Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

1. Kutokupata kumaliza degree kwa muda maalum accordingly.
Nilipostpone Masomo kisa biashara. Na nilikua nimeshafika mwaka wa pili.
Nikarudi miaka miwili baadae , nilisoma kwa shida , nikamaliza kwa shida. kama una nafasi ya kusoma soma muda huo kijana usicheze na muda.


2. Ukiona unaweza kuzaa au kuzalisha. Zalisha mtu sahihi. Tuliza kichwa. Majuto yake ni hatari, haswa kama hujajipanga. Though upande wangu nilijuta kuzaa na mwanamke aliyekua wakupita tu. Nikaachana na chuma nilichokua mimekielewa na nilikua tayari nimeshawekeza maisha yangu, nilipoteza mwanamke na mali.
Nilianza upya maisha. kijana jitahidi sana hisia, kupunguza, jitahidi sana uzae ukiwa na mipango na maamuzi yako binafsi si ya rafiki wala mpenzi wako.

3. Ukipata hela miradi na mipango ni mingi usisubiri kwamba utaja pata mbeleni. Hicho ndicho chenyewe. Niliwahi pata hela nyingi sana nikiwa bado 20-25 nikachezea sana.
Nilipata shida sana kuzipata after miaka hiyo, bata la kila aina. Wanawake, roadtrips na marafika starehe za sinza zilinikoma. Kijana kua makini na starehe, fany huku unawekeza. Laki ni pesa kubwa sana.

4. Na mwisho, ujanja ujanja, umenicost sana, mbele ya wazazi ndugu na marafiki, kijana usiwe much know. Hii hupoteza sana muda, uwongo. Umenicost sana. Kijana jitahidi sana hapo.

Zaidi Thread tamu sana hii.
 
Kuamini ana chura kufika ndani kumbe kavaa kigodoro.
255624176250_status_273393a4ec884f819199aaa137325c62.jpg
 
Daa nina makosa hadi najiona paka,,

Kuchagua kutanyia kazi wilaya ya nyumbani(unaogopa kuchanganyikana)

Kujiunga vicoba,saccos

kuoa kwa kuvuta/pasi kushirikisha

kuoa mapema

Kukopa pesa ndefu

Kubeti pesa ndefu tena kwa wachina(mbaya mnoo)!!

Kumpa uhuru sana mwanamke(mke wangu)

Kukubali kesi(ilikuwa inanikabiri) iishe ili twende kwenye bargain!!(bora ningekaza)!!

kutokupenda kusali,kujumuika na waumini!!
Ila we jamaa ulizidi ujinga daah
 
Habari zenu wananchi wa Taifa la Jamii Forum, Leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and down nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo, Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze wasikosee ?
Hakuna zaidi ya kuanza kubeti
 
Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.

Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.

Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.

Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
Honest comment..sina cha kuongezea brother japo manufaa utakuja yaona hapo mbele na sio mbali kama utaendelea kupambana kiume ila kiukwel family za mapema ni hatar 😂😂
 
Back
Top Bottom