Hakuna kitakacho Baki kwani kila Nafsi itaonja umauti na hata yeye mtoa roho pia hatobakia.... Na hii ni kwa wale waliomini wakakatazana amabaya na kuamrishana mema (Islam)
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]
Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:
كُلُّشَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ
((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]
Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((كُلُّمَنْ عَلَيْهَا فَانٍ)) ((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُوالْجَلَالِ وَالْإِكْرَام))
((Kila kilioko juu Yake kitatoweka)) ((Na Atabakia Mwenyewe Mola wakoMwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]
Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى.Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,