Sihitaji kusoma historia ya Libya. Wakati Gaddafi anaingia madarakani kwa kumpindua King Idris wa Benghazi nilikuwa nina miaka 10 na nilijua kilichotokea kupitia Redio.
Umemeza hadithi za uwongo kuhusu Gadaffi. Angekuwa anatakiwa asingeuliwa na watu wake
Ndio maana nikakwambia huwa sipendagi kabisa kubishana na nyie machawa, maana hamnaga kitu kichwani.
Vizuri umejitanabaisha wewe mwenyewe kwamba wakati Gaddafi anaingia madarakani mwaka 1969 ulikuwa na umri wa miaka 10 so mpaka Sasa hivi hapo ulipo wewe ni mzee wa umri wa miaka 65 na umeshuudia regimes nyingi sana za kisiasa na matukio yake hapa Afrika.
Muammar Gaddafi baada ya kushika madaraka alifuta Kila kitu ambacho kiliachwa na mfalme Idriss akianza na sera zake ambazo zilionekana kuwanufaisha Zaid ma imperialists wa ulaya hasa wabritain, alipunguza kabisa haki za uchimbaji mafuta kwa makampuni ya kingereza na serikali kuwa ndio mwenye miliki nyingi kwenye uchimbaji... Na kama hiyo haitoshi akakataa offer ya $550m kutoka kwa benki ya Uingereza akiwaambia kwamba rasilimali zilizopo Libya zinatosha kuiendesha Libya na ndio kipindi hicho hicho akafanya wide economy diversification ya Hali ya juu... Haya yote yalifanyika 1970s
Katika kipindi chote Cha utawala wa Gaddafi wanainchi wa Libya hawakuwahi kujua bill ya umeme Wala maji, elimu ilikuwa ni Bure kwa level zote, kumiliki makazi ilikuwa ni haki ya msingi ya asili ya Kila mwanainchi(natural human right), wanainchi wa Libya walipata mikopo bila riba kutoka kwenye mabenki,walitibiwa Bure kwenye hospital za pale pale Libya na kama kuna ulazima wa kwenda kutibiwa nje basi serikali ya Libya ndio iligharamikia matibabu yote na yote haya yalifanyika kwa pesa zinazotokana na rasilimali za pale pale Libya na Wala sio mikopo ya kiholela holela.
Chini ya utawala wa Gaddafi Libya haikuwahi kuwa na megenge ya uhalifu au wizi uliokithiri miongoni mwa raia.
Kwa ufupi tu ni kwamba Gaddafi alikuwa ni aina ya kiongozi mwenye akili nyingi aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuifanya Libya kuwa self-sufficient ambapo Kila Mwanainchi alinufaika na rasilimali za taifa effectively..... Haya niambie ni viongozi wangapi wa kiafrika wanaweza kufanya hivyo tukianza na Hawa tulionao hapa wa CCM?????
Viongozi wengi wa kiafrika wanachoweza kufanya ni kushirikiana na ma imperialists wa ulaya na Marekani kuzikomba rasilimali za taifa kupitia mikataba mibovu ambayo inawanufaisha viongozi hao binafs huku wakiwaacha majority ya wanainchi wakiishi kwenye umasikini wa kutisha.
Tunafahamu nyie machawa huwa hamtaki na mnatumia kuona viongozi mahiri na wazalendo wakipewa maua yao, na badala yake mnapenda sifa kama hizi ziende kwa viongozi dhaifu na wajinga wajinga wasiokuwa na hata chembe ya uzalendo wanaouza rasilimali za taifa ovyo ovyo kama Samia a.k.a Chura Kiziwi.
Na Cha mwisho licha ya uzee wako lakini unaonekana Bado una akili changa sana, nani amekwambia kuwa Gaddafi aliliuliwa na watu wake? Kwamba licha ya kuishi miaka mingi ila mpaka leo hujui kabisa mikakati ya kumuua Gaddafi ilipangwa na akina nani na ilitekelezwa vipi?? Kweli wewe ndio maana ni chawa maana hata akili ya kudadisi tu hili kujua ukweli wa mambo huna.
Kiongozi Kama Gaddafi suala la kufa lilikuwa ni given, na ilikuwa afe tangu miaka ya 1980s huko kipindi kile anapambania movement ya Pan-Arabism, lakini amewakwepa mpaka ilipofika mwaka 2011 baada ya marekani kutengeneza kundi la wapenda demokrasia feki.
Hao ma imperialists huwa wanapenda afrika iwe na viongozi dhaifu ambao watakuwa ni madalali wazuri wa rasilimali zetu na Kila wanachoambiwa wanakubali, mfano kama mama yenu ambayo wewe na machawa wenzio Kila siku huwa mnamtetea na kumpamba kwa sifa ambazo Hana.
Umewahi kujiuliza hata siku moja ni kwanini viongozi mahiri wenye elements za kizalendo huwa hawakai sana Wala kuishi muda mrefu kulinganisha na Hawa viongozi walafi na wezi kama akina mzee Kikwete na wengineo??
Tanzania kwa huge potential iliyonayo endapo kama tungekuwa na watu makini kwenye key positions za kuamua mustakabali mzima wa taifa letu, basi walau wanainchi wake tungeweza kuishi hata nusu tu ya aina ya maisha walioishi walibya kipindi Cha Gaddafi....umetolewa mfano wa Saud Arabia hapo kwamba familia ya kifalme imejitahidi sana kufanya maisha ya wanainchi wa Saud yawe Bora kiasi kwamba hawatamani hata kuwabugudhi watawala wa taifa Hilo kama ambavyo sisi Kila siku tunashinda mitandaoni humu kuwasema na kuwalaani viongozi muda mwingine mpaka kuwaombea vifo.