Wakati wa Mwinyi kulikuwa IPTL, wa Mkapa kulikuwa na Bulyankuru, North Mara, na Mkwere kulikuwa na Songas. Wakati wa Negotiation kipindi hicho wananchi walipewa moyo kuwa neema inakuja.
Matokeo:
Songas: wananchi walilipa tozo kubwa ya umeme kuliko bei ya soko, serikali ikapoteza umiliki wa share na kodi, tozo na gawio vikawa nehi.
Madini: Serikali ilipewa share chini ya 2%; msamaha wa kodi wa kudumu wakapewa wawekezaji na mwisho ikatupeleka kwenye makinikia crisis.
Facts kuhusu LNG: Ni kweli initial investment cost yake ni yakutisha. Mathalan, Serikali inahitaji sio chini ya TZS trilioni 75 ili kuwekeza katika LNG. Serikali haina huo uwezo. Matokeo yake Investors wanaongeza gharama za uwekezaji hadi kufikia zaidi ya TZS trilioni 100 ili kuweka mazingira ya fursa ya kuipunja serikali kwenye share na kodi.
Hakika nawaambia, Nivigumu kwa serikali kupata deal fair katika uwekezaji wa LNG kuliko Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Kutokana na mvuto mkubwa wa ufisadi, Katika baadhi ya nchi akitokea mtu anataka deal la gesi au wese linyooke, beneficiaries kutoka pande zote, malaka na mwekezaji umwondoa katika ramani daima.
Kwa kuwa tuna uhaba wa kutisha wa wataalamu (kiuchumi na kiteknolojia - hapa simaanishi wenye vyeti bali wanaoijua hiyo sector vilivyo) na hatuna hata robo ya mtaji, ingekuwa busara tukasubiri hadi tutakapopata wajuzi (watoto wetu). Kizazi cha kwanza, cha pili na cha sasa Afrika kimeshindwa kuivusha Afrika.
Kutokana na human capital kuwa chini Tz, kwa sasa wadanchi hawajui kinachoendea na athari zake, wamelala dolo. Ila hakika nawaambia uvunaji ukianza, hawa waliolala dodo wakiona foleni za mameli makubwa zikitia nanga mtwara na kuondoka na mitungi ya gesi kwa kasi ya kutisha huku Tz ikipata nehi kwenye kodi na shares, wataamka, watahoji na wataliamsha hali itakayopelekea kutokea yale yaliyotokea Niger Delta. Hivyo, tafadhali wakubwa zetu, chukueni taadhali stahili ili deal la LNG liwe baraka na siyo laana kwa taifa. Inasisitizwa LNG siyo mradi wa mchzo mchezo haijawahi tokea nchi yeyote ya kusini mwa jangwa la sahara kuwa na deal nono la aina hiii. tukipata deal fair tutatoboa, tukitanguliza ubinafsi imekula kwetu mazima na kwa watoto/wajukuu wetu.
Note: wanaosema hela anatoa mwekezaji hivyo wananchi na serikali hawana cha kupoteza. hawajatafakari vema, hawaoni mbali, hawakumbuki ya Bulyankuru na hawana upeo sahihi kuhusu mantiki ya fedha za mwekezaji. Fedha za mwekezaji utolewewa kwa sharti la serikali na wananchi kupoteza haki zao za asili hasa share na kodi kwenye mradi husika (ndio maana huwa mikataba ya aina hiyo inafichwa kwani mkiona mtapofuka macho).
Kama Botswana wameweza kwenye Almasi kwa nini sisi tunashindwa?
Mungu awaongoze viongozi wetu mtuvushe salama kwenye LNG.