Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Mcanada

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
982
Reaction score
1,942
Habari zenu wananchi wa Taifa la JamiiForums, leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and downs nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo.

Wakati nipo chuo mwaka wa tatu UDSM huko Tanzania nikipiga zangu Computer Science nilipata mchongo Nokia Siemens kuna mradi wa kusimika minara walikuwa wakifanya na walihitaji watu competent kwenye eneo la Network Systems nikapewa hiyo connection na nilipiga kazi kama mwaka hivi hela ilikuwa tamu ila bahati mbaya kuna rafiki yangu wa karibu sana (family friend) alipata majanga ya kifamilia kodi nyumbani ilimuishia.

Michongo alikuwa hana na mke wake alikuwa akiumwa sana aliniomba nimsaidie amalize suala lake la kodi nikamsaidia lakini baadae aliniomba nimkopeshe kama milioni 12 aende morogoro akafanye mishe za kilimo ila ndani ya miezi 7 atakuwa kasharejesha yote so kwasababu ya ukaribu wetu na jinsi nilivyomfahamu way back sikuwa na shaka na ombi lake..

Dah niliingia benki nikamtolea milioni 12 akanishukuru akasepa yaani toka nimempa hiyo pesa sikuwahi kummwona tena maishani nilimtafuta sana baadae hata mke wake naye akawa hapatikani nilienda kwao kupeleka malalamiko yangu lakini ni kama walinipoza tu kwa maneno mwisho nikachoka na kuamua kupotezea ila iliniuma hii mistake.. usimuamini kiumbe anayeitwa mtu kupita kiasi..

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha nyuma cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze ili wasikosee?
 
Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.

Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.

Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.

Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
 
Hata Mimi nilichelewa kuijua kweli.

Nimeokoka na kumjua Mungu nikiwa na miaka 20. Sasa Nina miaka 10 ya wakovu.

Mjueni sana Mungu Ili muwe na Amani ndivyo Mema yatakavyowapata.
Ayubu20:21.

Wakujue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristu uliyemtuma.
Yohana 17:3
 
Back
Top Bottom