwa kuwa Ntorya tayari ilikwisha chukuliwa na waomani. Unajuwa masharti yake yapoje huko? Hiyo ndiyo namna 'Chura Kiziwi' alivyo amua kulinajisi taifa hili, kimya kimya. Hataki kelele.
Wanachotaka kufanya Equinor ni kama walichotaka kufanya wale wa EPC+f. Serikali akae katikati kama mdhamana wa mikopo

NWM mpya nimemsifu kwenye hili maana Equinor wamemlalamikia baada ya yeye kuingia tu akasimamisha mkataba ambao ulikua ushafika mwisho bado kusaini.

From $30bil to $42bil kutoka 2015 hadi 2021 haipo sawa. So NWM ashikilie Hapo hapo. Ndani ya miaka 6 haiwezekani gharama ikaongezeka zaidi ya Trillion 30
 
Hakika.
Ndiyo maana tukawa na 'Chura Kiziwi', na kumbe washauri wake wakuu ndiyo nyinyi!

Fanya mambo gizani ili uepukane na "nzi wa chooni". That's the type of arrogance you think is going to work for you!
Sasa umejibu kitu gani? Si uweke hizo details ambazo nimeuliza? Nyie pongapinga sasa mnakuwa wendawazimu
 
Wanachotaka kufanya Equinor ni kama walichotaka kufanya wale wa EPC+f. Serikali akae katikati kama mdhamana wa mikopo

NWM mpya nimemsifu kwenye hili maana Equinor wamemlalamikia baada ya yeye kuingia tu akasimamisha mkataba ambao ulikua ushafika mwisho bado kusaini.

From $30bil to $42bil kutoka 2015 hadi 2021 haipo sawa. So NWM ashikilie Hapo hapo. Ndani ya miaka 6 haiwezekani gharama ikaongezeka zaidi ya Trillion 30
Ninakuelewa, pamoja na kutokuwa na uhakika wa unachodhani huyo NWK ataweza kukisimamia. Huyo yupo hapo kwa muda mfupi tu. Anashikilia nafasi ambayo wakati wowote anaweza kuondolewa, kupisha mipango iendelee.
Huyo NWM na wenzake wote akina Mramba na wengine, niliwaonea huruma sana walivyo onekana kuwa wanyonge wakati wanakabidhi gesi ya Ntorya kwa wajomba zetu!
Tayari Hamza ska wekwa mahali stahiki, kumaliza kazi ya hiyo gesi baada tu ya uchafuzi wa 2025.
 
Tanzania bado haija-sini mkataba wa kujenga natural gas refinery ila uko mezani mpaka sahivi

Mwanasheria wa serikali alitaka mazungumzo zaidi juu ya mkataba kwa sababu kuna mambo bado kama serikali hajaridhika nayo

Wito ni huu tunaomba serikali isi-sini huo mkataba iangalie option nyingine billion 42 ni nyingi sana kwa mradi mmoja tu na kwa nchi maskini kama Tanzania

Mfano usd billion 42 unaweza tengeneza miradi ifuatayo na itakua na faida kubwa sana
  • Aluminium smelter
  • Copper smelter
  • Pig iron smelter
  • Glass smelter
  • Spinning
  • Paper pulp
  • Oil refinery
  • Petrochemical plant
Ok, hebu analyse hizo alternatives unazozipendekeza, uwezo wa kuzalisha na gharama za uendeshaji wa zote hii unayokata na unazopendekeza.
 
Sasa umejibu kitu gani? Si uweke hizo details ambazo nimeuliza? Nyie pongapinga sasa mnakuwa wendawazimu
Nime kueleza mnavyo fanyia mambo gizani ili tusiyajue, halafu unanitaka nikupe 'details'!

"uenda wazimu" ni kufikiri kuwa wenye mali "waTanzania" hawa stahili kujulishwa mipango na namna raslimali zao zinavyo pangwa kuwaletea manufaa wenyewe; badala yake kila kitu kinafanywa kuwa siri kubwa ili kupitisha madudu yasiyo wanufaisha wenye mali.
Kama mikataba iko sawa, kuna jambo gani la siri kiasi kwamba mujiite vyura viziwi ili msisikie sauti za wananchi kuhusu mikataba hiyo.
 
Back
Top Bottom