Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Habari zenu wananchi wa Taifa la JamiiForums, leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and downs nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo.

Wakati nipo chuo mwaka wa tatu UDSM huko Tanzania nikipiga zangu Computer Science nilipata mchongo Nokia Siemens kuna mradi wa kusimika minara walikuwa wakifanya na walihitaji watu competent kwenye eneo la Network Systems nikapewa hiyo connection na nilipiga kazi kama mwaka hivi hela ilikuwa tamu ila bahati mbaya kuna rafiki yangu wa karibu sana (family friend) alipata majanga ya kifamilia kodi nyumbani ilimuishia.

Michongo alikuwa hana na mke wake alikuwa akiumwa sana aliniomba nimsaidie amalize suala lake la kodi nikamsaidia lakini baadae aliniomba nimkopeshe kama milioni 12 aende morogoro akafanye mishe za kilimo ila ndani ya miezi 7 atakuwa kasharejesha yote so kwasababu ya ukaribu wetu na jinsi nilivyomfahamu way back sikuwa na shaka na ombi lake..

Dah niliingia benki nikamtolea milioni 12 akanishukuru akasepa yaani toka nimempa hiyo pesa sikuwahi kummwona tena maishani nilimtafuta sana baadae hata mke wake naye akawa hapatikani nilienda kwao kupeleka malalamiko yangu lakini ni kama walinipoza tu kwa maneno mwisho nikachoka na kuamua kupotezea ila iliniuma hii mistake.. usimuamini kiumbe anayeitwa mtu kupita kiasi..

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha nyuma cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze ili wasikosee?
Ndoa....
 
Najuta kuzaliwa afadhali nisingezaliwa mateso juu ya mateso
miaka 10 sasa naumwa ugonjwa usioeleweka sijui ni kansa ya ngozi ?
Nikienda hospitali madoctor wanasema siyo kansa napewa madawa tu siponi
namuomba Mungu achukue maisha yangu au aniponye lakini hakuna hata moja linalotokea
kweli dunia jalala
Kumuomba Mungu kuna taratibu zake mkuu,watafute watumishi wa Mungu walio vizuri,wakuongoze katika misingi mizuri ya kiroho,ungekuwa umesimama vizuri usingeongea hayo,unapoteza tumaini wakati Mungu wetu hana linalomshinda.'Yak.4:3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu'.Mtafute Mungu kwa kumaanisha utakuja kunishukuru...
 
Back
Top Bottom